Rais Samia, jaribio lolote la kuipa Zanzibar mamlaka kamili ndilo litakuwa anguko lako

Kwani siyo nchi huru?
 
Zitaje hizo dalili ili watu wazijadili. Namna nyingine, hili andiko lako linakuwa nibumvea au majungu.

Hiyo mamlaka kamili maana yake nini? Maana mpaka sasa, nijuavyo mimi, Zanzibar ni mamlaka kamili tayari. Ina Rais, ina Bunge, ina wimbo wa Taifa, Tumeungana nao katika mambo machache. Wana mipaka na ardhi yao. Wana tume yao ya uchaguzi.
 
Nchi sasa ina amani mbona mama wa watu mnamzushia vitu ambavyo sivyo, hakika mama ni muungwana kuliko kawaida... MUNGU mkubwa sana
 
Tuambizane tu mipaka yetu ya bahari ilipo waende zao tuwaache wapambane vita yao ya identity crisis.

Hakuna faida yoyote ya muungano kwa bara unawanufaisha wao halafu ungrateful people.

Wana akili za kitoto kweli kama utalii wao wanadhani utalipa, ebu waangalia visiwa vya Caribbean kama Jamaica, Barbados wanaenda watu wangapi halafu wajilinganishe nao. Na hizo nchi bado maskini.

Bila ya bara ndio wataelewa amani waliyo nayo nani alikuwa anawatunzia.

Ifike wakati tuwaache waende inatosha; hakuna cha serikali tatu let Zanzibar go.
 
Political instability ya nchi jirani huwezi kusema it’s none of your business. Labda kama hujui unachoongea!
Itakuwa ni nchi ya kwanza jirani ya Tanganyika kuwa na tatizo hilo? Tutawapokea kama wakimbizi haina shida maana tumeshawapokea majirani zetu toka kila pande wakitaka hifadhi ya ukimbizi
 
Hamna cha maana ambacho Zanzibar inaipatia Tanganyika

Mbona hatujaungana na Comoro upande wa kusini mashariki

All in all kila upande uwe na mamlaka yake, yaani kuwe na Zanzibar huru na Tanganyika huru
Hili ni swali ambalo Tanganyika hawajiulizi! ni kipi wanapata kwa uwepo wa Zanzibar?
Sina tatizo na muungano, nina tatizo na muundo wake

Juzi akiwa Oman Rais Samia alisaini mkataba wa mashirikiano ya mafuta na gesi kati ya shirika la Oman (OPAL) na Taasisi za Tanzania (TOGLO) na Zanzibar (ZOGLO)

Jiulizeni, hapa Tanzania ni nani? Kama Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar kwanini kuna Zanzibar Pekee?
Pili, Rais wa JMT ni Samia, hawa Zoglo wanamwakilisha Rais yupi?

Gesi ya Mtwara inawafaidisha Wazanzibar leo hii, kesho wakiwa na yao hao ZOGLO hawana habari na Watanganyika

Ile 4.5% wanayopewa Wazanzibar ni kutoka rasilimali kama madini, gesi na kodi. Tanganyika inapata nini?

JokaKuu Pascal Mayalla Tindo
 

Punguza jazba halafu soma historia hapo chini. Zanzibar ilikuwa na uchumi mzuri kabla Nyerere hajaifilisi.


 
Watajijua wenyewe sisi tendelee kutafuta ugali wetu wa Kila siku
 
"Mbuzi alichinjwa wazee wakaniambia ruka nami nikaruka" J k Nyerere si rahisi kuitenganisha bara na visiwani
NB: Maneno yangu si torati
 
Good for them ni muda wa kurudisha uchumi wao kwanini tuwe kikwazo; issue ni mipaka ya bahari.

Sababu za Nyerere za kuungana leo tunajua hazina mashiko tumezungukwa na nchi 8 zenye mipaka ambayo vifaru vya adui anaweza pitisha sehemu yeyote ya kutushambulia; kwanini aende Zanzibar iliyombali zaidi.

Na kwanini tuwalazimishe kama wenyewe awataki, vunja tu huu muungano.
 

Kulinganisha pre-independence Zanzibar na post-independence Zanzibar ni uvivu wa kufikiria. Unadhani Karume alikuwa mjinga aliposema yeye alikuwa tayari kuwa VP ndani ya Muungano wa Serikali?
 
Sawa ila kuwa makini unaweza jinyea
 
Mkuu Suzy Elias, ungekuwa umetutendea haki kama ungesema hilo tishio la usalama wa JMT ni tushio gani endapo Zanzibar itepewa hadhi sawa na haki sawa ndani ya JMT kama ilivyo Tanzania Bara, mfano muungano wa federation au muungano wa mkataba?.

Kuna wengi wamemjua Samia baada ya kuwa Rais wa JMT, ndio mnaweza kuwa na mashaka na Samia kwenye kuulinda huu muungano wetu adhimu. Angalia bandiko hili ni la lini na Rais Samia alisema nini kuhusu muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Na kwa faida ya wavivu to follow links
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…