Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Rais Samia kaniangusha na kunisononesha sana ripoti ya CAG 2021-2022

Mkuu anazungumzia mfumo maanisha mfano Waziri kaiba pesa PCCB wanaweza kumkamata na kumshtaki bila kuwasiliana na Rais? Au Katibu mkuu kiongozi kafanya ufisadi je mkurungezi anaweza akamfungulia mashtaka bila kumuomba kibali Raisi?
Ndipo umuhimu wa Katiba unapokuja !!
 
Mkuu anazungumzia mfumo maanisha mfano Waziri kaiba pesa PCCB wanaweza kumkamata na kumshtaki bila kuwasiliana na Rais? Au Katibu mkuu kiongozi kafanya ufisadi je mkurungezi anaweza akamfungulia mashtaka bila kumuomba kibali Raisi?
Ndomaana nasema kwamba mfumo uliopo unampa raisi nguvu ya kumuwajibisha mtu yoyote anaeiibia serikali.
Kwahiyo kama mkurugenzi hawezi kumchukulia hatua katibu mkuu, basi raisi anao uwezo huo na autumie kunyoosha nchi.
 
Ndomaana nasema kwamba mfumo uliopo unampa raisi nguvu ya kumuwajibisha mtu yoyote anaeiibia serikali.
Kwahiyo kama kama mkurugenzi hawezi kumchukulia hatua katibu mkuu, basi raisi anao uwezo huo na autumie kunyoosha nchi.
Hapo hapo mkutanoni unaagiza wote waliohusika wakamatwe !! Hivyo ndivyo inavyotakiwa ! Bila hivyo miaka yote itakuwa ni kukopa na kuyaletea pesa majizi yazichukue !!
 
Hapo hapo mkutanoni unaagiza wote waliohusika wakamatwe !! Hivyo ndivyo inavyotakiwa ! Bila hivyo miaka yote itakuwa ni kukopa na kuyaletea pesa majizi yazichukue !!
Kweli kabisa. Raisi umeitisha kikao ambacho kimehudhuriwa na ..

1)mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama
2) mkuu wa jeshi lote la polisi
3) mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa
4) mkurugenzi mkuu wa Takukuru
5) mkurugenzi wa mashtaka
6) mwanasheria mkuu
7) jaji mkuu
8) na kadhalika

Alafu bado unashindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa wizi serikalini.

Unahofia nini tena na wakati hiyo list yote hapo juu iko mikononi kwako?
 
Nafikiri anaamisha hata hivyo vyama vingine vina wapigaji kibao, na hili lipo clear.

Cha kufanya ni kuwa na kiongozi ambae hatokani na chama chochote cha siasa.
Hata kwenye Chama tawala wapo watu waadilifu lakini wanashindwa kujua wafanye nini kwa sababu taratibu za kuanzisha Chama zimewekwa ngumu sana ili kuwazuia wenye nia njema wasipate nafasi ya kuanzisha Chama cha siasa kipya !! Na humo ndani ndio hawafurukuti kabisaaa ! Wanaogopa kushughulikiwa !!
 
Kweli kabisa. Raisi umeitisha kikao ambacho kimehudhuriwa na ..

1)mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama
2) mkuu wa jeshi lote la polisi
3) mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa
4) mkurugenzi mkuu wa Takukuru
5) mkurugenzi wa mashtaka
6) mwanasheria mkuu
7) jaji mkuu
8) na kadhalika

Alafu bado unashindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa wizi serikalini.

Unahofia nini tena na wakati hiyo list yote hapo juu iko mikononi kwako?
Wote wale wanasubiri Order tu ya Mkuu wa Nchi na Kazi ianze palepale !!
 
Hivi mtu aliyeiba biloni 300 utampeleka mahakamani ashindwe kwenye nchi ya kijamaa yenye mabepari walioko madarakani na wananchi wanaowaza kuwa mabepari.
Rushwa itahamia kwenye taasisi zitakazomchunguza na mahakamani . Hakimu Gani anayetaka kuwa maskini wakati anaona majaji ni mabilionea?
Polisi Gani au Takukuru Gani anayetaka kuwa maskini wakati serikali haiwezi hata kufidia familia yake anapokufa akiwa anapambana na majambazi au anapokuwa mlemavu Hana fidia maalumu ya kuhakikisha anaishi maisha mazuri pamoja na ulemavu wake ? Polisi mwadilifu akistaafu anachekwa na jamii nzima na KUONEKANA kuwa ana laana ya kudhulumu watu. Yaani waliofanya ufisadi wakapata fedha nyingi wao ndio jamii inawaona kuwa walikua wema na Mali walizo nazo ni baraka ya wema wao. Jamii isiyojua watu wema haiwezi kutoa viongozi Bora . Anahitajika mtu mmoja madhubuti atakayeitengeneza njia. Mtu mmoja ataifanya jamii kuwatambua na kuwatofautisha watu wa baya na watu wema.

Nchi kama hii hahitaji TU Bora peke yake Bali mtu mmoja anayeweza kuwanyoosha wahuni. Na kuhakikisha watu wanaogopa kuchezea Mali za umma.
JPM aliweza Kwa kiasi Fulani kupambana na wahuni japo wahuni walikua na mtandao mpana sana mana wamejikita kila Kona ndani ya Chama na serikali na wamejineemesha Kwa kiwango kikubwa sana . Wanaweza kuhonga yoyote . Hii nchi inahitaji Rais dikteta kamili. Anayeweza kutembeza chuma Kwa watu hata laki Moja. Yaani atakayesafisha mafisadi na wezi na vizazi vyao vyote bila hofu.
Yaani akijua kuwa Jaji amekula rushwa akatoa hukumu ya kumsafisha fisadi naye ananyooka naye. Kule Kenya tunaona majaji wanavyotumika kuidhoofisha serikali na kuwahalalisha mambo ya hovyo na Sasa kuhalalisha ushoga ,maandamano yasiyo na umuhimu wowote na yanayoweza kulifanya taifa kuwa kama Libya na wote wakaumia na nchi ikaporomoka kabisa kiuchumi .

Vinginevyo tukubali kuwa hakuna wa kumnyooshea mtu kidole zaidi ya Kuruhusu Demokrasia ifanye kazi Kwa uwazi na watu wabadili Chama ili wabadili sura za walaji na huenda watu wema nao wakaonekana.
Watu wengi wanachaguliwa au kuteuliwa kupitia connection ya kujuana na urafiki na undugu. Lakini connection nyingi zinapatikana kwenye starehe kama pombe ,uzinzi n.k. Hakuna connection nje ya hapo labda undugu na urafiki. Sasa kama mtu alimuunganisha mtu akateuliwa Kwa sababu ya ni kampani yake ya pombe au ni demu wake au mpenzi wake unategemea Kuwa Kuna uwajibikaji hapo ?

Faida ya kubadili Chama ni kubadili walaji na marafiki zao na jamaa zao Huko nako wanapeana Walevi na mahawara .
Kama sio Udikteta basi pawe na Demokrasia nje ya vyama vya siasa , angalau hapo kidogo inawezekana wakaanza kujitokeza watu wenye Nia njema na waadilifu wakajipenyeza.

Tumeona Kenya Raila na Uhuru wameungana kulinda Mali zao na familia zao dhidi ya Ruto anayeonekana kukerwa na watu waliopora Rasilimali za umma Kwa muda mrefu.

Chama kama Chadema na CCM ukiviangalia namna vinavyoendeshwa ni ubadhirifu mtupu. Yaani wamelenga Kupiga pesa tuu . Usione sijui mikutano sijui maandamano ni wizi mtupu. Kuna watu wanawaza kuuza tishrt, bendera, posho za safari, scafu, vitenge, majora ,kupamba majukwaa lakini sio kujenga ofisi rasmi na kuweka mitandao ya kuweza kujitangaza Chama kimtandao kama CCM ilivyokuwa Miaka ya 80 na ujenzi wa maofisi na maukumbi nchi nzima mpaka Leo ni Mali za Chama.
Sasa watu wanaowaza kuchwa kutwa maandamano na safari za kufanya mikutano hata wakiingia Ikulu watawaza hayo hayo mana hayana faida Kwa jamii zaidi ya kujinufaisha Kwa posho za safari na kumaliza fedha za taasisi au Chama.

Leo mtu akiiba ndani ya Chadema akafukuzwa atakimbilia CCM na ataonekana wa maana anaweza akatumiwa kwenye kampeni na kuwaponda wapinzani . Akiiba ndani ya CCM atahamishwa idara alimradi akae kimya ale urefu wa kamba yake.

Tuna watu wabunge 19 walisio na vyama kinyume na katiba ya nchi na kanuni za Bunge wanalipwa mabilion ya fedha ambazo zingetumika Kununua nafaka na kuweka kwenye ghala la serikali ili mahindi yasipande Bei lakini Bunge na mahakama ndio vimetumika kuhalalisha wizi na ufisadi huo. Sasa hapo katiba ndio mbovu au watu waliopewa dhamana ndio wabovu.
nimesihia hapo nilipoona jina la JPM nikajua anayeandika akili zake kama hazipo makalioni basi zipo chato
 
Hata kwenye Chama tawala wapo watu waadilifu lakini wanashindwa kujua wafanye nini kwa sababu taratibu za kuanzisha Chama zimewekwa ngumu sana ili kuwazuia wenye nia njema wasipate nafasi ya kuanzisha Chama cha siasa kipya !! Na humo ndani ndio hawafurukuti kabisaaa ! Wanaogopa kushughulikiwa !!
Kweli kabisa mkuu. Na hata wakifanikiwa kuanzisha basi watadumbukiziwa mamluki ambao kazi yao itakuwa kukichafua chama hicho kwa style ambayo waanzilishi wa chama hawataitambua mapema.
 
Kujiridjisha ni muhimu jawezi kuchukuwa hatua bila kuwa na ushahidi wa kutosha pili, hizo invoice zinapitia mikono mingi saana kwa wote walikosea ama kazi ya procurement inafanywa na mtu mmoja. Anyway yusubiri report ya TAKUKURU
 
Acha tusubiri mwisho wa haya yanayoendelea nchini.
 
Binafsi naona vyama vyote Tanzania au Afrika vimeanzishwa kwa lengo kutafuna fedha za wananchi, ndomaana ukivichunguza hata uendeshaji wao ni wa upigaji upigaji.

Cha kufanya ni kuwa na wagombea huru ambao watagombea uongozi bila kupitia chama chochote cha siasa. Maana wanasiasa wote ni wezi, waongo na wanafiki.
Good answer 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom