Rais Samia hawezi kufanya ‘effective reforms’ kwa sababu anautaka Urais

Rais Samia hawezi kufanya ‘effective reforms’ kwa sababu anautaka Urais

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Nakumbuka Baba wa Taifa Mwal. Nyerere, miaka ya 70, Wabunge walitaka kujiongezea mishahara.

Akauliza “Nchi hii masikini, mnaotaka wawape mishahara mikubwa ni wananchi masikini, watatoa wapi hizo hela za kuwapa?”

Wakang’ang’ania. Akasema basi hili sikubaliani nalo. Twende kwa wananchi watuamulie. Akasema, nitavunja Bunge wananchi waamue nani atarudi.

Wakaufyta kwa kujua kuwa wengi wao hawatarudi.

Rais alisema atafanya reforms kubwa, Sasa Rais Samia ana guts /ubavu wa kufanya hilo? Si ataogopa kufanya reforms kwa vile CCM wenzake watakataa kumpitisha kwenye kura za kugombea Urais!

Can she dare to make substantial reforms?

Nadhani nimeeleweka
 
Nakubaliana nawe 100%

Reforms zote anazodai kuzifanya/kutaka kuzifanya kwa sasa hazitakuwa na manufaa yoyote kitaifa, anaangalia maslahi yake binafsi zaidi kuelekea 2025.

Hata hiyo Katiba Mpya wanayodai kutaka kuanzisha mchakato wake, kama wakiileta, watahakikisha inawatengenezea mazingira kwao kuendelea kubaki madarakani kwa kuweka sheria ambazo zitawasogeza karibu ili kufikia malengo yao, nothing else.

Maeneo kama Tume Huru ya uchaguzi lazima watayatengenezea sheria za kuwalinda kwa namna yoyote ile.
 
Nakumbuka Baba wa Taifa Mwal Nyerere, miaka ya 70, wabunge walitaka kujiongezea mishahara. Akasema: nchi hii masikini, mnaotaka wawape mishahara mikubwa ni wananchi masikini, watatoa wapi hizo hela za kuwapa...
Sidhani kama mama ana moyo tena wa kugombea urais 2025 sasa hivi si unaona kaacha kabisa kujipigia debe kuhusu kugombea 2025 .....sasa hivi hata kaacha kusema sema mimi mwanamke sijui wanawake wenzangu sijui tupate rais mwanamke wa kuchaguliwa ......kama hali ya mambo ikiendelea hivi hivi basi samia awezi kujitokeza kuwania urais
 
Ni mchumia tumbo, ni mbinafsi kama wwalivyo wanasiasa weengi wa kitanzania
 
Sidhani kama mama ana moyo tena wa kugombea urais 2025 sasa hivi si unaona kaacha kabisa kujipigia debe kuhusu kugombea 2025 .....sasa hivi hata kaacha kusema sema mimi mwanamke sijui wanawake wenzangu sijui tupate rais mwanamke wa kuchaguliwa ......kama hali ya mambo ikiendelea hivi hivi basi samia awezi kujitokeza kuwania urais
Sio kweli mkuu, angalia nyimbo, mapambio na maandamano mengi ya kumsifia yalivyotamalaki.
 
Mama has the right kind of ingredients kuwa rais wa nchi (hana uchu wa kifisadi, siyo power monger, etc) lakini hana msuli wa kukabiliana na mafisi wa kitaifa na kimataifa kupambania maslahi ya nchi. Pia sidhani kama ana vision yoyote kuhusu nchi. She is there kama care taker administrator.

Ila nikizoom ndani ya CCM sioni mtu yeyote bora zaidi.
 
Nakumbuka Baba wa Taifa Mwal Nyerere, miaka ya 70, wabunge walitaka kujiongezea mishahara. Akasema: nchi hii masikini, mnaotaka wawape mishahara mikubwa ni wananchi masikini, watatoa wapi hizo hela za kuwapa....
Marais waliotangulia mbele za haki (hayati Nyerere, Ben na JPM) ndio walikuwa na uwezo wa kusimamia maamuzi yao hata kama wengi wangewapinga . Ili mradi yawe kwa maslahi ya taifa.Hasa hasa JP.

Kwa sasa nchi haina muelekeo. Yeyote mwenye ushawishi akishauri jambo linatekelezwa bila kuhoji madhara yatakayojitokeza.
 
Nakumbuka Baba wa Taifa Mwal Nyerere, miaka ya 70, wabunge walitaka kujiongezea mishahara. Akasema: nchi hii masikini, mnaotaka wawape mishahara mikubwa ni wananchi masikini, watatoa wapi hizo hela za kuwapa...
Hataweza hata kidogo. CCM ni mchanganyiko wa chama cha siasa, dola na serikali. Kwa collusion hiyo, mabadiliko hayatatokea. Kila kundi hapo litataka kulinda uwepo, umathubuti na mustakabali wake yaani kuna uhafidhina wa hali ya juu.
 
Mabadiliko aliyopropose hadi sasa ni:

1. Tume huru ya Uchaguzi na mazingira bora ya kidemokrasia nchini

2. Uanzishwaji wa mchakato wa katiba mpya

3. Mabadiliko ya utendaji katika jeshi la polisi

Kama haya maproposal yana baraka za Rais na wenzake ndani ya serikali basi anaweza akafanikiwa kwa kiasi lakini kama na yeye tu anaanzisha ili kupata umaarufu wake binafsi, basi mabadiliko hayo yatakuwa ndoto. Na unajua kushindwa kunakuwaje?

Mfano: Toka kamati kuu ya CCM ipitishe azimio la kuanzisha au kuendeleza mchakato wa uandishi wa katiba mpya, nini kimeendelea? Si tumeishia kwenye press conference ya Katibu wao wa Itikadi na Uenezi, Bw. Shaka H. Shaka?

Je, CCM na serikali wapo tayari kutumbua kweli majipu yanayokwamisha yote hayo?

Je, Wapo tayari tume kuwa huru kweli?

Je, dola ipo tayari kwa aina ya Muungano unaopendekezwa na wanasiasa wa Zanzibar?

Je, wapo tayari chombo muhimu kwao kama jeshi la polisi kufanya kazi zao kwa uhuru kwa kufuata misingi ya kazi zao na katiba ya nchi?
 
Nakumbuka Baba wa Taifa Mwal Nyerere, miaka ya 70, wabunge walitaka kujiongezea mishahara. Akasema: nchi hii masikini, mnaotaka wawape mishahara mikubwa ni wananchi masikini, watatoa wapi hizo hela za kuwapa...
Kama anaishia 2025 atafanya reform yenye maana na ataiacha tanzania ikistawi sana. Tutamshukuru kwa hilo.
 
Mama has the right kind of ingredients kuwa rais wa nchi (hana uchu wa kifisadi, siyo power monger, etc) lakini hana msuli wa kukabiliana na mafisi wa kitaifa na kimataifa kupambania maslahi ya nchi. Pia sidhani kama ana vision yoyote kuhusu nchi. She is there kama care taker administrator.

Ila nikizoom ndani ya CCM sioni mtu yeyote bora zaidi.
Pamoja na mapungufu yake kwa ccm yeye ndiye ana nafuu.
 
Nakumbuka Baba wa Taifa Mwal Nyerere, miaka ya 70, wabunge walitaka kujiongezea mishahara. Akasema: nchi hii masikini, mnaotaka wawape mishahara mikubwa ni wananchi masikini, watatoa wapi hizo hela za kuwapa...
Hawezi, lakini Urais hapati tena, wawe wanaangalia Maneno ya Mungu pitia KWa watu wake, hata Mara moja moja ,hapati
 
Marais waliotangulia mbele za haki (hayati Nyerere, Ben na JPM) ndio walikuwa na uwezo wa kusimamia maamuzi yao hata kama wengi wangewapinga . Ili mradi yawe kwa maslahi ya taifa...
Nashauri askari wa usalama barabarani wapunguzwe, hah hah na wanapunguzwa ni pale mwanasiasa hata kama ni kanali mstaafu anapoingilia taaluma za wengi kwa msingi wa kisiasa, tusije anza laumu jeshi la polisi hapo baadae kwa maamuzi haya, unadhani ile miamba iliyotangulia mbele za haki ingetekeleza ushauri huu wa mtaani?

jibu ni hapana na hata mtoa hoja angeufyata, haya mambo ya kuingilia polisi ni tofautikabisa na pale akina Polepole, Bashiru walivyokuwa wanadai na kuuliza kwa mfano kwanini maji hayapatikani au kwanini jengo halijaisha. hizi amri /ushauri wa mtu asiyemhusika kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ni hatari, sijui kama Sirro angeutekeleza.
 
Back
Top Bottom