Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Rais Samia: Huwa napitia JamiiForums naangalia maoni yenu

Imagine maoni yangu yanasomwa na raisi wa nchi. [emoji1787]
Ndiyo tujitahidi kuandika mambo ya kujenga na kama ni kukosoa tukosoe kwa ukweli na kwa nidhamu.
Naamini ni mchukuaji wa maoni mengi ya humu jukwaani.
Kongole Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.
Kongole JamiiForum.
Mungu mbariki Rais Samia.
Mungu ibariki Jamii Forum.
Mungu tubariki wana Jamii Forum wote.
 
Now all is Well ?!!!!!

Apunguze kupita huku au apite huku; wakati akipita kule na kuhakikisha mambo hayaendei mrama (hizi story za kwamba we are better off kushinda majirani) tunasahau kwamba tuna resources kushinda majirani....
 
Point kabisaaa mkuu
Mods, JF imepewa heshima kubwa sana. Kama Rais huwa anapitia humu kupata maoni yetu kama sehemu ya umma wa Watanzania, hakika nawaambieni, hakuna kiongozi ambaye hatapita JF.

Lakini ili maoni yetu yapewe uzito wa kupewa tafakuri ni lazima Mods walinde hadhi ya jukwaa kwa kuwapa adhabu kale wale wote wanaoligeuza jukwaa lionekane ni la wahuni.

Mtu akitukana au kukejeli, apigwe ban hata ya miezi 6 au mwaka mzima. Kuna watu humu, wanashangaza, wanafikia kumtukana kiongozi, unatafakari na kujiuliza JF siku hizi imebeba watu wa namna gani?

Mods, lirudisheni jukwaa kwenye heshima yake ili kiwe ni chanzo muhimu cha habari kwa wasio na habari, liwe ni jukwaa la ushauri kwa viongozi wa Serikali, vyama na taasisi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom