Rais Samia ikiwezekana kwepa kuwalenga Wasukuma moja kwa moja kwenye hotuba zako

Rais Samia ikiwezekana kwepa kuwalenga Wasukuma moja kwa moja kwenye hotuba zako

anasema ngombe mmoja anakunywa lita 40 kwa siku.

anasema kwato za ngombe wa wasukuma zinakanyaga ardhi na kuharibu ecolojia na hivyo kiusababisha ukame

my take. michongo iendelee.
Akili huna unakalia ukabila maji
 
Kama ni kweli asiseme kisa kuwahofia?

Mbona Wachaga wanasemwa waziwazi wezi miaka nenda Rudi..


Acha vitisho vya kitoto
 
Ni leo tena.

Mheshimiwa Rais amewatupia lawama Wasukuma kwa kuharibu vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa sababu ya ufugaji wao wa ng'ombe wengi.

Nia yangu bayana kwenye andiko langu ni kumshauri Rais ikiwezekana ajizuie kuwataja moja kwa moja Wasukuma kwenye hadhira kwa sababu hali ile pengine inaweza kutafsirika tofauti na walengwa hasa ukizingatia ndani ya muda mchache wa Utawala wake tuhuma nyingi za kubaguliwa walengwa zi bayana.

Ingetosha mheshimiwa Rais angetoka kauli ya jumla tu kwamba wafugaji ni sehemu ya wanaoharibu vyanzo vya maji

Sasa unapowataja Wasukuma moja kwa moja ilhali wapo wamasai na makabila mengine mengi yanayofuga maelfu ya mifugo ni sawa na kuwabagua watajwa

Mungu ibariki Tanzania.
.........pia asiwataje wamachinga moja kwa moja awaite wajasiriamali wa kujitegemea..........
 
Kwa kweli mama ameteleza mno kuwananga tena kwa kuwataja kabisa huku akiwa amezungukwa na Maaskofu Wasukuma zaidi ya Saba 🤔 tena wakatoliki!
Lawama ziwaendee hao maaskofu. Kulikuwa na ulazima wa yeye kualikwa?!
 
Back
Top Bottom