Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Rais akitaka apeleke mswada bungeni ajira za kudumu zifutwe

Posho zifutwe asiyetaka kazi aache.

Wawekeze kwenye internet
 
Nchi inaendeshwa kwa kufuata katiba. Rais akiamua kutumia madaraka yake unavyotaka si tutarudi kwenye mambo ya awamu ya 5? Vyombo vya dola ndo vinatakiwa viwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. Tukisema Mama aanze kutumia ubabe hakutakalika. Tumshukuru sana kwa kuamua kufuata utawala wa kisheria.
Shida kama hiyo issue ameifanya waziri ambae kimsingi yeye ndiye anamteua, au katibu wa wizara je? Lazima asimame amtumue na atoe agizo la kwa takukuru na vyombo vingine asipotoa hakuna wakumkamata yule! Mbona kwa Sabaya aliweza? Huku anaogopa nn kwani?
 
Tatizo mama washamuona wana mmudu ndio shida ilipo : nakauli yake imemponza et kula kwa urefu wa kamba yako sasa ndio hao sasa wanakula kwa urefu wa kamba yao : angeendeleza pigo za late:sasa kitendo cha ku switch ndio amebaki hajui aende na mwendo wake au arud na mwendo wa the late sasa kabaki kat na time inasonga
 
Hii Nchi watu wasiolewa mambo kama mtoa mada ni wengi sana,hata hapa hapa nimeona comments za watu kusapoti hoja ya mtoa mada ni nyingi kweli.

Jamani Lowassa aliwahi kuwaeleza shida ya Watanzania ni Elimu,elimu elimu.MTU upo hapa hapa na wengine Serikalini but wengi hawajui mifumo inavyofanya kazi.

Hizo kauli anazitoa Mh.Rais ni za kisiasa na kupata points kutoka kwa watu wajinga.Serikalini kila manunuzi ya umma yana mudhinishaji wake kulingana na uthamni wa kitu husika.

By the way manunuzi kama hayo ya ndege yanaidhinishwa na Katibu Mkuu Kiongozi naye hawezi kuidhinisha pasipo ruhusa ya Rais.

Sasa unapopiga kelele sijui mnataka SAMIA ajipeleke yeye mwenyewe mahakamani au ajiachishe ngazi yeye mwenyewe. Ukiona anafukuza wahusika au kupelekwa mahakamani jua ndani ya Serikali moshi unafuka na anatakiwa watu watolewe kafala.

Ukiona familia inalala njaa basi jua Baba ndio chanzo.
 
Yuko wapi bwana Lucas mwashambwa mpambe wa mama
Hakuna atakayebakia salama Wala kusalimika katika suala hili la ufujaji wa pesa za umma,Nafikiri umesikia mh Rais namna suala hili lilivyomkera,hivyo Tuwe na subira watanzania maana Tunaamini hatua Kali za kisheria zinakwenda kuchukuliwa ,wahusika watapitishwa katika njia ya majuto na maumivu makali Sana kisheria ambayo itakuwa fundisho kwa watu wengine
 
Mfumo huo huo umempaa mamlaka ya kuchukua kuwajibisha wezi wa mali ya umma lakini yeye mwenyewe anashindwa.
Je kama yeye kapewa mamlaka ya kuwajibisha analalamika, je wananchi tufanyaje?

Kama anaturuhusu tuchukue sheria mkononi aseme tu
Hiyo sentence ya mwisho ni mfumo ambao tukifika huko tutakuwa tumesaidia kubadilisha mengi sana!
Na hutakiwi kusubiria ruhusa ya mtu!
 
Kuipiga chini CCM ni kukubali kumwaga damu tu vinginevyo hawawezi kuachia starehe ya madaraka ya nchi kwa style ya vikaratasi vya kura [emoji1787][emoji1787][emoji1787]!!!

Hilo mulisahau.
Huwa natamani nijitoe mhanga kabisa kuipoteza mbali sisiemu ila sasa kwa akili zetu kamwe haitoka madarakani na ata ikitoka ata wanao ingiza vyama vingine ni wale wale hakuna jipya ..Nchi iongonzwe ata kijeshi kwa muda hivi wakati huo kila kitu kinakuwa kinaenda kijeshi hutaki kula udongo ..baada ya muda wao ndio waweke mtu anaeweza sukuma gurudumu jembe siyo wanawake hawa hovyo kabisa.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Huwa natamani nijitoe mhanga kabisa kuipoteza mbali sisiemu ila sasa kwa akili zetu kamwe haitoka madarakani na ata ikitoka ata wanao ingiza vyama vingine ni wale wale hakuna jipya ..Nchi iongonzwe ata kijeshi kwa muda hivi wakati huo kila kitu kinakuwa kinaenda kijeshi hutaki kula udongo ..baada ya muda wao ndio waweke mtu anaeweza sukuma gurudumu jembe siyo wanawake hawa hovyo kabisa.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Mama watu wanacheza mziki wake kisha wanampiga kwa kumsifia sifia wanamtandika haswaa.
 
KWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE

1) Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.

Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa raisi kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.

Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake raisi eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo.

Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.

Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anaeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?

Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe.

China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi kusimamia vyeo kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali.
Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.

Raisi na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.

Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.

Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Nimeanza kuamini, kuna mtu alisema Samia atapita tu ila yupo atakayekuja kushika vizuri Urais.

Naamini pia Samia hawezi kuendelea 2025
 
Hiyo sentence ya mwisho ni mfumo ambao tukifika huko tutakuwa tumesaidia kubadilisha mengi sana!
Na hutakiwi kusubiria ruhusa ya mtu!
Kabisa mkuu

Mbona mtaani wezi wa kuku wanachomwa moto
 
Kabisa mkuu

Mbona mtaani wezi wa kuku wanachomwa moto
Wezi wa kuku wale wana njaa ya chakula. Wale tunawaonea sana.
Kuna haya majizi yaliyotengenezwa na mfumo wa ovyo wa ccm (mbeleko).
Hawana njaa... Ila ni walafi... wanakula na kutapanya! Raha yao wewe, yule, wale na Mimi sote tukose wapate wao alafu tuanze kuwaabudu!
Hawa inabidi tujitokeze umma wote kama tunavyojitokeza kwenye mikutano yao lakini sasa ni kwa malengo tofauti ya kuwatia adabu na kuwazomea.
Baada ya hapo ni kufanya civil disobedience Moja balaa kuwashika na kudhulumu haki ya kuishi mmoja baada ya mwingine!
 
Back
Top Bottom