Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Nasikiliza hapa kwa redio mh rais anasema Huwa anapita humu kuangalia baadhi ya maoni ,

Anasema Huwa anacheka sana kuona wanaomkosoa

Mimi napenda kusema kosoa kwa staha
Tema madini yako
Huenda mkuu akakuona unafaa akakuchagua kutoka humu jamiiforums

Inawezekana.
Kumbe mnasaka uteuzi humu?
 
Sasa Maxence Melo umemsikia mwenyewe mama anapitia JF kusoma mijadala.

Rai yangu kwako jukwaa la siasa limejaa uchafu ningependekeza thread zote zisiruke hewani bila approval ya moderator ili kupunguza uchafu jukwaani.

Na ikiwezekana uongeze nguvu jukwaa la siasa ili mijadala yenye afya irudi kama zamani, watu hawachangii jukwaa la siasa Sasa hivi limejaa matakataka mengi.

Please litendee haki JF ambayo leo mama ameipaisha kama platform anayoitegemea kupata maoni.

Na ndio sababu tuliokataa unafki tumejipambanuwa wazi kwamba Magufuli alikuwa ni shetani na muuwaji, mama ameyasoma yote haya na leo ameahidi kwa kusema never, never again.

Cc: Pascal Mayalla
Tatizo sio thread Bali wachangiaji hawana staha
 
Rais Samia: Hakuna kisichowezekana kwenye mazungumzo, tumesuhudia nchi kadhaa zimeingia kwenye vita hawakupata suluhu, suluhu imepatikana kwenye mazungumzo kwahiyo tuendelee kuzungumza. Najua si rahisi kabisa watu kuja na utamaduni huu mpya ukakubalika mara moja, si rahisi, kwangu kuna vikwazo kwangu kuna vikwazo.

Huwa napitia Jamiiforums naangalia maoni yenu kule ndani, nasoma nnacheka, nasema lakini huu ni utamaduni mpya, si rahisi kukubalika kwa ghafla, kwahiyo pande zote Tanzania nzima si rahisi kukubali utamaduni huu mpya kwa haraka.

anacheka.....
 
Wanataka rais atoe maneno kupingana na msimamo wa chama chake cha CCM. Akifanya hivyo, angewafurahisha. Hata hivyo, naona Samia ameepuka kukamatwa katika mtego wa CDM. Mbowe ametoa lawama nyingi na hata kumuita JPM dikteta na kudai kwamba aliwatesa watu. Hivyo, isitokee tena. Sijui kama Samia alijua. Njia ya maendeleo kwa Tanzania ni ile ya kimagufuli tu. Na hiyo ndio njia ya kinyerere, Ki Edward Sokoine, njia ya Kisamora Machel, njia ya Ki Thomas Sankara, njia ya kijamaa. Binafsi, nilihofu kuwa mtego utamfetukia Mama Samia lakini ameepuka hilo.

Vita kubwa inaendeshwa na maajenti wa ubeberu kupitia upinzani, ambao wanajaribu kufuta jina la JPM na ujumbe wake katika mioyo ya Watanzania. Hata hivyo, hili halitafaulu kamwe. Wametumwa watu kama Lissu, Lema, na Mbowe, lakini hawawezi kufaulu.
Hata Mimi nimemshangaa yaani alivyoongea Catherine Ruge ni kistaarabu ila Mbowe ameongeza utumbo na shida kubwa hana IQ..

Huwezi alika mtu ambae hamna maoni sawa yet unamzodoa tena Kwa Kauli chafu mara useme uchafu wa uchaguzi nk nk hii sio sawa.
 
nafarijika kuona hata mama huwa anapitia uzi humu mjengoni mwwtu na kusoma halafu anacheka
ngoja niendelleee kuleta nyuzi zangu nahisi nitapanda pale mlimani

happy women's day
 
Kwakweli mama umeupigwa mwingi sana, wanawake wa CDM wamefarikika sana nikupongeze sana kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, umefungua njia naamini wema huo ni mola pekee atakaye kulipa.

Unakwenda kuandika historia ambayo wengi walishidwa, ubarkiwe sana
 
Back
Top Bottom