Rais Samia: Haiwezekani jeshi lifanye mauaji na lijichunguze lenyewe

Huyu kwa kusema yupo vizuri sema utekelezaji sasa mbingu na ardhi.
 
Ndo umuhimu wa Katiba mpya inayoweza kuyaweka mambo haya kikatiba. Yaani an Oversight Committee. Tume huru inyojitegemea ili kama kuna uonevu uliofanywa na vyombo kama Polisi, basi mtu anaweza kupeleka malalamiko yake na tume ikatuma wachunguzi. Bila hivyo hizi kamati zitakuwa zinatibu DALILI tu. Ila Maradhi yatazidi.
 
Ndo hapo jambo la kuhitaji Katiba mpya unaingia. Maana kungekuwa na chombo kingine HURU cha kuwafanyia Oversight ingekmuwa vyema sana.
However, huhitaji katiba mpya kuwa na chombo huru cha kusimamia taasisi ya jeshi la polisi.
Huwezi kuwa na katiba ambayo ni exhaustive namna hiyo. Kwamba kila kitu kiwe constitutionally covered. Mambo mengine yanahitaji kutungiwa tu sheria basi
 
Watanzania ni wapumbavu sana. Juzi hapa mlikuwa mnalalamika kuwa haiwezekani JESHI LIJICHUNGUZE LENYEWE, leo Rais kaamua kuwe na tume huru ya kufanya uchunguzi huo bada mnalalamika. WAPUMBAVU
Watu wanachotaka ni kamisheni huru na ya kudumu itakayosimamia muda wote majukumu ya jeshi la polisi na sio hizi tume za muda.

Ivyo nadhani mpumbavu ni wewe ambae ata kuelewa walichosema hukuelewa
 
Unafiki mtupu, mmeshindwa kuchunguza shambulio la kiasi, mauaji ya ben sanane nk.
 
USA kuna katiba inayosimamia mambo yote haya.Bado Polisi wanafanya makosa na uoevu.
Mmomonyoko wa maadili na wahusika kutotimiza kazi zao kikamilifu na inavyotakiwa haya yasingetokea.
USA wana mfumo mzuri lakini ndio wanaongoza kwa kuwa na magereza zilizojaa wahalifu.
Hamna magic bullet ya matatizo yetu bali kila mtu atimize wajibu wake kwa uadilifu bila uonevu wala upendeleo.Sheria zifuatwe bila ubaguzi wewe ni nani na unatokea wapi.
 
Katiba mpya ndio suluhu ya haya yote na mengine mengi
 
Kama polisi msomi, analytical Sana anaitwa KAHATANO Kama sikosei alihamishiwa kuwa mkurugenzi mkuu Sumatra , he can lead jeshi la polisi
 
Watanzania ni wapumbavu sana. Juzi hapa mlikuwa mnalalamika kuwa haiwezekani JESHI LIJICHUNGUZE LENYEWE, leo Rais kaamua kuwe na tume huru ya kufanya uchunguzi huo bada mnalalamika. WAPUMBAVU
Ndugu yangu hao ndio Wabongo. Ukiwapa Ugali watalalamika, ukiwapa wali bado watakosoa na kusema ni wali sawa lakini sio wa Kyela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…