Rais Samia: Kamera za Usalama zitaondoa Rushwa na ulazima wa kutumia 'Matrafiki' kila sehemu

Rais Samia: Kamera za Usalama zitaondoa Rushwa na ulazima wa kutumia 'Matrafiki' kila sehemu

Sidhani kama serikali ya ccm inaweza kuwazuia police kukusanya rushwa .Wenyewe ccm wako madarakani kwa kuiba kura,wanawezaje kuwazuia wenzao kupokea rushwa?
Halafu bado anawambia nadhani huko mliko kwenye maeneo yenu mnapata.
 
DPW wamegawa rushwa kote yupo kimya anawalinda mpaka leo, hilo igizo aliloenda kulifanya kwa polisi halina maana.
Wewe kila linalosemwa na Samia unapata kichefuchefu. Hiyo yakutesa kweli kweli
 
Ni kweli my President, ona kati ya Dar na Morogoro ni 194km,ila kuna check points zaidi ya 27!!!,Kasane hadi Gabbs ni 800km,kuna check points 3 tu,Cpt to joberg ni 1400km ,no check points at all !!!
SA ni hub ya ushenzi,usiilete hapa,hata hivyo una hoja ya maana,waizingatie
 
Yes kwa makosa ya speed na bima itakuwa ni vuziru kutumia kamera, lakini sidhani kama kamera pekee yake zitaweza fanya inspection ya ubora wa magari, kukagua mizigo na mengineyo, bado watahitajika askari kwaajiri ya ukaguzi wa magari. Labda ukaguzi kama huu pia ufanyike sehemu ambazo zina kamera pia
Zitafanyiwa kwenye check points.siyo Kila sehemu polis wanakusimamisha waende kufanya kazi zingine Huko
 
Kuna askari wapo hapa STOP OVA kimara ni zaidi ya wehu.
 
Kwanza hata hyo mishahara masikini ya mungu askari wanapewa kid kiduchu sana makazi yao pia ni duni ssa mnapowafungiwa kamera ni kuwakosesha watoto wao njaaaa
Kwa hiyo walikubali kuajiriwa ili wakalichafue jeshi kwa rushwa?
 
Nimemsikia Rais Samia alisema Serikali itapinguza idadi ya Askari Polisi Barabarani Kwa kutumia teknolojia ya kamera maeneo mbali mbali.

My Take
Ni jambo jema ila Sasa Trafiki watakula wapi?
Kwani askari wengine ambao siyo trafiki huwa wanakula wapi? ama hao trafiki peke yao ndo wenye haki kula rushwa?
 
Issue ni hii project itakamilika? Ama itatutengenezea Lugumi mwingine? Tunakumbuka sababu zilizopelekea Project ya kufunga fingerprint devices kila kituo cha polisi kufeli? Maana project za design hii inafahamika kabisa wazee wa 10% ni kina nani. Kila la kheri
 
Polisi wa Pale Kitonga,Ruaha Mbuyuni na Berrier ya Iringampaka aibu!wapo pale kwa ajili ya kupokea rushwa na sio kuhudumia Raia!

Wakati mwingine wanalazimisha mpaka kutoa rushwa!Aibu sana

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Popote Tanzania hii pallipo na beria ya polisi hakuna la maana wanalofanya zaidi ya rushwa. Ukipita ukajifanya hutoi rushwa utawekewa zengwe kwa kupekuliwa mpaka uchoke na hata ukitoka hapo hiyo safari unayokwenda inakuwa imeshakuwa na kisirani tayari kwa maana nyingine kunao madereva wanaopata ajali kwa sababu ya kuendesha vyombo vyako kwa hasira na kisirani baada ya kuwa wameshatibuana na hao Askari huko barabarani na hasa kwenye maberia yao.
 
Nchi ya kelele na maneno kwa kwenda mbele. Rushwa inamalizwa kirahisi hivyo? Hebu kwanza aanze kujiwekea kamera yeye mwenyewe. Halafu waache kuuza vipande vya nchi na kupora uchaguzi kwani polisi nao ni binadamu na wana akili. Huwezi kumtuma polisi apore kura au akamate watu wanaokukosa makosa ya kweli halafu kesho umwambie usipokee rushwa kwa kumtishia na kamera.
 
Zitakuwa zinaharibika kila siku...na traffic polisi watafanya hivyo ili mchezo uendelee

Na labda zitumie solar, kama ni umeme bado ni tatizo
Zitakuwa za kampuni binafsi
 
Back
Top Bottom