love life live life
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 2,584
- 3,051
Huyu kwa kusema yupo vizuri sema utekelezaji sasa mbingu na ardhi.
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumzia mauaji yaliyotokea Mtwara ambapo maafisa wa Jeshi la Polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara Mussa Hamisi ambapo Jeshi limeunda kamati kuchunguza tukio hilo.
Rais amesema haiwezekani Jeshi kutuhumiwa kisha liunde kamati ya kujichunguza lenyewe, hivyo amesema amemuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aunde kamati nyingine kuchunguza tukio hilo.
Amesema taarifa ya kamati ya polisi inayochunguza tukio hilo, italinganisha na taarifa ya kamati huru itakayoundwa na Waziri Mkuu.
Ameyasema hayo akiwa njiani akielekea Mwanza.
=======
Pia soma:
Mtwara: Maafisa Saba(7) wa Polisi wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kijana aliyekuwa akiwadai zaidi ya Tsh milioni 33.7
Mtwara: Askari Polisi mmoja kati watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara alikutwa mahabusu akiwa amejinyonga tarehe 22 Jan 2022
Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi
Polisi Tanzania limekuwa jeshi ambalo linaweza kubambika kesi kwa yeyote wamtakae na lisihojiwe na chombo chochote. Wameenda mbali wanaua mtu yeyote hasa wafanyabishara endapo wataona ana mali za kumpora,wanamuua na wanamtupa na kuchukua mali zake kwa jeuri kabisa wakijua kabisa kwamba hakuna...www.jamiiforums.com