Nilipomuona Waziri Januari amevaa suti na miwani, akizungumza kama philosopher ingawa maneno hayakuwa na philosophy, nikajua TANESCO kwa heri. Tanesco haihitaji ujidai unajua, inahitaji mtu anayejitambua hajui ili watu wamweleze asiyoyajua. Sasa kama aliingia kwa ujuaji, ameanza kuonesha u-mbumbumbu wake.
Pale Dar kuna viwanda vinayeyusha vyuma chakavu usiku kwa kutumia umeme bila mita. Mchana ukienda wanatumia mita. Vijana wa TANESCO wanajua na wanakula bili kila mwezi! Haya ni mengi muno na 'mameneja' wa kanda na mikoa na makao makuu wanafahamu. Sasa huyo Maharage Chande na ujanja wa misheni misheni atafika wapi na wa-TZ?