Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Huyu Bwana ameandika tweets kadhaa kuhusu hiyo kampuni ya kichina na namna wanavyopewa tender huku akionyesha kumtilia mashaka/ kumshangaa waziri Mwigulu.
Binafsi sisemi mengi hapa ila natoa with kwa Mhe. Rais kuchunguza mambo hsya ambayo hata kamati husika ya Bunge inatajwa.
Baadhi ya tweets ni hizi:
Mnakumbuka niliwapa simulizi, wizara ya fedha wameingia makubaliano na China Civil Engineering construction corporation kwa utaratibu wa single source (tenda bila ushindani) thamani ya Shs. 6.7 trilioni kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ bila ushindani?
Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 16. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni mzaha.
Utaratibu wa ‘single source’ ni LAZIMA mkandarasi awe amekidhi vigezo na uwezo. Huyu mkandarasi wa Mwigulu hana sifa hizo. Miezi 16 ameshindwa kupeleka hata ambulance, hakuna usala kwa wafanyakazi, na amefanya kazi kwa 4.4%. Mkandarasi huyu hajakidhi vigezo vya single source.
Ukumbi wa Msekwa imefanyika semina, wabunge wamelipwa Shs. 440,000 (Shs. 172.9M). Kuipitisha bajeti ya miundombinu (ujenzi wa lot Na. 6 ya Tabora - Kigoma (411km). Na gharama za ujenzi ni (Sh.11.1bn) kwa kila 1km. 411km mkandarasi atatumia Shs. 4.6T. Kapewa tender bila ushindani.
Kwa kuwa tenda hii ina matatizo na harufu mbaya ya rushwa, wabunge wamekusanywa ukumbi wa Msekwa na kupewa semina kuhusu jambo hilo na kisha nje ya utaratibu wa kawaida, wakalipwa Shs. 440,000 kwa kila Mbunge ambayo inafanya jumla kuwa Shs. 172.9M kwa wabunge 393.
Haya ni mambo yanafanyika gizani lakini wabunge wengine wenye nia nzuri na taifa letu wanatoka nje na kusema hi siyo sawa. Wapo waliopinga hoja hiyo. TAKUKURU, tunaomba jambo hili lichunguzwe, na wahusika wawajibishwe. Tusifanye rushwa kuwa ni kama DNA yetu.
MMM