Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Hawa watu wasipoangalia watasababisha vurugu nchi hii
 
Watu so walishatoa maoini Yao? Kwani Ile rasimu ya Warioba ilipatikanaje kama siyo maoni ya wananchi? Acheni usanii....Rais amesema amesomeshwa dini yake vizuri, sasa kwanini anataka kumkosea Mungu wake hadharani mchana kweupe?
 
Hawa maraisi kila tunayemchagua anatumiaga techniques hizihizi za kusema wananchi hawaielewi katiba ya sasa[emoji3]jiulize huo utafiti waliufanya lini! hii ni mbinu ya kutumia panadol kwa mgonjwa wa malaria.
 
Elimu ya katiba bado sana nchi hii wanasiasa uchwara na wanaharakati wanadai katiba ili iwawezeshe kuingia ikulu wakati mambo ya muhimu mengi hakuna mwenye habari nayo. Namuunga mkono rais bado elimu inahitajika sana.
Tume huru isiyokuwa na manipulation ya mgombea yeyote (Kutokana na ukweli kwamba, asiwepo mgombea anayeitisha tume kwa namna yoyote Ile. Na hili nalo linahitaji elimu).
By the way, washindani kuwa na nafasi sawa, halihitaji MAONI ya wananchi( Hii ni OBJECTIVE APPROACH).
 
Kumbe na Samia anaiogopa Katiba Mpya akidhani ndio itamuondoa ikulu?!

Sasa hivi visingizio vyenu vya mpaka tufundishwe Katiba ya 1977 leo 2023, vina maana gani?
Hata katiba idondoke kutoka mbinguni kama ccm wakigoma kuachia madaraka hakuna chama cha upinzani kitachukua nchi
 
Ni kweli kabisa. 2025 inamtesa sana anajaribu Kuja fix zake. Hivi tuambie ni nchi gani ambayo wananchi wake wanajua katiba tofauti na Wananchi wa Bongo.

Anajidai kalelewa vizuri... Hivi kuelewa vizuri unaweza Kuja na uongo, hadaa na wizi wa aina hii. Please, God forbid.
 
Hicho kizazi Cha 2050-2070 sipati picha
 
Raisi yupo sahihi kabisa kuhusu uelewa wa Watanzania bila ya Kusahau kwamba naye ni Mtanzania. Itoshe, imepita miaka miwili na ushee toka ashike dola na Bado haijaielewa.

Ikumbukwe au izangatiwe pia, kuwa, mwaka wake watatu wa kuisoma na kuilelewa Katiba utakuwa ndio mwaka wake wa kuingia kinyang'anyiro cha Uraisi- Je atafaa kuwa Rais wa JMT kama haonyeshi nia ya kulinda Katiba hiyo ya Jamhuri, asiyoielewa? Haijalishi....wabobezi wa sheria wanadai "ignorantia legis neminem excusat"

Kwamba," kwamba mtu asiyejua sheria hawezi kukwepa dhima kwa kukiuka sheria hiyo kwa kutojua maudhui yake"

SSH hawezi kujifunika katika wingu la kutokuwa na Uelewa wa Maudhui ya Katiba yetu, kwani yeye amekuwa ni miongoni mwa viongozi walioapa Kutii na Kuilinda katiba hiyo, unaapa kufanya hivyo bila ya Uelewa wa unachokiapia? Je, anataka kusema kuwa Watanzania wengine hawana akili ya kung'amua yaliyomo kwenye Katiba yao? Kwamba hawana uelewa wa Katiba yao?
Tunapozingatia SSH ni miongoni mwa Watanzania na tunapozingatia hayo aliyoyasema ni kweli, basi Yeye binafsi hana pakutokea, narudia, haya kwamba mtu asiyejua sheria hawezi kukwepa dhima kwa kukiuka sheria hiyo kwa kutojua maudhui yake


Akemewe kwa Vijembe vyake, akemewe kwa kuwatukana Watanzania

2025 apumzishwe.
 
Hamna mabadliko ya sheria hadi zilizopo wananchi waache kuzivunja, mitaala ibaki ilivyo hadi pasiwepo na watoto wanaofeli, tusipitishe mabadiliko ya kodi mpaka wananchi waelewe zilizopo, na DP world wangoje wale wa Mpitimbi wasowahi kuagiza hata t-shirt wajue kuendesha bandari.
 
Hicho kizazi Cha 2050-2070 sipati picha
Watakuwa kama hawa waliopo sasa au watakuwa even worse kuliko hawa wanaimba honeeeey honeeey πŸ˜…πŸ™
Watu wanaogopa hata kukanyaga matope huko mashambani unategemea watazaa vizazi vya aina gani ??!
 
Maana yake hata yeye haijui katiba
 
Apumzishwe na nani ??!!πŸ˜…πŸ˜…πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…