Rais Samia ingilia kati suala la Mbowe ukubalike zaidi kisiasa; kesi ikitupwa au akishinda itakuharibia taswira yako na ya CCM

Mbowe mwenyewe hajionei huruma kwahiyo hastaili kuonewa huruma abaki huko alipo,kumchekea nyani shambani ujira wake ni kuvuna mabua.

Unamuonea huruma,unamfutia kesi,akirudi uraiani anakusanya tena wapumbav wenzie waandamane[emoji3525]

Ukitaka uonewe huruma,jionee huruma mwenyewe kwanza kisha waonee huruma na wenzio...
Angemuacha mama afanye kazi ngumu aliyonayo ya kuongoza nchi.

Mkumbuke those first days za mama alifanya huruma nyingi kwa wana CHADEMA na Mbowe wao,aliwafutia makesi, alitengua ile hukumu ya fine na mamilioni ya pesa walirudishiwa

Sasa mama awafanyie nini hawa watu au awanyonyeshe ndo waone wanahurumiwa???[emoji3525][emoji3525][emoji3525]
HARAKATI ZINGINE ZA KI FALA...
 
Very bad advice!
Sahia hata kuwa wa kwanza kuingilia maana Nyerere akisha weka precedent alipomtoa Yule mahabusu mgiriku akiyesema kaiweka serikali ya kifimbo mfukoni...
Au labda una reasoning tofauti- iweke hapa tuichambue...

mwisho, ccm na serikali yao wapambane kwa hoja sio maguvu wanna mitambo ya watoa hoja sasa wanaogopa nini katiba Mpya na tume huru kwa kumshitaki messenger? Fair play uwanjani ndio mpango mzima siku hizi sio maguvu na kukandamiza watu kwa makesi ya kijinga
 
Kosa ni kosa hata kama mtendaji atakuwa si wa kwanza kulitenda!

Mimi napendelea zaidi mfumo wa haki ndiyo uamue hatia ya Mbowe. Siyo Rais wa nchi.

Leo watu wanataka waziwazi kuwa Rais aingilie kati na kumtoa Mbowe jela na kumfutia kabisa mashitaka.

Ni precedent mbaya sana maana akifanya hivyo, nini kitamfanya asifanye tena hivyo kuhusu mtuhumiwa mwingine yeyote yule huko mbeleni?

Si vizuri hata kidogo Rais kuanza kuingilia mambo ya utoaji haki wakati mfumo wa kufanya hivyo upo.
 
Upo sahihi..
Mbowe amekamatwa kwa maelekezo ya ikulu...kwa hiyo Rais anahusika moja kwa moja.
Na kwasababu yeye ndie alietoa go ahead ya Mbowe kukamatwa, ni yeye ndie wa kuondoa haya mashtaka..kwa namna gani?? Atajua yee mwenyewe.
 
Na zile kesi watu walifunguliwa zikawa Mahakamani na Raisi Magufuli akaagiza watuhumiwa wanaweza kukubaliana na DPP ili walipe faini haikuwa kuingilia uhuru wa Mahakama?

Dont read selectively. Thread imeshasema "Katika mazingira kama haya, ushauri wangu kwa Rais Samia ni kwamba atafute namna ya kuingilia suala hili, bila kuonekana anavunja uhuru wa Mahakama, ili watu wote waone kwamba Mbowe na wenzake waliachiwa na kesi hii kutupwa kwa sababu Raisi Samia alitumia busara katika kuimaliza.

Najua kwa sasa suala hili limemuweka Rais Samia mahali pagumu sana kwa kuwa halikupaswa kufika kote huku,"

Kwa hiyo unachokitataa wewe tayari kimekuwa factored katika thread na sio suala tena la kujadili.

Labda swali la maana ambalo ungeuliza ni "ni vipi Raisi Samia anaweza kuingilia kumaliza hili bila kuingilia uhuru wa Mahakama".

Then ungekuwa una-contribute constructively to the thread, la sivyo unatuambia kitu ambacho tumeshakuambia. Give us suggestions dont expand on challenges that have already been acknowledged in the thread.
 
Watu mnawaza 2025 wakati mnajua kwa katiba hii rais na mwenyekiti wa ccm ndyo anayeamua nan awe mrithi wake
 
Kuna jambo hapa wengi hawajui!!..Mbowe has nothing cha kupoteza kwenye case hii!!..Sasa kama ndivyo Itakua aibu kubwa Kwa serikali kupoteza case hii alafu italeta mtikisiko mkubwa nchini na Duniani kote!!.. Angali jinsi chadema na marafiki zao walivyojipanga kushinda case angalia jinsi case ilivyo kiajabu hata mtu ambae siyo mwanasheria anaweza kusema tayari Mbowe kashinda labda serikali iamue kuingilia Mahakama lakini Kwa jinsi ilivyo ni ngumu sana!!!..
 
Acha poroja mahakama ipo. Ukweli mama samia akitaka mustakabali wake mwema amuachie mara moja sabaya ndio kabambikwa kesi sio mbowe.
 
Mtauliwa kama wale wa kibiti
 
Tatizo la washabiki wa wanasiasa wa Nchi hii hilo likifanyika watasema Rais aliwaogopa au walishinda kesi kwa nguvu zao "rejea kesi za Mashekh wa Uamsho na ya Mdude "
 
Hata mimi nakubaliana na wewe kuhusu haki mahakamani, lakini je akipatikana hana hatia, ni nini hatma ya waliomstaki ? Inabidi sasa nchi kama nchi ifikie mahali na kuwafidia wote wale ambao walishtakiwa na baadae mahakama kuona kwamba hawana hatia... pili hizi kesi zinazo wafanya watu wake mahabusi bila dhamana zina-breach haki za watu na due process nzima, sijui majaji wetu hizi sheria huwa wanasomea wapi na kuiacha serikali ifanye inavyotaka katika suala zima la kumaliza hizi kesi haraka...nimesikia wanasema kwamba upelelezi umekamilika , ya nini sasa kuendelea kumshikiria humo ndani na dana dana kibao za procedures tu na kukomoana..,. humu duniani hatuishi milele, tutafute namna ya kupendana sote kama ndugu wa Taifa moja bila chuki, mkwaruzo wala kesi za kuokotezea ushahidi...
 
Kama kujipanga ndiyo ticket ya uhakika kwa asilimia 100 ya kushinda kesi mahakamani wote waliojipanga wangekuwa wanashinda vyesi vyao. Hivi hujawahi kujiuliza pamoja na wingi wa mawakili wote wa Mbowe kwa nini wanashinikiza aachiwa kabla ya kesi kusikilizwa?. Kuna kitu haukijui. Wao wanaelewa potential risk iliyo mbele ya Mbowe. Usifanye utani na sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…