Rais Samia, jaribio lolote la kuipa Zanzibar mamlaka kamili ndilo litakuwa anguko lako

Rais Samia, jaribio lolote la kuipa Zanzibar mamlaka kamili ndilo litakuwa anguko lako

Kulinganisha pre-independence Zanzibar na post-independence Zanzibar ni uvivu wa kufikiria. Unadhani Karume alikuwa mjinga aliposema yeye alikuwa tayari kuwa VP ndani ya Muungano wa Serikali?

Alikuwa mjinga haswa. Kenyatta alikataa Muungano na mpaka leo Kenya ipo sembuse Zanzibar taifa la kihistoria? Kenya na Zanzibar ni wapi kuna ukabila na ubaguzi zaidi?

 
Kabla hata hajafikiria kufanya hivyo, bendera zitapepea nusu mlingoti. Huo muungano hakuna atakekuja kuuchezea kizembe.
Wacheni upumbafu watanganyika wadanganyika tume zote zilizoundwa zilikuja na MTAZAMO WA SERIKALI TATU dunia nzima hakuna mfano WA Muungano huu ulopitishwa KILAGHAI
UHURU WA ZANZIBAR NI SASA
 
Unadhani kila mtu anatamaa ya kuendelea kuwa Rais?! Alishawaambia kuwa kuna hatua anazichukua akielewa kuwa anaweka Urais rehani, kwake it's okay.

Hata mkimtoa leo ataendelea kula mema ya nchi hadi anakufa, roho ya Mama haina tamaaa kama TEAM JIWE.
Waambie wapumbavu hao
 
mleta mada, ungeongezea udadavuzi kwenye mada yako!!!
umeona nini kuorodhesha dalili unazoona wewe na umetumia utaratibu gani kuzijua au unahisi wote tuko kama wewe kuona......
 
Mkuu Suzy Elias, ungekuwa umetutendea haki kama ungesema hilo tishio la usalama wa JMT ni tushio gani endapo Zanzibar itepewa hadhi sawa na haki sawa ndani ya JMT kama ilivyo Tanzania Bara, mfano muungano wa federation au muungano wa mkataba?.

Kuna wengi wamemjua Samia baada ya kuwa Rais wa JMT, ndio mnaweza kuwa na mashaka na Samia kwenye kuulinda huu muungano wetu adhimu. Angalia bandiko hili ni la lini na Rais Samia alisema nini kuhusu muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Na kwa faida ya wavivu to follow links

P

Mayalla, katika system ya federation, state government haiko sawa na federal government. Ingawa state government inazo taasisi nyingi ambazo federal government inazo state government haina taasisi zinahusika na ulinzi, foreign affairs, currency na uraia & uhamiaji. Hakuna kipya ambacho Serikali ya Zanzibar inaweza kupata ndani ya federation isipokuwa uwezo wa kuwa na polisi wake yenyewe, which won’t make a whole lot of difference!

Hakuna muungano ambao sio wa mkataba. Hata wa sasa ulizaliwa na mkataba. Federations zote zinazaliwa na mkataba. Hata ndoa yako ilizaliwa na mkataba. Upekee wa hii mikataba pengine ni kule kutokuwa na sunset provisions. The contracts are indefinite!
 
Muungano wa watu ulianza karne kibao kabla ya Muungano huu uliofaywa wa kisiasa 1964.

Sasa kama watu kabla ya muungano wa kisiasa walikuwa wanafanya biashara, wanakwenda soma skuli Zanzibar, wanaenda kuwa vibarua vya muda kama wakwezi wa minazi na kuchuma karafuu halafu wanarejea kwao Sukumaland, wa visiwani nao walikuwa wanakwenda bara kutafuta bidhaa n.k kisha wote kulowea katika pande mbili yaani bara na visiwani.

Na watu wa pande hizi mbili walikuwa wanaona manufaa yake, je ni kweli wanasiasa wanaweza kusema wao ndiyo wanadumisha muungano wa kweli wakati wanasiasa hao walianzisha muungano wa 'makaratasi' yaliyotiwa saini kama hati mwaka 1964.

Wakati wananchi wa bara na visiwani muungano wao ni wa mioyoni mwao kwa karne kibao tujiulize nani hasa ana nguvu ni watu wa pande mbili au ni wanasiasa watia hofu ?

Romani ya Dola Kubwa ya Zanzibar almaaruf Zanj iliyokwenda mpaka Afrika ya Kati Congo DR na kuacha kiswahili cha kingwana n.k

1655949248830.png
 
Unadhani kila mtu anatamaa ya kuendelea kuwa Rais?! Alishawaambia kuwa kuna hatua anazichukua akielewa kuwa anaweka Urais rehani, kwake it's okay.

Hata mkimtoa leo ataendelea kula mema ya nchi hadi anakufa, roho ya Mama haina tamaaa kama TEAM JIWE.

Kama unafikiri Hangaya hautaki Urais, think again! Huoni sarakasi anazocheza kuhusu Katiba mpya na juhudi anazozifanya kuweka mazingira ya uncontested nomination ndani ya CCM?
 
Alikuwa mjinga haswa. Kenyatta alikataa Muungano na mpaka leo Kenya ipo sembuse Zanzibar taifa la kihistoria? Kenya na Zanzibar ni wapi kuna ukabila na ubaguzi zaidi?



Seriously, unawezaje kuilinganisha Kenya na Zanzibar?

Mtifuano unaoweza kutokea Zanzibar ni kama ule wa Wahutu na Watutsi.
 
Nje ya Muungano, hakuna Zanzibar isipokuwa kuna Unguja na Pemba. Kama wanadhani sumu inaonjwa, wajaribu waone. Haitaisha miaka mitano kabla Tanganyika haijapokea wakimbizi kutoka upande huo!
Hacha mawazo ya kale na ya kikuda ya akina juius na karume wewe mgese
 
naanza kupata picha ya katiba mpya!
 
Katiba mpya ndio kila kitu. Aendeleee kuupifa pande hizi tuone tofauti. Kizaxi hiki hakitapita hata haya yote yawe yametokea
 
Wacheni upumbafu watanganyika wadanganyika tume zote zilizoundwa zilikuja na MTAZAMO WA SERIKALI TATU dunia nzima hakuna mfano WA Muungano huu ulopitishwa KILAGHAI
UHURU WA ZANZIBAR NI SASA
Sipo hapa kujadili uzuri au ubaya wa muungano ili kujua kama una faida au laah... nipo hapa kukumbusha kuwa;-

Ikiwa wazo la kuuharibu muungano litakuwa ni lake binafsi(SHH) bila kuungwa mkono na wanaomfanya aendelee kuwepo hapo, basi hawezi kufanya lolote juu ya hilo (watammaliza).

Namaanisha yeye oekeyake hataweza na kigezo cha yeye kuwa Rais hakitoshi kukamilisha hilo.
 
Kuna hoja ya 'kipuuzi sana' inayoenezwa na wapotoshaji kuhusu uwepo wa serikali 3 utaongeza gharama

Hakuna gharama yoyote itakayoongezeka hasa kwa Tanganyika

Rais SSH akisafiri anakwenda na timu mbili, ya JMT na ya SMZ. Tofauti iliyopo ni kwamba timu ya JMT ndiyo inagharamia timu ya SMZ. Mfano Waziri wa Utalii wa Zanzibar alikwenda kwenye Royal tour lakini gharama za ujumbe wa Zanzibar zilibebwa na JMT ambayo ni Tanganyika.

Pili, kuna taasisi gani ya JMT isiyo na mbadala Zanzibar? Maana yake ni moja Taasisi za JMT ni za Tanganyika
Tatizo linakuja kwamba Zanzibar wakitaka mafao wanatumia jina la JMT. Mfano, wakitaka mikopo wanapata kutoka JMT lakini kulipa wanajiita SMZ na kuacha mzigo wa deni kwa Tanganyika.

Kuendesha taasisi za muungano limekuwa jukumu la JMT ambayo ni Tanganyika. Kunapokuwepo na mafao Zanzibar wanatumia jina la Tanzania. Kwa mfano, BoT inawapa 4.5% ya pato la Tanganyika kutokana na vyanzo vyote

Bajeti ya Zanzibar 2022/23 ni Tsh 2.5. Hakuna mahali kuna kipengele cha kulipa madeni yanayotokana na mikopo, hakuna bajeti ya Ulinzi, Mambo ya ndani, nje wala uchangiaji wa taasisi za muungano kama mishahara ya Wafanyakazi ambayo Zanzibar inapata 21%. Gharama hizo anabeba Mtanganyika

Kwa wale wanaosema kuna gharama, njooni mtuonyeshe gharama za serikali 3 zipo wapi?

Tuna serikali 3 leo hii isipokuwa serikali ya 3 imefichwa ndani ya Tanganyika.
Tanganyika inabeba serikali 2 ya Tanganyika na ya muungano ambayo Zanzibar wamo

Serikali 3 itakuwa na mambo 7 kwa mujibu wa rasimu ya Warioba. Hayo 7 ndiyo yatampa Rais wa JMT uwezo, kama vile ulinzi, mambo ya ndani, nje , Fedha, vyama vya siasa n.k.

Tanganyika itasimamia mambo yake na Zanzibar itakuwa na yake ! hilo ndilo suluhisho
Kinyume chake leo Zanzibar wanafurahia kwasababu ''kero zao'' zimemalizwa bila kutumia sheria

Ipo siku Rais atatoka Tanganyika kama ilivyotokea miaka 6 na kufuta mambo yote yasiyo kisheria
Ikitokea hivyo Wazanzibar watasema nini?Watamlaumu nani?

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Kuna kila dalili Zanzibar ikajitenga na kuwa nchi kamili kwa maslahi ya Viongozi wetu wa awamu hii.

Ni zaidi ya hatari endapo Zanzibar itaruhusiwa kuwa na mamlaka kamili kwa usalama wa Tanganyika!

Na hapa nisipepese macho NAONA KILA DALILI RAIS WETU WA SASA ANATAKA ZANZIBAR IWE NCHI HURU.

Kwenu Tiss.
Mjomba ni mama dada.. Akitaka kitu kumkatalia ngumu.. Iwe kwa mahaba, utii au shuruti
 
Back
Top Bottom