Rais Samia kasafiri na kundi kubwa la watu, kodi za Watanzania zinatumiwa vibaya

Ona huo msululu jamani. Halafu mzigo unakuja kurudi kwa watanzania kulipa kodi lukuku.

Kichekesho ni jana kasema timu ya olimpiki ilikuwa na viongozi wengi kuliko wanamichezo, lakini yeye leo yuko kwenye safari ya kiserikali na wanaccm ni wengi kuliko viongozi wa serikali? Hapo wazungu wanaachaje kuendelea kutuita manyani kwa mfano?
 
Mkuu ndio leo umejua kuwa mama wa kambo ni hewa? Haya bana.
 
Wanakwenda kuteta usijue! Wanakwenda kujifunza kwa kushuhudia namna kupoteza madaraka kama ilivyotokea kwa PF kunavyokuwa, ujue! Au, pengine hata amewabeba washauri wake apate maoni yao kuhusu mpango wake wa kuvunja Baraza la Mawaziri na kuuunda baraza jipya!?
 
Sio ndio vzr? Kusafirisafiri kwa viongozi huleta uhusiano Mzuri kimataifa.

Naona safari hii maisha yamekuwa nafuu mara baada ya mwenye Roho mbaya kuondoka ambaye hakutaka kusafiri, ambaye alikuwa anawanyanyasa watanzania ambaye.

Dhalimu hakutaka kusafiri kwenda nje ya maana kiingereza kilikuwa kinamsumbua. lakini safari zake za hapa nchini yalikuwa ni matumizi ya hovyo ya pesa za wananchi. Usidhani hatuna uwezo wa kutofautisha matumizi sahihi ya pesa za umma.
 
Yaani blunder za mama wa kambo ndio unataka kumsafishia yule dhalimu? Dhalimu atabaki kuwa dhalimu, huku mama wa kambo akiendelea kutokuwa mama.
 
Kichekesho ni jana kasema timu ya olimpiki ilikuwa na viongozi wengi kuliko wanamichezo, lakini yeye leo yuko kwenye safari ya kiserikali na wanaccm ni wengi kuliko viongozi wa serikali? Hapo wazungu wanaachaje kuendelea kutuita manyani kwa mfano?
Ndio maana ninasema ukiondoa mapungufu ya kibinadamu,kwenye mambo mengi MAGUFULI alikuwa sahihi
 
Dhalimu hakutaka kusafiri kwenda nje ya maana kiingereza kilikuwa kinamsumbua. lakini safari zake za hapa nchini yalikuwa ni matumizi ya hovyo ya pesa za wananchi. Usidhani hatuna uwezo wa kutofautisha matumizi sahihi ya pesa za umma.
Ndio maana nasema dhalimu aliyekuwa na kila uovu ameondoka. Furahini na kushangilia kwamaana aliyepo ni mtetezi wenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…