Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Rais Samia: Kabla sijaingia, biashara na Kenya ilikuwa ngumu. Asema kuchoma vifaranga wa Kenya yalikuwa makosa

Vifaranga tu, watu wanachinja mazizi ya ng'ombe mkoa mzima wakipatikana wachache tu wenye ‘mad cow’ disease na kuwapa hasara wafugaji ya kufa mtu.

Export ya mifugo ina taratibu zake ukivunja hakuna negotiations kwenye wasimamizi makini. Hata paka na mbwa wa ndani nchi za wenzetu akitoka tu nje ya nchi kurudi lazima awe amechomwa vaccination ya rabies vinginevyo haingii.

Seuse mtu anaeingiza vyakula wakati sheria ipo wazi inataka certification yenye kuonyesha hawana magonjwa, halafu unatetea uvunjifu wa sheria.
 
Yeye vipi Serikali yake ilipowaacha watu wa ajali ya ndege masaa matatu wakiwa wamefunikwa na maji hadi kufa kule Kagera? Anaona liko sawa? Kwa vifaranga ndio kinamuuma.

Mama yupo kwenye harakati za mfa maji. Uongozi umemshinda kila kitu kinaenda halijojo.

Tulivyokuwa na matatizo ya maji, umeme na bei ya vyakula angekuwa na muda wa kushughulika nayo wala asingekumbuka habari ya vifaranga vya kuku.

Kama ana guts azungumzie namna Kenya walipokuwa wanasema tanzanite inatoka Kenya.
 
Tunapoelekea mama atakuja kueleza yafuatayo
1. Alyempiga Lissu Risasi
2. Aliyetunga kesi ya mbowe
3. Aliyefadhili wizi wa kura na kuharibu uchaguzi
4. Aliyekuwa kiongiozi wa wasiojulikana
5. Aliyeiba 2.4T

Mpaka sasa kashasema
1. Wezi wa BOT
2. Waliotunga kesi za kubambikia watu.
3. .....
Halafu akisema hayo ndio yatatuhakikishia umeme na maji.
 
Sina wanajulikana hao waliochoma vile Vifaranga why nao wasichomwe vingaja. Siamini kama Magu alitoa tamko la kuvichoma bali naamini walikuwa waimba nyimbo zake.
 
Kwenye hili Rais Samia yupo sahihi. Kila mwenye akili timamu alijua uamuzi ule ulikuwa ni ukichaa, na Dunia nzima iliiona Tanzania kama ni nchi ya watu wenye uwendawazimu.
 
Kuvichoma ilikuwa ukatili ilitakiwa wazuie visiingie nchini virudishwe viliko toka au viwekwe quarantine vipewe chanjo zote, vikaguliwe vigezo vya kuingiza vitu kama vile kama sheria inavyotaka kisha wapigwe faini walio ingiza bila kufuata sheria.
Kuchoma ilikuwa ukatili, pia siamini ama a,mri ilitoka kwa mkuu wa nchi. Kama ndivyo mkuu alikosea.
Ilikuwa ni amri ya marehemu.

Mengine yote umenena vema.
 
Akili nyingine ni ya ajabu sana, inakuwaje unachoma Moto viumbe hai bila huruma??? Hata kama mmiliki ameingiza kimakosa haikufaa apigwe faini ili siku nyingine afuate utaratibu!?

Hatuwezi kuunga mkono Jambo hilo!
 
Mbona hasemi na Ben Saanane yuko wapi Azory Gwanda na Tundu Lissu nani aliwapiga risasi na watu waliookotwa bahari wamekufa nani aliwaua au vifaranga kwake ni bora kuliko roho za binadamu.
 
Hapa ni kwamba wala sio kupinga kwa nia njema, ila huu mjadala wa vifaranga unalenga kuzima mambo ya msingi yanayoendelea nchini kama mgao wa maji, umeme na gharama za maisha kupanda. Wameona kujadili mlango wa ndege na majaliwa haitoshi waongeze kingine wanachohisi kitakuwa na nguvu
Absolutely right.
 
Rais Samia amesema amri ya kuchoma vifaranga 6400 vilivyoingizwa kutoka Kenya miaka mitano iliyopita ilikuwa sio sawa.

Rais Samia kasema hawakushulikia vizuri uingizaji ule wa vifaranga maana pia vifaranga vinavyo haki ya kuishi.

Kuhusu biashara na Kenya, Rais Samia kasema mpaka karibuni ilikuwa ngumu, vikwazo vingi na kuchoma vifaranga ilifanya mambo yawe mabaya.

Rais Samia alizubgumza haya wakati akiongea na mawakili wa ukanda ya Afrika Mashariki.

View attachment 2427229
Jumapili iwe siku maalumu ya kuwaomba wakenya msamaha, lakini wakati huo maafisa wote waliochoma waje TBC na watubu na yule aliyeagiza kama yupo kaburini aombewe msamaha!
 
Akili nyingine ni yaajabu sana ,,inakuwaje unachoma Moto viumbe hai bila huruma??? Hata kama mumiliki ameingiza kimakosa haikufaa apigwe faini ili siku nyingine afuate utaratibu!?

Hatuwezi kuunga mkono Jambo hilo!
Ungekuwa na akili ungeuliza kwanza sababu iliyosababisha vikachomwa.
 
Akili nyingine ni yaajabu sana ,,inakuwaje unachoma Moto viumbe hai bila huruma??? Hata kama mumiliki ameingiza kimakosa haikufaa apigwe faini ili siku nyingine afuate utaratibu!?

Hatuwezi kuunga mkono Jambo hilo!
We na mama yako mmeona vifaranga ila watu waliopotea na waliouawa sio bora kuliko kitoweo.
 
Labda vilibeba ugonjwa unaosambaa kirahisi na vingeachwa vikae ata one hour tuu labda Nchi yetu ingekumbwa na ugonjwa Hatari sana....Nchi kama Australia wao pia hufanya hivyo..Namshauri RAIS afanye Kazi yake jinsi katiba inavyomwelekeza, sio Busara kuwakosoa watendaji/wataalamu waliopatiwa dhamani katika sekta Mbali mbali kwenye Taifa hili tena mbele za wageni...That goes to all political leaders, Kazi yenu ni kusimamia Sheria na kanuni na kupiga siasa katika wakati muafaka..mkiona kuna mtendaji kavunja Sheria, mnayo dhamana ya kumwajibisha kwa kufuata utaratibu na kanuni zilizopo kisheria... acheni tabia ya ku-politicize issues Bila kutumia taarifa na ushauri halali kutoka kwenye Taasisi zenye Authority. Imagine duniani kote viongozi wakuu wa Nchi wanapopata international audience wanaongelea global issues na jinsi ya kuifanya Dunia kuwa sehemu salama kwa kuishi ,sio kuongelea petty issues....Hilo suala la vifaranga ilitakiwa aandaliwe press conference yenye coverage kubwa VET au afisa mifugo wa wilaya aliongelee kitaalamu with enough facts ili ku-counter attack any diplomatic conflict na Hilo suala ndio lingekuwa limeisha..But kwasababu viongozi wetu ni Misters & Mrs know everything wanapenda kujibia kila issue...ndio maana sometimes wanajikuta kwenye firing line za wananchi wenye hasira Kali just because issues zote inaelekea wenyewe ndio wanaozijua na kuzifanya .... its about time wawaache wataalamu wetu watoe ufafanuzi wa kitaalamu, wao wake nyuma na kuongelea maswala ya jumla na kisera..sio waziri au RAIS unajifanya unajua tatizo na solution wakati hujui lolote zaidi ya kukusanya political mileage.
Fikra mfu kabisa kutoka kwa asiyeelewa kitu.

Haya, tukubali vifaranga walikuwa na ugonjwa. Wangefungiwa mahali bado ugonjwa ungesambaa nchini? Hata hivyo hakuna mtu yeyote, aliyefanya vipimo vyovyote juu ya afya ya wale vifaranga.

Yule kichaa wetu alikurupuka tu na kusema, "choma moto". Akakurupuka tena, "hao ng'ombe wote waliokanyaga ardhi ya Tanzania, taifisha wote, hili siyo shamba la bibi".

Yule mtu alikuwa mgonjwa, hata baba zake wadogo wana ugonjwa huo huo wa akili, wapo pale Bukoba. Inaonekana ni tatizo ambalo lipo kwenye ukoo wao. Tatizo ni mifumo yetu. Iliwezekana vipi mtu ambaye aliwahi kuugua tatizo la akili, huku kukiwa na matendo yake mengi yanayotia shaka ukamilifu wa akili yake, anapenya mpaka kuja kupewa nafasi ya juu ya uongozi. Kosa siyo la mgonjwa, bali walio wazima.
 
Do you really, from the deep bottom of your heart believe the guy could sign off on something like that?
... did it happen or just a mere story? If it happened, who authorized it? If it was wrongly done, was anybody accountable? If none was accountable, who do you think was behind that saga?
 
Back
Top Bottom