Mwanamaji
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,905
- 4,518
Ni post namba 43.Kwanini isiwe BURE kabisa? We unaonaje? Yaani Tanesco anatafuta WATEJA halafu WATEJA ndio wampe mtaji? Hili unalionaje kwa mtazamo wako? Ngoja nikukumbushe kidog in case you don't know, zamani TTCL, sorry kwanza hata kabla ya TTCL kulikua na kitu inaitwa POSTA na SIMU then ndio zikatengana mwanzoni mwa miaka ya 90, hapa tuizungumzie TTCL, ilikua ukitaka simu kwanza unabembeleza ikibidi uwe na connection lakini bado ilikua lazima ulipe hizo installation charges kama ambavyo wewe unaishangaa hiyo Tsh 27,000/= Yameingia makampuni mengine ya simu, TTCL nao wameondoa hizo unazozishangaa leo.
Nacho taka kusema, huwezi kunidai gharama za installation wakati mimi ni mteja wako, jenga na sambaza kwa gharama zako, mimi nitalipia services kulingana na matumizi yangu. Mbona vitu vingine virahisi tu kueleweka mkuu?
Nainukuu...
"Mkuu, hili suala mimi naliona katika sura mbili (nina hisia mchanganyiko).
1. Mambo yalivyopaswa kuwa (as it should be).
Kwakuwa umeme na miundombinu yake ni mali ya TANESCO, umeme ulipaswa kuunganishwa kwa mteja bure kabisa. Au pengine kulipaswa kuwa na "bonus" kwa mteja kuunganishiwa umeme.
Mfano, Unganisha umeme ujishindie smartphone, au Unganisha umeme ujishindie unit 100 za bure.
2. Mambo yalivyo (as it is).
Huu sasa ndio UHALISIA wa mambo.
Uwezo wa TANESCO kwa sasa kuunganishia watu umeme bure, au kwa 27,000 ni mdogo mno au haupo kabisa.
Tukiwalazimisha kuunganishia watu umeme kwa hiyo 27,000 au bure, watakua wanachukua buku 27 zetu then wanaanza kutupiga chenga kuunganishia umeme. NJOO KESHO zitakua nyingi.
Msingi mkubwa wa hizi gharama ni "tusaidiane ili mambo yaende" yaani cost sharing.
Hivyo mabishano yote haya msingi wake ni nani achange nini.
Mimi binafsi nawaelewa TANESCO katika hili, elfu 27 kimsingi sio jukumu la mteja, ila kiuhalisia italitia hasara shirika tajwa."
Mwisho wa kunukuu.