Rais Samia: Katiba mpya hadi watu wasome waelewe maana ya katiba hata hii tuliyonayo

Elimu ya katiba bado sana nchi hii wanasiasa uchwara na wanaharakati wanadai katiba ili iwawezeshe kuingia ikulu wakati mambo ya muhimu mengi hakuna mwenye habari nayo. Namuunga mkono rais bado elimu inahitajika sana.
Hakuna ulazima vyama vya upinzani kuingia ikulu kama katiba mpya itapatikana jambo la msingi kila muhimili ujitegemee kama itatokea mbunge kazulumiwa ushindi wake basi atapata haki yake
 

Yote aya yalifanyika kwenye mchakato wa warioba , kwa nini tusiboreshe huo kwa muda mfupi tukaja na katiba mpya
 
Mama si aliwahi kuwa Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba? Wakati ule hakujua kwamba watanzania hawaijui katiba hata hii iliyopo? Kingine Rasimu ya katiba ya warioba ndio maoni halisi ga watanzania...

Tuijue au tusiijue atupatie katiba mpya. Aache uoga.
 
Tunakwenda kusomea chuo gani. Hii iliyopo waliekimishwa?
Swali la uzushi ni elimu ipi itafaa kwa hii katiba ya 1977 au ile mpya itakayoundwa. mimi nadhani katiba mpya yes itakapo pitishwa wananchi waelemishwe kwa vile hiyo ndiyo itakuwa hai na kitendea kazi kuendesha maisha yao. Busara, Tutunge katiba mpya elimu baadaye,Kamati ya Prof Mkandala nayo imebaini na kupendekeza hivyo kuhusu kipindi cha utoaji elimu
 
Mimi mama Abdul sijaielewa vizuri iliyopo! Nipeni muda angalau kila mwaka niwe nasoma ukurasa mmoja nikimaliza twende kwa wananchi. Hiyo itakuwa 2098, wote tuseme CCM HOYEE
 

Huyu mama ana ubongo wa Ki-Zanzibar;
 
Hakuna ulazima vyama vya upinzani kuingia ikulu kama katiba mpya itapatikana jambo la msingi kila muhimili ujitegemee kama itatokea mbunge kazulumiwa ushindi wake basi atapata haki yake
Sasa wenzako wa vyama wanataka katiba ibadilishwe ili waingie ikulu which ofcorse siyo mbaya lakini hawana nia njema na wananchi.
 
Ni bora CDM hawajashiriki huo mkutano wa kupotezeana muda. Acha washiriki hao wenye muda wa kupoteza.
 
..Ccm waachwe wang'ang'anie madarakani lakini wasiwanyime Watz mambo mengi mazuri yatakayopatikana kutokana na Katiba Mpya na Bora. Masuala ya chama kipi kitatawala ni component ndogo sana ktk Katiba nzima.
Tatizo wananchi hawapewi nafasi ya kujua mambo ya msingi wanayohitaji serikali iwafanyie. Walioshika kidedea mabadiliko wao wanaangalia ni namna gani wataingia ikulu. Rais yupo sahihi elimu kwanza itolewe.
 
Acha watu wakapige hela watakaopata nafasi ya kuzunguka kutoa elimu kwa wananchi
 
We form two hukusoma mada ya constitution kwenye somo la civics??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…