Rais Samia: Kamera za Usalama zitaondoa Rushwa na ulazima wa kutumia 'Matrafiki' kila sehemu

Rais Samia: Kamera za Usalama zitaondoa Rushwa na ulazima wa kutumia 'Matrafiki' kila sehemu

Polisi wa Pale Kitonga, Ruaha Mbuyuni na Berrier ya Iringa mpaka aibu. Wapo pale kwa ajili ya kupokea rushwa na sio kuhudumia Raia.

Wakati mwingine wanalazimisha mpaka kutoa rushwa. Aibu sana

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Madereva wenyewe baadhi huwai kutoa rushwa ili kuepuka fine kubwa, kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani kwa makusudi
 
Watatega Barabara nzima? wanaenda kupiga rushwa ambapo hakuna camera nimewakuta Lugalo pale maofisa wameacha kukaa ofisini wamekuja kuziokota barabarani maana ofisini hazifiki
 
1. Hazitaondoa kabisa tatizo la rushwa kwa Askari ingawaje litasaidia kupunguza kwa kiasi Fulani.

2. Wasifunge kamera barabarani na/au mitaani tu, Bali kila Askari Polisi awapo kazini iwe LAZIMA AVAE KAMERA MWILINI MWAKE, yaani Body-Camera (BodyCam) kama vile walivyo Askari Polisi wa Marekani.

Hii itasaidia kurekodi matukio yote yamhusuyo Askari huyo wakati akiwa katika majukumu yake ya kazi sambamba na kuweza kufuatilia mienendo ya Maaskari Polisi kwa urahisi na kuweza kuwabaini wale Askari Polisi ambao watajihusisha na matukio ya uhalifu.

Iwe ni sharti la LAZIMA kwa Askari Polisi kuvaa BodyCam awapo kazini, ili kuwadhibiti Askari Polisi Wahalifu ambao wamekuwa wakilichafua Jeshi la Polisi, BodyCam iwe mojawapo ya Sare za Askari Polisi awapo kazini.
 
Polisi wa usalama barabarani wanakera mpaka basi. I wish wangeondolewa kabisa barabarani. Wengi wao wanapenda sana rushwa.
 
Yes kwa makosa ya speed na bima itakuwa ni vuziru kutumia kamera, lakini sidhani kama kamera pekee yake zitaweza fanya inspection ya ubora wa magari, kukagua mizigo na mengineyo, bado watahitajika askari kwaajiri ya ukaguzi wa magari. Labda ukaguzi kama huu pia ufanyike sehemu ambazo zina kamera pia
Hizo kamera si zitasimamiwa na watu au zitajiendesha zenyewe? Polisi watazichezea tu. Ni vizuri kila basi iwekwe namba ya simu ya kamanda. Abiria akihisi kuna rushwa anapiga simu kwa kamanda nakala kwa Takukuru.
 
Yes kwa makosa ya speed na bima itakuwa ni vuziru kutumia kamera, lakini sidhani kama kamera pekee yake zitaweza fanya inspection ya ubora wa magari, kukagua mizigo na mengineyo, bado watahitajika askari kwaajiri ya ukaguzi wa magari. Labda ukaguzi kama huu pia ufanyike sehemu ambazo zina kamera pia
Ni rahisi sana kutunxa takwimu za wenye magari na kuyakagua mara 2 au 3 kwa mwaka, simple
 
Hizo kamera si zitasimamiwa na watu au zitajiendesha zenyewe? Polisi watazichezea tu
Ni vizuri kila basi iwekwe namba ya simu ya kamanda. Abiria akihisi kuna rushwa anapiga simu kwa kamanda nakala kwa Takukuru
Hapana mkuu, police wakiwezeshwa kuvaa camera itakuwa bonasi, hizi camera zitakuwa mali ya metro na municipalities, na wao wata outsource kwa kampuni ili iwe ndio wahusika wa camera hizi, yaani kama point A wameweka fixed speed camera 📷, motorist aka overspend na kupigwa picha, hizi picha zitachukuliwa na kampuni hii binafsi, ambayo itazipeleka kwa municipalities au metro ambao ndio watakautuma notice kwa mtenda kosa thr physical address ya lile gari lililopo sajiriwa, traffic officer's hawatahusika na camera hizi, ila wakiamua kuweka road block, touch ndio hapo watahusika
 
Yes kwa makosa ya speed na bima itakuwa ni vuziru kutumia kamera, lakini sidhani kama kamera pekee yake zitaweza fanya inspection ya ubora wa magari, kukagua mizigo na mengineyo, bado watahitajika askari kwaajiri ya ukaguzi wa magari. Labda ukaguzi kama huu pia ufanyike sehemu ambazo zina kamera pia
Kwa ukaguzi vibaki vituo maalumu viwili tu kwa barabara za mikoa
 
Kuwatawala watanzania ni rahisi Sana kwa sababu ni wasahaulifu. Wakati was utawala wa serikali ya awamu ya tatu ubalozi wa China ulitoa kamera za kufungiwa barabarani kwa jeshi la polisi lakini hizo kamera hazikuwahi kufungiwa na hakuna mtu aliyewahi kuhoji mpaka Leo badala yake watu wanaongea ujinga na kusifiwa.
 
Mama kabla ya kuweka hizo camera basi tunagae basi na sisi mishahara yetu ilivyo, maisha yetu yanategemea walau mia mbili za barabarani.
 
Camera hazina.maana kama bandari yetu na mapori yetu yanauzwa
ha ha ha, flow mita za bandarini hazijawahi kufanya kazi hata siku moja tangu zifungwe itakuwa hivyo vi camera.
 
Traffic Police niliowaona Arusha sijapata kuona popote!!! Kila baada ya kilomita moja unakuta kundi la askari....
 
Back
Top Bottom