Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Sindio viongozi mnaowapenda hao mnalalamika nini sasa? Wanaume wakikamata nchi mnalia lia ooh madikteta. Uliona wapi mtu anayepambana na mwizi akala nae kwenye meza moja.
Toka lini mwizi akabembelezwa au kuhamishwa kutoka sehemu aliyoiba kupelekwa sehemu nyingine akaibe zaidi?

Dawa ya mwizi ni kunyang'anywa alichoiba, kufukuzwa na kufungwa ili iwe tishio kwa watu wengine wenye mawazo ya kuiba kama ya kwake.
 
Ripoti ya CAG sio hukumu ya Mahakama,ikithibitika hatua zitachukukiwa..

Kumbuka Rais Samia sio mtu wa mihemko,kukurupuka na ku loose temper kirahisi ,ukifanya hivyo anaweza umiza wengi.
Si umesikia kwamba kuna watu wamekutwa na makosa zaidi ya matatu katika ofisi hiyo hiyo moja mpaka akaomba wawe wanabadilishiwa ofisi.

Sasa mtu anaekutwa na makosa zaidi ya mara mbili bado unaona kuwa akichukuliwa hatua au akisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi nayo itakuwa ni kukurupuka?
 
Tatizo la mama ni kutaka kuonekana mwema machoni pa kila mtu. Pia anaogopa kufuata nyayo za mtangulizi wake maana ashaonekana mara nyingi akimkataa. Sasa amejikuta haelewi nini afanye hivyo anajiendea tu.
Akiendesha nchi kwa hisia hizo, basi itamshinda mapema sana.
 
Raisi:Nimtumbue au nimwache.

Raia: Mtumbueeee.

Raisi: Kuanzia leo ww sio mkurugenzi.

Raia: yeeeeeeeeee

Chawa: Raisi hacheki na kima
 
nshakuambia ww ukikoment uache namba ya simu.

Teuzi inakuhusu

pumbavu ww
Sio kwamba teuzi inamhusu bali huenda ni mmoja wa watafunaji. Kwahiyo anahofia raisi akianza kuwachukulia hatua na yeye atakwenda na maji.
 
Hakuna atakayebakia salama Wala kusalimika katika suala hili la ufujaji wa pesa za umma,Nafikiri umesikia mh Rais namna suala hili lilivyomkera,hivyo Tuwe na subira watanzania maana Tunaamini hatua Kali za kisheria zinakwenda kuchukuliwa ,wahusika watapitishwa katika njia ya majuto na maumivu makali Sana kisheria ambayo itakuwa fundisho kwa watu wengine
Mkuu leo hujasifia? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nchi inaendeshwa kwa kufuata katiba. Rais akiamua kutumia madaraka yake unavyotaka si tutarudi kwenye mambo ya awamu ya 5? Vyombo vya dola ndo vinatakiwa viwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. Tukisema Mama aanze kutumia ubabe hakutakalika. Tumshukuru sana kwa kuamua kufuata utawala wa kisheria.
Unakatwa
 
You determine how serious people are based on how they solve pressing challenges.
Mkuu uendeshaji wa serikali ni mifumo. In short serikali ni protocols na systems na siyo mtu mmoja mmoja. Uozo wa mifumo ndo chanzo Cha mpenda sifa JPM kuwa aliko leo. Mifumo imeoza. Inanuka like huwezi kupambana nayo peke yako! Utaondolewa tu!
Wananchi tuamke Sasa!
Wasitubemende na propaganda za ushoga ushoga tunashadidia kumbe waandamizi wapo bize kupishana kukwapua mabilioni ya fedha!
Sasa kama hawezi kupambana nayo peke yake au wa kumsaidia kupambana nayo wako wapi?

Wanafanya kazi gani? Kama anaona wanashindwa kumsaidia si awafukuze na kuteuwa wengine ambao wataweza kumsaidia. Wewe unaona ni sawa kila ripoti inapotolewa raisi mzima analalamika bila kuchukua hatua.
 
Toka lini mwizi akabembelezwa au kuhamishwa kutoka sehemu aliyoiba kupelekwa sehemu nyingine akaibe zaidi?

Dawa ya mwizi ni kunyang'anywa alichoiba, kufukuzwa na kufungwa ili iwe tishio kwa watu wengine wenye mawazo ya kuiba kama ya kwake.
Hahahahahah na ndio maana huu upuuzi ulipungua sana awamu ilioisha. Sasa sahizi mtu karuhusu kuanzia wakurugenzi wote wawe wezi, mawaziri, wana usalama kuna kitu kitabakia kweli?
 
Mkuu unafikiri kuna rais pale?!!

Pale kuna kivuli tu kisichojitambua.
Inaonekana hata yeye mwenyewe haelewi mamlaka yake ni yapi, yupo kupiga mipasho tu.

Jiandae kutembelewa na vipepeo weusi hapo kwenu.

You are not free to talk to that extent, tena jaribu basi kushow some respect to our Madame President.
 
Mh. Rais ametoa agizo washughilikiwe haraka, Najua wahusika tumbo joto huko....sidhani Kama wizara/waziri husika atakubali apoteze kazi kwa kutotekeleza.
Raisi hakuagiza wachukuliwe hatua, bali aliwaomba waachie nafasi zao na kuendelea kula walichoiba.

Ingekuwa vizuri kama angewasimamisha kazi na kuagiza uchunguzi ufanyika, endapo wamehusika basi wafikishwe mahakamani na mali zao zote zitaifishwe. Zurudishwe kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom