Kuna hoja ya
'kipuuzi sana' inayoenezwa na wapotoshaji kuhusu uwepo wa serikali 3 utaongeza gharama
Hakuna gharama yoyote itakayoongezeka hasa kwa Tanganyika
Rais SSH akisafiri anakwenda na timu mbili, ya JMT na ya SMZ. Tofauti iliyopo ni kwamba timu ya JMT ndiyo inagharamia timu ya SMZ. Mfano Waziri wa Utalii wa Zanzibar alikwenda kwenye Royal tour lakini gharama za ujumbe wa Zanzibar zilibebwa na JMT ambayo ni Tanganyika.
Pili, kuna taasisi gani ya JMT isiyo na mbadala Zanzibar? Maana yake ni moja Taasisi za JMT ni za Tanganyika
Tatizo linakuja kwamba Zanzibar wakitaka mafao wanatumia jina la JMT. Mfano, wakitaka mikopo wanapata kutoka JMT lakini kulipa wanajiita SMZ na kuacha mzigo wa deni kwa Tanganyika.
Kuendesha taasisi za muungano limekuwa jukumu la JMT ambayo ni Tanganyika. Kunapokuwepo na mafao Zanzibar wanatumia jina la Tanzania. Kwa mfano, BoT inawapa 4.5% ya pato la Tanganyika kutokana na vyanzo vyote
Bajeti ya Zanzibar 2022/23 ni Tsh 2.5. Hakuna mahali kuna kipengele cha kulipa madeni yanayotokana na mikopo, hakuna bajeti ya Ulinzi, Mambo ya ndani, nje wala uchangiaji wa taasisi za muungano kama mishahara ya Wafanyakazi ambayo Zanzibar inapata 21%. Gharama hizo anabeba Mtanganyika
Kwa wale wanaosema kuna gharama, njooni mtuonyeshe gharama za serikali 3 zipo wapi?
Tuna serikali 3 leo hii isipokuwa serikali ya 3 imefichwa ndani ya Tanganyika.
Tanganyika inabeba serikali 2 ya Tanganyika na ya muungano ambayo Zanzibar wamo
Serikali 3 itakuwa na mambo 7 kwa mujibu wa rasimu ya Warioba. Hayo 7 ndiyo yatampa Rais wa JMT uwezo, kama vile ulinzi, mambo ya ndani, nje , Fedha, vyama vya siasa n.k.
Tanganyika itasimamia mambo yake na Zanzibar itakuwa na yake ! hilo ndilo suluhisho
Kinyume chake leo Zanzibar wanafurahia kwasababu ''kero zao'' zimemalizwa bila kutumia sheria
Ipo siku Rais atatoka Tanganyika kama ilivyotokea miaka 6 na kufuta mambo yote yasiyo kisheria
Ikitokea hivyo Wazanzibar watasema nini?Watamlaumu nani?
JokaKuu Pascal Mayalla