mkwawa masawe
JF-Expert Member
- Nov 19, 2018
- 225
- 346
Mimi huwa najiuliza,Ina maana hata Kama Ni msomi na unao uzoefu wa kutosha kwamba umeshakifanyia kazi Serikalini kwa muda mrefu kile ulichosomea.Ina maana huwezi kuteuliwa Nafasi ya juu ya uongozi Hapa nchini kwa vile TU unatokea familia isiyofahamika(ya ki-masikini) ? Maana teuzi nyingi za maana Ni za Watoto wa wanasiasa(viongozi) wa zamani na wa Sasa.Ukienda walioajiriwa mashirika muhimu Ni ndugu haohao.e.g huko TRA,BOT,UHAMIAJI,TRAFIC POLICE,MAWAZIRI NA MANAIBU WAO,MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU,WAKUU WA WILAYA,WAKUU WA MIKOA,WAKURUGENZI KWENYE MASHIRIKA NA MANAIBU WAO,n.k.familia hizi hazikosi Watoto wao kwenye Hayo maeneo niliyoyataja hata Kama Watoto hao Ni vilaza.Viongozi wetu kumbukeni kutunyanyua na Sisi ndogo mdogo Watoto familia masikini waliosoma.