Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Nchi inaendeshwa kwa kufuata katiba. Rais akiamua kutumia madaraka yake unavyotaka si tutarudi kwenye mambo ya awamu ya 5? Vyombo vya dola ndo vinatakiwa viwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. Tukisema Mama aanze kutumia ubabe hakutakalika. Tumshukuru sana kwa kuamua kufuata utawala wa kisheria.
na katiba hiyo hiyo inampa mamlaka raisi kuwa na maamuzi binafsi .

kiufupi acha uchawa kwa kuongea usilolijua
 
WANGEKUWA WAPINZANI WOTE WANGELALA GEREZA LA KEKO NA KESHO WANGEAMKIA MAHAKAMA ya MAFISADI bahati nzuri hao wote ni MAKADA
Sabaya na yeye ni wa chama gani cha upinzani?
 
Raisi alisema huwa anapita sana humu JF. Naamini hiki uloandika atakiona na kukifanyia kazi.
Sababu tulioumizwa na upotevu huo wa mamilioni ya kodi zetu ni wengi
 
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa raisi kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake raisi eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anaeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi kusimamia vyeo kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali.
Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Raisi na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Halafu utasikia mi5 Tena hata kama hataki na ikiwezekana hadi 2030!
Kweli nchi ngumu ya mamluki!
 
Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake raisi eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo
Pumbavu stupid haiwezekani.. hauelewi au ?
 
Kuna mawaziri wa hovyo kibao kawakumbatia na hawana msaada wowote kwake.
Chawa hao wanaitwa chawa ukiwaelewa hawakupi tabu... Maji hii inaenda wiki ya 3 Dar kumekauka maji hayatoki Juma Aweso yupo Marekani mvua zinanyesha maji hayatoki what is this alafu baadae akaseme watupishe wakati ujinga ujinga wanafanya unaonekana stupid pumbavu stupid haiwezekani ?
 
Dah......tumpe muda banaa ....miaka 2 ni muda mfupi sana 🤣 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hatunywi sumu hatujinyongi.... Hii mistari inaonyesha walivyo jeuri.
 
Raisi alisema huwa anapita sana humu JF. Naamini hiki uloandika atakiona na kukifanyia kazi.
Sababu tulioumizwa na upotevu huo wa mamilioni ya kodi zetu ni wengi
Ngoja tuone raisi atakachowafanya wezi wetu.
 
Pumbavu stupid haiwezekani.. hauelewi au ?
Kumtukana mwizi sio suluhisho. Hata wacheza movie huwa wanatukanana afu wakishamaliza ku act wanalipwa na kila mtu kusahau alichotukanwa.

Dawa ya wezi ni raisi kuagizwa wakamatwe wafungwe na kutaifisha mali zao zote ili iwe funzo na mfano kwa wengine.

Kuwambia wajitasmini ni kuwapa njia nyingine ya kupiga kwa style ambayo wanajua itakuwa ngumu tena kujulikana.
 
Anatumbua wa chini tu ila kule juu huwa hagusi.
Kuna mawaziri wa hovyo kibao kawakumbatia na hawana msaada wowote kwake.
Kama febuary , chemba na nepi wapo tu kwa hisani ya msonga hawana lolote kichwani mwao
 
Back
Top Bottom