Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Sasa Maxence Melo umemsikia mwenyewe mama anapitia JF kusoma mijadala.

Rai yangu kwako jukwaa la siasa limejaa uchafu ningependekeza thread zote zisiruke hewani bila approval ya moderator ili kupunguza uchafu jukwaani.

Na ikiwezekana uongeze nguvu jukwaa la siasa ili mijadala yenye afya irudi kama zamani, watu hawachangii jukwaa la siasa Sasa hivi limejaa matakataka mengi.

Please litendee haki JF ambayo leo mama ameipaisha kama platform anayoitegemea kupata maoni.

Na ndio sababu tuliokataa unafki tumejipambanuwa wazi kwamba Magufuli alikuwa ni shetani na muuwaji, mama ameyasoma yote haya na leo ameahidi kwa kusema never, never again.

Cc: Pascal Mayalla
 
Maraisi huwa wanasoma. Wala usianze kuweka masharti mengi Cha muhimu wajinga walio wengi hasa wa ufipa wawekwe chini ya uangalizi
 
Wanataka rais atoe maneno kupingana na msimamo wa chama chake cha CCM. Akifanya hivyo, angewafurahisha. Hata hivyo, naona Samia ameepuka kukamatwa katika mtego wa CDM. Mbowe ametoa lawama nyingi na hata kumuita JPM dikteta na kudai kwamba aliwatesa watu. Hivyo, isitokee tena. Sijui kama Samia alijua. Njia ya maendeleo kwa Tanzania ni ile ya kimagufuli tu. Na hiyo ndio njia ya kinyerere, Ki Edward Sokoine, njia ya Kisamora Machel, njia ya Ki Thomas Sankara, njia ya kijamaa. Binafsi, nilihofu kuwa mtego utamfetukia Mama Samia lakini ameepuka hilo.

Vita kubwa inaendeshwa na maajenti wa ubeberu kupitia upinzani, ambao wanajaribu kufuta jina la JPM na ujumbe wake katika mioyo ya Watanzania. Hata hivyo, hili halitafaulu kamwe. Wametumwa watu kama Lissu, Lema, na Mbowe, lakini hawawezi kufaulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…