Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Rais yupo sahihi. Ni hela ya Tanzania na sio Tanganyika. Tanganyika haina Tanganyika Revenue Authority. Ni hela iliyokusanywa na Tanzania Revenue Authority ambayo baadhi ya mapato yanatokea Zanzibar.
Ni mpaka Tanganyika iwe na institutions zake ndio inaweza claim kitu flani ni chake! So far, we shut up
Kwahiyo fungu moja la fedha zipelekwe Zanzibar na jingine Tanganyika au Tanzania? Kwasababu Tanganyika haina mamlaka ya mapato?
 
Unaposema Tanganyika iliungana na nchi ya zanzibar kwa hiari yake Je nchi ya zanzibar haikuungana na nchi ya tanganyika kwa hiari yake? Unapojibu weka unafiki pembeni.
Hatamu za muungano zipo Tanganyika, Zanzibar kote kumetapakaa vichogo/majeshi kutoka Tanganyika, kama 50-50 imekuwa nongwa basi vunjeni muungano mkaungane na Algeria nchi kubwa mwenzenu.,

Unapokuja kwenye mgao na faida ya muungano huwezi kumuangalia mshiriki mwenza wako kwa udogo wake sababu nchi 2 huru ziliungana.
 
Mama hakusema wazigawe 50% kwa 50% amesema wazigawe kwa usawa , sasa Dr. Mpango anajuwa usawa ni upi
Nchi 2 huru ziliungana, hiyo theory yenu haileti mantik yoyote kama muliungana kwa bahati mbaya na nchi ndogo vunjeni muungano, hatamu za muungano zote ziko Tanganyika, Wazanzibar wataenda kuungana ata na Comoro ikibidi au watajitegemea
 
Nakumbuka sherehe ya muungano ya mwaka juzi.fedha zake zilienda kujenga Mwanza barabara ya lami iendayo Airport
...Jpm tutamkumbuka kwa mengi..uzalendo kwanza nyumbani..[emoji2211]
 
Nchi 2 huru ziliungana, hiyo theory yenu haileti mantik yoyote kama muliungana kwa bahati mbaya na nchi ndogo vunjeni muungano, hatamu za muungano zote ziko Tanganyika, Wazanzibar wataenda kuungana ata na Comoro ikibidi au watajitegemea
Ndo mjue kuwa hakuna atakaeweza kumlidhisha kila mtu..!! Malalamiko yataendelea kuwepo tu.
 
Nakumbuka sherehe ya muungano ya mwaka juzi.fedha zake zilienda kujenga Mwanza barabara ya lami iendayo Airport
...Jpm tutamkumbuka kwa mengi..uzalendo kwanza nyumbani..[emoji2211]
Hivi kuna mapato yanakusanywa Zanzibar ambayo yanakuja kwenye kapu kuu la Taifa?
 
Hivi kule visiwa vya mafia kwenye huu mgao wanakua upande upi.

Bara au Zanzibar?
 
Nchi 2 huru ziliungana, hiyo theory yenu haileti mantik yoyote kama muliungana kwa bahati mbaya na nchi ndogo vunjeni muungano, hatamu za muungano zote ziko Tanganyika, Wazanzibar wataenda kuungana ata na Comoro ikibidi au watajitegemea
Nimepata jambo hapa
Screenshot_20210426-112538.jpg
 
Ndo mjue kuwa hakuna atakaeweza kumlidhisha kila mtu..!! Malalamiko yataendelea kuwepo tu.
Hakun ulazima wa malalamiko Zanzibar na Tanganyika sio nchi za kwanza kuungana., kuna miungano kibao duniani na wanakwenda vizuri sana kwa mfano muungano wa nchi za falme ya kiarabu husikii ngongwa kama hizi na wameungana karibu nchi 8 zote wanakula bata
 
Kumbuka ni fedha ya sherehe ya Muungano hivyo zanzibar wanahusika na Wana haki kupata.miaka ya nyuma fedha yote ilikuwa inaenda mwanza kama utakumbuka ndio zilijenga barabara ya airport.mama ameamua kugawa kwa usawa zaid

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Dodoma!

Akizungumza Leo katika kongamano la Muungano jijini Dodoma, Makamu wa Raisi Dr . Philip Mpango amesema Raisi Samia Suluhu Hassan ameelekeza Fedha zilizotakiwa kutumika katika shughuli za maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zigawanywe pande hizo mbili (Tanganyika na Zanzibar) ili zikafanye shughuli za maendeleo!

Dk. Philip Mpango ametumia takribani dakika 20 kuhutubia wanakongamano na Kisha kuondoka ili aendelee na shughuli zake za Kila siku za kulijenga taifa!
View attachment 1764536
TAREHE 26 Aprili, 1964 Mataifa mawili haya ya Jamuhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar yalioungana na kuunda Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo badae ikabadilishwa na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo kila mwaka ifikapo Aprili 26, tunakumbuka siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo mwaka huu Muungano huu unatimiza miaka 57, huku ukiwa ni Muungano wa mfano na imara katika Bara la Afrika na ulimwenguni pote.
Fedha kugawanywa sawa siyo sahihi ukizingatia mahitaji ya Idadi ya watu kwa pande zote mbili , ni wazi kabisa kwamba Tanzania bara mahitaji yake ni makubwa karibia mara kumi ya mahitaji yaliyopo kule Visiwani Zanzibar.


Watanzania bara tusipoamka mapema huu Muungano ni wa kinyonyaji kwetu
 
Muliidhulumu sana Zanzibar tokea uhuru at least mama aonyeshe kwamba nchi 2 ziliungana hivo faida iwe 50-50
Huna akili wewe. Kugawana ni sawa.lakini ni lazima kutokane namna nchi zote zinavyochangia kwenye muungano na kuzingatia jiografia ya nchi zote mbili.

Kutoa mapato ya nchi moja kupeleka nchi nyingine ilhali wao wana mapato yao ambayo nchi nyingine haifadiki nayo siyo sawa. Kugawana 50 - 50 wakati nchi moja ukubwa wake sawa na mkoa mmoja, na nyingine ina mikoa zaidi ya 26 siyo sawa pia.
 
Hizo hela zimepatikana wapi? Kama znz nao walichanga basi wagawiwe....hama hawakuhusika katika kupatikana kwake basi utakua ni upendeleo wa wazi
Kuna mikoa hua inachangia pato la taifa kuliko mikoa mingine, ila likija suala la keki ya taifa wanapata sawa na mikoa isiyofanya vizuri kwenye makusanyo.
Hii ndio gharama ya kuwa taifa moja!
Zanzibar ni sehemu ya Muungano wana haki ya kupata mgao wa keki ya taifa kama Tanganyika.
Changamoto za mambo ya Muungano (union affairs) isiwe kikwazo cha mgawanyo.
 
Huu upumbavu aliuanzisha Jiwe.
Wakati wanatenga hizo fedha walikuwa wamepungukiwa akili(vichaa)?
Ni vyema wangeifuta sherehe yenyewe isisomeke kwenye kalenda
... wao (CCM) wanakuambia muungano ni miongoni mwa tunu za taifa lazima uenziwe. Kumbuka miongoni mwa "roho" za CCM ni muungano.
 
Ufafanuzi: Usahihi ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Siyo Jamhuri ya Muungano Ya Tanzania

Kwa kiingereza ni #United Republic of Tanzania na siyo #The United Republic of Tanzania

Mhesh Profesa Palamagamba Kabudi
 
Back
Top Bottom