Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Rais Samia: Fedha ambazo zingegharamia Sherehe za miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, zigawanywe sawa

Brexit ya nini mkuu fuatilia kifo cha sheikh Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar kwanini alipigwa risasi, mchonga meno alitumia ujanja kumshawishi karume aungane na Tanganyika...
Usipindishe historia.

Karume mwenyewe ndiye aliyeomba ulinzi kwa Nyerere tangu Mapinduzi ya Zanzibar, kwa sababu Zanzibar haikuwa na jeshi na Karume aliogopa Mapinduzi yatahujumiwa.
 
TRA haihusiki kabisa kule Zanzibar.

Zanzibar wanna taasisi yao ya kukusanya mapato
Aisee unaishi nchi gani? Zanzibar wanakusanya kodi 2, kodi 1 inaitwa ZRB hii kwa maendeleo ya Zanzibar lakini TRA kule Zanzibar wanakusanya kodi zinapelekwa Tanganyika kwa ajili ya maendeleo yenu.,

Kwa lugha nyepesi ili Tanganyika waishi ni lazima wazanzibar wakusanye fedha zao za karafuu kukusaidieni nyinyi huko mujengewe barabara na na izo hospitali pamoja na mishahara yenu. Washukuruni Wazanzibari, mkivunja muungano mtaumia sana Tanganyika
 
Usipindishe historia.

Karume mwenyewe ndiye aliyeomba ulinzi kwa Nyerere tangu Mapinduzi ya Zanzibar, kwa sababu Zanzibar haikuwa na jeshi na Karume aliogopa Mapinduzi yatahujumiwa.
Ungejibu swali kwanini sheikh Abeid Aman Karume alipigwa risasi? Nyerere ndio alimshawishi karume kuhusu ulinzi lakini hamtaki kuachia mnangangania mumeitawala Zanziabr
 
Nimejikuta nakumbuka Mh. Least aliyekuwa mbunge wa Nkasi!
 
TRA haihusiki kabisa kule Zanzibar.

Zanzibar wanna taasisi yao ya kukusanya mapato
TRA ipo Zanzibar na inakusanya kodi
Ukipata muda uwe unapitia kwenye katiba uisome, katika orodha ya mambo ya Muungano. Na ukipata nafasi pia nenda Zanzibar sio mbali uende kwenye ofisi zao za TRA kula ukawaulizie vizuri.
Screenshot_20210426-153005.jpg
 
Ungejibu swali kwanini sheikh Abeid Aman Karume alipigwa risasi? Nyerere ndio alimshawishi karume kuhusu ulinzi lakini hamtaki kuachia mnangangania mumeitawala Zanziabr
Karume alikuwa dikteta aliyeua watu wengi, na watu wengi walikuwa na visasi naye binafsi.

Mpaka sasa hakuna jibu lililokamilika kuhusu kwa nini alipigwa risasi, kwa sababu hata aliyemuua aliuawa.

Lakini, huwezi kuondoa habari ya visasi binafsi katika kifo cha Karume.

Hujakanusha kwamba Karume aliomba ulinzi kwa Nyerere na si kweli kwamba Nyerere ndiye aliyemshawishi Karume amlinde kama ilivyodaiwa awali.
 
Ila kama Serikali haina mpango wa kuadhimisha Sherehe za Muungano, kwanini wanatenga bajeti yake kila mwaka?

Kwanini fedha hizo in a first place zisipangiwe shughuli za maendeleo badala ya kuja kuzibadilishia gia angani ilhali kuna vifungu vingi tu vya muhimu vinakosa bajeti katika wakati wa kupanga.
Kusema ukweli hili ni jambo la kipumbavu na la kipuuzi kuwahi kufanyika na serikali......ni waTanzania wachache sana wanaowaza kwa upana kama hivi.....ubarikiwe.......
 
Rais yupo sahihi. Ni hela ya Tanzania na sio Tanganyika. Tanganyika haina Tanganyika Revenue Authority. Ni hela iliyokusanywa na Tanzania Revenue Authority ambayo baadhi ya mapato yanatokea Zanzibar.
Ni mpaka Tanganyika iwe na institutions zake ndio inaweza claim kitu flani ni chake! So far, we shut up

Hujui unaloliandika, umeandika kwa hisia zako, in practice haiko hivyo, uliza uambiwe.
 
TRA ipo Zanzibar na inakusanya kodi
Ukipata muda uwe unapitia kwenye katiba uisome, katika orodha ya mambo ya Muungano. Na ukipata nafasi pia nenda Zanzibar sio mbali uende kwenye ofisi zao za TRA kula ukawaulizie vizuri.
View attachment 1764826

Hela yote inayokusanywa na TRA Zanzibar uwa haivuki bahari wakati ile inayokusanywa na TRA Bara inavuka bahari. Huu muungano una mambo ambayo tukiyachokonoa, nadhani tunaweza kuona umauti wa muungano huu.
 
Back
Top Bottom