Pre GE2025 Rais Samia: Jeshi na vikosi vyote vya Ulinzi vikae tayari kwa lolote wakati wa uchaguzi

Pre GE2025 Rais Samia: Jeshi na vikosi vyote vya Ulinzi vikae tayari kwa lolote wakati wa uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kura zitaibwa ndo maana jeshi wamewekwa at pa
Sidhani kama jeshi litakubali hilo. Wakikubali wanaiweka nchi hii katika precedence mbaya. Maana kesho hao hao ambao wamechomekwa Wanaweza tumia jeshi kubakia madarakani.

The dilemma is watakataaje amri halali ya Commander in Chief? Hapo sasa ndipo kauli ya Mh. Inapozua tafrani ambayo lazima kuwe na solution ya haraka, sidhani kama ameshauriwa vizuri na kama ndivyo basi aliyemshauri ana ulterior motives...My personal view
 
Jeshi kuwekwa alert ina maana ni tangazo la Vita!
Ndiyo kusema kilichotokea 2014 na 2015 ndicho kitakachotokea 2024 na 2025! Hakuna jipya!
Ili niwe na amani siku hizo nitakuwa naendelea na shughuli zangu binafsi!
 

Ombi langu kwenu (JWTZ) ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu na hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi, niwaombe sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenye Kamandi zenu tofauti kujipanga kwa ajili hii, mwaka huu tunaanza na chaguzi za serikali za mitaa kwa sababu tuko wengi, ni chaguzi zinazoshirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti, hatuoni kwamba kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa kwahiyo ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitogeza.

Hatusemi tukafanye chaguzi za kutumia nguvu hapana, taratibu, sheria na miongozo ya uchaguzi itafuatwa lakini Jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vikae tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza, mwakani tunaenda kwenye uchaguzi mkuu na ule ndiyo wenye vishindo vikubwa basi ikabidi nitoe tu taarifa na kuwaweka 'alert' kwamba hayo mambo yanakwenda kutokea na jeshi hatuna budi kujiweka tayari.
Ili wakulindie kura sio.
 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT amevitaka vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na hasa Jeshi kukaa tayari Kwa Lolote Ili kulinda amani ya Nchi wakati Taifa linajitayarisha na uchaguzi Mkuu kuanzia mwaka huu.

Sio Kwa Nia mbaya ni Kwa Nia njema tuu maana Machadema hayakawii kuogopa 😆😆

===

Mwizi wa kura anajiandaa kuiba
 
Alikuwa akiwahutubia wanajeshi wa JWTZ kukaa standby kukabiliana na uvunjifu wa Amani katia chaguzi zijazo. Amesema hiyo haina maana kuwa kutakuwa na uchaguzi wa vurugu, bali kujiweka tayari.

1. Polisi kwahiyo hawawezi kwa maana vurugu zitakuwa kubwa? Ana hofu ya nini?

2. My worries: mama anahofia nini? To me ni kuwa WATAIBA KURA KAMA MAGUFULI lakini anajua kuwa safari hii haitawezekana kirahisi na hivyo , watu wako tayari kuanzisha KAMKUNJI na hivyo kutumia JWTZ!

I stand to be correct on my worries
 
Mimi nikimaliza kupiga kura, huyooo nyumbani. Siwezi kupigwa virungu nitolewe ndulundi, wala kupigwa mitama nivunjwe miguu, eti kwa sababu namgombelezea tundu lisu aingie ikulu. Siwezi kufanya ujinga wa hivyo!
 
1000031057.jpg
 
Watu wengi hufikiri Tanzania ni nchi ya vyama vingi na kwamba Mwinyi aliruhusu vyama vingi kwa maelekezo ya Nyerere huwa nafurahi.

Majeshi yote Tanzania yapo chini ya CCM makamanda wengi ni wana CCM wana miliki na kadi za uanachama.

Zidumu fikra za mwenyekiti hii kauli haijawahi futika vichwani mwa wanajeshi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom