Rais Samia hapa ulikosea kidogo na sijui ni nani alikujaza Upepo na ukalisema hili

Rais Samia hapa ulikosea kidogo na sijui ni nani alikujaza Upepo na ukalisema hili

Kauli yako kuwa Balozi za Kigeni ambazo zilikemea na kutaka Uchunguzi wa Kifo cha Mzee Kibao (ukiilenga hasa Marekani) kuwa zilifanya hivyo bila ya Baraka za Marais wao umeikosea mno Kuisema.

Na ukaenda mbali zaidi kusema kuwa kama kungekuwa na baya basi hao Marais wenye Uwakilishi wao kupitia Balozi zao nchini Tanzania wao wenyewe wangekupigiia.

Yaani Rais Samia pamoja na Urais wako wote huo na hao Wasaidizi wako hujui kuwa Sauti ya Balozi mwakilishi wa nchi ni Sauti ya Rais wa hiyo nchi husika?

Kiufupi ni kwamba huna Watu wazuri wa Masuala ya Kidiplomasia kwani kama ungekuwa nao nina uhakika wasingekuruhusu Kukizungumza hiki Kituko ulichokizungumza leo.

Namalizia kwa Kukushauri tu kwamba ukitaka haya Mataifa ya Kigeni yaache ulichokimaanisha kuwa ni Kihehere chao kwa Kukemea matukio mabaya ya Utekaji na Mauwaji basi nawe hakikisha unaongoza vyema na Kuchukua hatua stahiki kwa haraka.

Na ni matumaini yangu makubwa GENTAMYCINE kuwa baada ya leo Kukerwa nao (haya Mataifa makubwa ukiilenga Marekani) kwa Kukemea matukio mabaya nchini basi hata Wewe (kama Rais) hutotembeza tena Bakuli Kwao kuwaomba Misaada mbalimbali kwakuwa kwa sasa Tanzania ilipofikia chini yako ina uwezo wa Kujitegemea yenyewe Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na tayari imeshaifikia Marekani kwa kila Kitu.

Soma Pia: Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu
Rais hana Elimu ya uraia wala diplomasia sifuri tu.
 
Nafikiri kuwasema hawa weupe, sio tatizo, ila wao hujifanya waemejisahau hivi, halafu kifuatacho, ni maumivu. Ni ukweli walitakalo lazima liwe. Ila nao weupe hupenda sana kusemea kila kitu. Mweupe ana mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu. Pamoja na matatizo yetu kadhaa,, mweupe yeyote hana uchungu na mtu mweusi.
Je, waliomuua Mzee Kibao Waafrika na Watanzania wenzetu na wale Waafrika Viongozi Mafisadi ndani ya Tanzania (Serikalini) Wao wana Uchungu kama ambavyo umesema hapa kuwa Wazungu hawana Uchungu na Sisi Waafrika?

Hovyoooooooo........!!
 
Msimtishe Bi. Mkubwa.

Tanzania is a sovereign state.

Tuna kila haki ya kufanya mambo yetu bila kuingiliwa.

Hata hivyo bado tuna mahusiano mazuri na marekani, jumuiya ya ulaya , uchina na nchi nyingine za kiafrika.

Sioni ubaya wowote Madam akiwakumbusha kuwa this is a sovereign state.
Sasa kama Tanzania ni Sovereign State inakuwaje Kutwa tu inatembeza Bakuli kwa hawa hawa Wakubwa (Marekani) ikiwemo Kuwaomba Misaada mbalimbali? Kwanini kwakuwa tayari ina Jeuri ya kuwa Sovereign State basi isijitegemee yenyewe kwa kila Kitu?

Nikiwa nawaambia Kutwa hapa JamiiForums kuwa 99.999% ya Chawa (Watetezi) wa Rais Samia hamna Akili (poor thinkers) msiwe mnabisha au mnakataa sawa?
 
rais wetu ana mesemo yake ukiitafakari unaweza kumdhania kama ana dharau flani hivi
Siyo kama ana Dharau bali ana Dharau halafu hakuna ambacho anakijua. Hivi unaweza kweli Kuwaambia Mabalozi wa nchi kuwa huwaamini wakisemacho na kwamba utawauliza Marais wa nchi zao walikotoka?

Halafu tukisema kwa sasa hatuna Mtu sahihi kama nchi badala ya Kutuelewa wenye Akili na Upeo wa mbali wanaanza Kutuchukia na hata kutukalia Vikao vya Kututeta na Kutuwahisha anakotupeleka Israeli Mtoa Roho akitutwaa.
 
Hebu tujibu hili. Vifo kwa Malaki ya watu na matatizo ya Kongo, Sudan, Libya, West Africa nk hawa weupe tunaowatetea wanahusika au wanasingiziwa ? Sasa kama upande mmoja wa Africa wamehusika kuuwa Malaki ya weusi wenzetu ili wapore mali zetu je, matamshi yao kwamba tunatekwa ni ya dhati ? Yeyote asiyetenda haki hafai. Awe mweupe au mweusi.
Huna Akili.
 
Kauli yako kuwa Balozi za Kigeni ambazo zilikemea na kutaka Uchunguzi wa Kifo cha Mzee Kibao (ukiilenga hasa Marekani) kuwa zilifanya hivyo bila ya Baraka za Marais wao umeikosea mno Kuisema.

Na ukaenda mbali zaidi kusema kuwa kama kungekuwa na baya basi hao Marais wenye Uwakilishi wao kupitia Balozi zao nchini Tanzania wao wenyewe wangekupigiia.

Yaani Rais Samia pamoja na Urais wako wote huo na hao Wasaidizi wako hujui kuwa Sauti ya Balozi mwakilishi wa nchi ni Sauti ya Rais wa hiyo nchi husika?

Kiufupi ni kwamba huna Watu wazuri wa Masuala ya Kidiplomasia kwani kama ungekuwa nao nina uhakika wasingekuruhusu Kukizungumza hiki Kituko ulichokizungumza leo.

Namalizia kwa Kukushauri tu kwamba ukitaka haya Mataifa ya Kigeni yaache ulichokimaanisha kuwa ni Kihehere chao kwa Kukemea matukio mabaya ya Utekaji na Mauwaji basi nawe hakikisha unaongoza vyema na Kuchukua hatua stahiki kwa haraka.

Na ni matumaini yangu makubwa GENTAMYCINE kuwa baada ya leo Kukerwa nao (haya Mataifa makubwa ukiilenga Marekani) kwa Kukemea matukio mabaya nchini basi hata Wewe (kama Rais) hutotembeza tena Bakuli Kwao kuwaomba Misaada mbalimbali kwakuwa kwa sasa Tanzania ilipofikia chini yako ina uwezo wa Kujitegemea yenyewe Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na tayari imeshaifikia Marekani kwa kila Kitu.

Soma Pia: Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu
Mkuu umemg'oa mtu jino bila ganzi 😛
 
Kwanza hata sijakaelewa kabisa namna kalivyokuwa kanaongea,eti kwa kofia ya amri jeshi mkuu sjui utopolo nn nin huko,sijui kufa watu kwa kutekwa ni kawaida yaan hotuba ya kijinga kabisa

Eti hatujawah kuwafundsha wao namna ya kuongoza kwann watuseme sisi wakat nchi zao zinamauaji pia,kameshasahau pia kwamba huwa kanaenda kuomba omba huko kwa wakubwa kukopa lakin wao hawajawah kuja kukopa hapa
Amiri Jeshi Mkuu kesha ongea,kilichobaki ni utekelezaji tu hakuna tena mjadala!!
 
Sasa kama Tanzania ni Sovereign State inakuwaje Kutwa tu inatembeza Bakuli kwa hawa hawa Wakubwa (Marekani) ikiwemo Kuwaomba Misaada mbalimbali? Kwanini kwakuwa tayari ina Jeuri ya kuwa Sovereign State basi isijitegemee yenyewe kwa kila Kitu?

Nikiwa nawaambia Kutwa hapa JamiiForums kuwa 99.999% ya Chawa (Watetezi) wa Rais Samia hamna Akili (poor thinkers) msiwe mnabisha au mnakataa sawa?
Kuomba msaada haimaanishi huna tena sovereignty .
 
Nafikiri mnapaswa kumshauri vizuri. Rais asijiingize kwenye malumbano na Mabalozi wa nchi za nje hususani nchi za Magharibi Kama Marekani, ni hatari Sana kwake yeye mwenyewe binafsi na kwa nchi pia. Hao watu Wana mbinu nyingi Sana za kuweza kutudhibiti na kutuhujumu au kumhujumu huyo Rais endapo kama watapenda. Uwezo huo wanao.
Achaa uwoga,sisi ni taifa huru na ni kweli hatupangiwi na beberu mambo yetu kama Nchi!!
 
Ila mlikuwa mnamnanga samia kuwa ni Rais lelemama, kwamba magufuli alikuwa kidume anawakemea mabeberu,

Sasa Samia anaendesha nchi vile alivyokuwa anaendesha magufuli tunaanza kumlaumu
Anawakemea mabeberu wanaolaani mauaji ya raia wake?

Msimamo wa utetezi huu ni nini na msimamo wa raia wanaotetewa ni nini?
 
Back
Top Bottom