Wanabodi,
Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.
Anasema Zanzibar inafaidika sana na muungano, kisiasa, kiuchumi na kijamii, ikiwemo kufaidika kielimu, wakati wa muungano, Zanzibar haikuwa na chuo kikuu chake hivyo Wanzanzibari wote wa enzi hizo waliofika elimu ya vyuo vikuu, wamesomea bara.
Mama Samia amesema watu waachiwe kuujadili muungano kadri watakavyo na hata kutema nyongo kuhusu muungano, na serikali inazitumia hizo hoja zinazolalamikiwa kuimarisha muungano, akasema ni heri watu wafunguke na kusema hivyo kuyatoa madukuduku yao, kuliko kunyamaza na madukuduka ndani yao, siku wakilipuka moto utawaka, hivyo watu waachwe waseme.
Amesema Zanzibar ni visiwa hivyo viko wazi pande zote, hivyo faida kubwa kabisa ya muungano ni ulinzi usalamax amani na na utulivu wa Zanzibar, bila muungano, ilikuwa ni rahisi sana kuivamia Zanzibar na Zanzibar ikivamiwa ni rahisi sana kuivamia bara, hivyo muungano umeimarisha sana ulinzi na usalama, amani na utulivu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amezungumza mengi na kumalizia kwa kusisitiza Muungano ni jambo jema, tuulinde na kuuenzi.
Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.
Paskali