Shazili mnali
JF-Expert Member
- Mar 25, 2023
- 362
- 569
Rais wa katiba kaingia madarakan haliyakua hajui wajibu wake nguvu yake. Daaah! inauma sana yan tumerudi zama za KIKWETE kila mbuzi anakula kwa ulefu wa kamba yake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena wanashindana kwa kumuimbia mapambio ili kumzuga zaidi !!Raisi ambaye anaangalia wezi wanaiba ndio raisi ambaye wapuuzi mnamtaka.
Mahakama zipi unazozungumzia mkuu, hizi hizi za bongo au?Mkuu mimi najua kwamba ni vigumu kwa nchi yoyote kutokomeza wizi serikalini. Hata huko Marekani kwenye mifumo bora ya uongozi, leo hii unasikia raisi mstaafu wa taifa hilo Donald Trump anataka kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa sababu zinazofanana na hizi tunazozungumzia hapa.
Ila sasa pamoja na kwamba ni vigumu kudhibiti wizi serikalini kwa 100%, kuna njia ambazo zinaweza kutumika japo kupunguza wizi huo kwa kiasi kikubwa na watu hawatokuwa tena wanailalamikia serikali kama ilivyo sasa. Ukisoma vizuri nilichoandika huko juu utanielewa.
Kwamba mtu anapopatikana na hatia ya wizi serikalini kitu cha kwanza kinachotakiwa kufanywa na raisi, waziri au kiongozi wake ni kumsimamisha mtu huyo na kuagiza akamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
1) Ikionekana kwamba mhusika hausiki na wizi bali alitengenezewa tu zengwe pengine kutokana na utendaji wake mzuri wa kuzuia upigaji, basi arudishwe kazini na ikiwezekana apandishwe cheo ili kutoa motisha kwa wengine kusimamia vyema maeneo yao ya kazi.
2) Ikionekana kweli aliiba basi afutwe kazi amepelekwe mahakamani ahukumiwe kifungo cha muda mrefu au arudishe fedha zote alizoiba na nyingine ya juu kama fidia ya wizi wake aliofanya.
Ikiwa tutakwenda kwa mwendo huo wengi wataogopa kuiba, na hivyo kupelekea wizi kupungua au kuisha kabisa serikalini.
Na huo ndio ukweli hakuna namna nyingine !!Ona huyu chawa!! Takataka kabisa, kuagiza polisi kuwakamata na kuwahoji watuhumiwa ni ubabe?
Hii nchi inahitaji kiongozi dikteta over
Mkuu tatizo la nchi hii ni zaidi ya ccm,CCM ni janga kubwa Sana hapa nchini.
Solution ya hiyo "laana" ni kuipiga chini CCM katika uchaguzi ujao
Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu (Yeremia 17:5)Raisi ambaye anaangalia wezi wanaiba ndio raisi ambaye wapuuzi mnamtaka.
Haswa.CCM ni janga kubwa Sana hapa nchini.
Solution ya hiyo "laana" ni kuipiga chini CCM katika uchaguzi ujao
Labda China 🇨🇳 Mtu akiiba pesa ya Umma anakula kitanzi !!Mahakama zipi unazozungumzia mkuu, hizi hizi za bongo au?
Na hawaguswi, sasa jiulize hio billion 500 ingeingizwa kwenye mishahara ni watu wangapi wangekuwa wamelipwa? 🤣 Ila hela yote hio imeliwa na kundi la watu wasiozidi 20.Hii nchi italiwa yote awamu hii
Daah kweli mwenye nacho anaongezewa sisi wanyoka tunakufa njaa na familia zetu watu wanajichotea hadi 500billion
Endeleeni kuiba kwa raha zenu.Ripoti ya CAG sio hukumu ya Mahakama,ikithibitika hatua zitachukukiwa..
Kumbuka Rais Samia sio mtu wa mihemko,kukurupuka na ku loose temper kirahisi ,ukifanya hivyo anaweza umiza wengi.
Na bado,muwe mnaelewa kwa nini CCM ni ukoo wa panya wote wapigaji tu wanazidiana viwango tu vya upigajiKWANZA HIVI NDIO VYEO VYAKE
1) Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2) Mkuu wa nchi na kiongozi namba moja kwa pande zote mbili za Muungano.
3) Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama.
Hivyo ni vyeo ambavyo vinamruhusu mheshimiwa raisi kuchukua hatua kwa mtu yoyote wa serikalini ambae anafanya kazi yake kinyume na sheria za nchi, aidha kwa yule anaeiibia serikali, anaetoa rushwa, anaepokea au kuchelewesha mipango ya serikali hasa inayohusu maendeleo nk.
Inasikitisha sana mtu mwenye vyeo hivyo anashindwa, au anasita kuwachukulia hatua kali za kuagiza wakamatwe na kufunguliwa mashtaka wale wote waliopatikana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma serikalini na badala yake raisi eti anawaomba tu waachie nafasi zao bila kufungwa au kurudisha fedha hizo ili zikatumike katika mambo mengine ya kimaendeleo.
Hata wale aliosema kwamba kila report zinapofika watu hao hao hukutwa na tuhuma zile zile ilitakiwa wakamtwe kwa tuhuma ile ile ya kwanza na kubanwa vizuri walipozipeleka fedha zetu, badala ya kutaka eti washushwe vyeo au kuhamishwa ofisi.
Yani mwizi wa ndala akamatwe na kufungwa huku mwanasheria wa serikali akitafuna kodi zetu kwa kuendesha kesi yake, afu yule anaeiibia serikali mabilioni ya shilingi ahamishwe tu kituo ili akaendelee na utafunaji wa fedha zetu huko katika ofisi nyingine. Ni kwanini asifukuzwe kazi ili nafasi yake ichukuliwe na mtu mungine na ukizingatia kuna watu wengi wana elimu zao mitaani lakini kazi hawana?
Lakini pia sio aishie kufukuzwa tu bali afunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na mali zake zote zitaifishwe na kurudishwa katika mikono ya wananchi.
China imeweza kupiga hatua duniani baada ya viongozi wa nchi hiyo kusimamia vyema kodi za wananchi wao kwa kutoa adhabu kali kwa yeyote atakaejaribu kugusa fedha za serikali.
Pia hata Rwanda ipo vizuri baada ya raisi wa nchi hiyo kukitumia vyema cheo chake.
Raisi na amiri jeshi mkuu ukibaki kulalamika, unafikiri mawaziri na viongozi wengine wa kawaida wataweza kuwa na uwezo wa kujiamini kuchukua hatua kweli.
Kama kulalamika umeshalalamika kwa zaidi ya miaka miwili sasa lakini upigaji ni ule ule. Sasa kabla ya kuwaambia watu na hili mkalitizame, tunakuomba na wewe kwanza ujitizame kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kuendelea ku deal na mafisadi.
Hebu tumia nguvu zako ulizopewa na katiba yetu kuwachukulia hatua wabadhilifu wa kodi zetu, kabla na sisi hatujaingia barabarani kama wakenya.
Ukicheka na nyani shambani usishangae kuvuna mabua.
Ni kweli wanasiasa ni kundi la watu wasiotaka kuongozwa . Ni kundi la watu wasioridhika na vipato vyao. Ni kundi la watu wenye uchu wa madaraka. Ni kundi la watu wanaopenda sana kujilimbikizia Mali . Nilimuona Waitara akilia machozi kila anapowaza kuwa uchaguzi ujao atashindwa vibaya .Binafsi naona vyama vyote Tanzania au Afrika vimeanzishwa kwa lengo kutafuna fedha za wananchi, ndomaana ukivichunguza hata uendeshaji wao ni wa upigaji upigaji.
Cha kufanya ni kuwa na wagombea huru ambao watagombea uongozi bila kupitia chama chochote cha siasa. Maana wanasiasa wote ni wezi, waongo na wanafiki.
Hapana Mkuu.Tatizo wala si SSH. Bali ni mfumo uliomfikisha hapo. Wengine wanadai Bora JPM lakini Mimi nasema mfumo kwenye Taifa la mamilioni ya watu haubadilishwi na mtu mmoja.
Fanyeni overhaul ya mfumo mzima uliotengenezwa na ccm.
Otherwise mtawalaumu sana wezi na Rais wenu.
Kwa hii mifumo iliyopo hata akija malaika mkuu Gabriel baada ya miezi kadhaa atakuwa mpiga Dili zaidi ya hawa waliopo!
Hiyo ni deal moja tu tena kwa watu wa kawaida tu !!Na hawaguswi, sasa jiulize hio billion 500 ingeingizwa kwenye mishahara ni watu wangapi wangekuwa wamelipwa? 🤣 Ila hela yote hio imeliwa na kundi la watu wasiozidi 20.
Kila nikiwaza hili naumia sana aisee. Sijui tumekosea wapi kupata maRais wasiojitambua.Mkuu unafikiri kuna rais pale?!!
Pale kuna kivuli tu kisichojitambua.
Inaonekana hata yeye mwenyewe haelewi mamlaka yake ni yapi, yupo kupiga mipasho tu.
Hahaha mimi sipendi kufoka foka hahahahTatizo la mama ni kutaka kuonekana mwema machoni pa kila mtu. Pia anaogopa kufuata nyayo za mtangulizi wake maana ashaonekana mara nyingi akimkataa. Sasa amejikuta haelewi nini afanye hivyo anajiendea tu.
Anajitengenezea Legacy yake ya kuacha Katiba, Astaafu kwa heshimaNimeanza kuamini, kuna mtu alisema Samia atapita tu ila yupo atakayekuja kushika vizuri Urais.
Naamini pia Samia hawezi kuendelea 2025