Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Kwanini wasiache kuzitenga hizo fedha wakati wa bajeti zielekezwe sekta zingine.
 
Tulijua tu kwa kuapishwa mama samia kuwa Rais wa JMT wenye chuki na maendeleo ya Zanzibar watanyoosha vidole tu, hawa ndio wanafiki ambao siku zote huitazama Zanzibar kwa udogo wake lakini siku zote hawako tayari kuiacha Zanzibar isimame kwa miguu yake pamoja na kwamba Tanganyika iliungana na nchi ya Zanzibar kwa hiyari zake.
Kweli ndugu hawa watu wanachuki mbaya sana.miaka yote ilikuwa inatumika huku tu .kusema basi igawanywe kwao imekuwa nongwa.hawa wanaroho mbaya sana. Tupo tunaimani na mama Samia.
 
Huu upumbavu aliuanzisha Jiwe.
Wakati wanatenga hizo fedha walikuwa wamepungukiwa akili(vichaa)?
Ni vyema wangeifuta sherehe yenyewe isisomeke kwenye kalenda
Hii ni bajeti ya Mwaka 2020/2021 Ilishapitishwa kuwa kutakuwa na sherehe hizo. Mama kaamua kuondoa acha ujuaji
 
Kweli ndugu hawa watu wanachuki mbaya sana.miaka yote ilikuwa inatumika huku tu .kusema basi igawanywe kwao imekuwa nongwa.hawa wanaroho mbaya sana. Tupo tunaimani na mama Samia.

Mbona unapenda vya bure na vya kunyonga, upewe mgawo sawa kwani unachangia nini kwenye muungano?
 
huu mgawanyo haupo sawa, yaani watu milion 50+ dhidi ya watu laki 6+ ?

baada ya utawala huu nabet muungano utakua taabani maana wazanzibar watataka migao hii iendelee.
 
Rais yupo sahihi. Ni hela ya Tanzania na sio Tanganyika. Tanganyika haina Tanganyika Revenue Authority. Ni hela iliyokusanywa na Tanzania Revenue Authority ambayo baadhi ya mapato yanatokea Zanzibar.
Ni mpaka Tanganyika iwe na institutions zake ndio inaweza claim kitu flani ni chake! So far, we shut up
TRA haihusiki kabisa kule Zanzibar.

Zanzibar wanna taasisi yao ya kukusanya mapato
 
Znz ilichangia Tsh ngapi za kugharimia sherehe hizo hadi alazimishe zigawanywe sawa?
 
Dodoma!

Akizungumza Leo katika kongamano la Muungano jijini Dodoma, Makamu wa Raisi Dr . Philip Mpango amesema Raisi Samia Suluhu Hassan ameelekeza Fedha zilizotakiwa kutumika katika shughuli za maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zigawanywe pande hizo mbili (Tanganyika na Zanzibar) ili zikafanye shughuli za maendeleo!

Dk. Philip Mpango ametumia takribani dakika 20 kuhutubia wanakongamano na Kisha kuondoka ili aendelee na shughuli zake za Kila siku za kulijenga taifa!
View attachment 1764536
TAREHE 26 Aprili, 1964 Mataifa mawili haya ya Jamuhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar yalioungana na kuunda Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo badae ikabadilishwa na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo kila mwaka ifikapo Aprili 26, tunakumbuka siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo mwaka huu Muungano huu unatimiza miaka 57, huku ukiwa ni Muungano wa mfano na imara katika Bara la Afrika na ulimwenguni pote.
View attachment 1764577
Hizo fedha kiasi gani? Na zinatokana na nini? Tunagawana sawa kwa vigezo gani? Kwà kuangalia idadi ya watu au ukubwa wa eneo?
 
Kwanini Tanganyika pamoja na udogo wa Zanzibar lakini ilikubali kuungana?? Kwanini mchonga meno hakuiunganisha Tanganyika na Algeria ama Nigeria nchi kubwa mwenzake??
Napata shaka juu ya Akili yako kama iko sawasawa. Rudia uandikacho
 
Salaam

Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Philip Isdor Mpango, amesmea kuwa, Rais Samia kaagiza fedha zilizotengwa kugharamia Sherehe za Muungano, amezibadilishia matumizi na kuagiza zigawanywe sawa kwa bara na Visiwani.

Pia kasema kila upande utajiamulia matumizi ya fedha hizo.
Na zile ambazo wao Zanzibar walizitenga nazo tutagawana sawa kwa sawa?
 
Hatamu za muungano zipo Tanganyika, Zanzibar kote kumetapakaa vichogo/majeshi kutoka Tanganyika, kama 50-50 imekuwa nongwa basi vunjeni muungano mkaungane na Algeria nchi kubwa mwenzenu.,

Unapokuja kwenye mgao na faida ya muungano huwezi kumuangalia mshiriki mwenza wako kwa udogo wake sababu nchi 2 huru ziliungana.

Hamna anayeangalia udogo kinachoangaliwa ni alichangia nini kwa ratio ya huo udogo wake na ndicho atakachostahiki siku kuna hitaji la kugawana. Hao watu 2M Zanzabar wanatoka wapi wakati wengi wako huku Tanganyika chungu cha asali kilipo?

Huu Muungano either Tanganyika nao wapate serikali yao ambapo serikali ya Muungano itakufa kifo cha hiari ama tuwe nchi moja na serikali moja. Kwa set up ya ulivyo muungano sasa hauna maisha marefu.
 
CHATO ya mama ni ZANZIBAR duh kifungu cha 37/5 kitatutesha sana mpk 2030
 
Salaam

Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Philip Isdor Mpango, amesmea kuwa, Rais Samia kaagiza fedha zilizotengwa kugharamia Sherehe za Muungano, amezibadilishia matumizi na kuagiza zigawanywe sawa kwa bara na Visiwani.

Pia kasema kila upande utajiamulia matumizi ya fedha hizo.
Kwani zimetoka upande gani?
 
Hii ni bajeti ya Mwaka 2020/2021 Ilishapitishwa kuwa kutakuwa na sherehe hizo. Mama kaamua kuondoa acha ujuaji
Hahaa kwaiyo CAG akija kusema zilitumika nje ya bajeti tusilalamike sio?
 
Back
Top Bottom