Umejitahidi kupotosha mkuu,
Alichosema ni kuwa, watu wapewe shule vizuri ya katiba hii tulionayo, na pia kasema vizuri kabisa, katiba ni ya watanzania, hatuwez sema tuchukue maoni ya wanasiasa tu ndio tuunde katiba, lazima kila mtu atoe maoni, na ili kila mtu atoe maoni ni lazima watu waijue hii katiba iliyopo, na yupo sahihi.
..suala la " kuijua " katiba iliyopo sasa hivi ni subjective.
..kwa mfano, Rais ametumia mbinu, utaratibu, na njia gani, kutambua kiwango cha uelewa wa wananchi kuhusu Katiba?
..Ni wakati gani Raisi atatoa tamko kwamba wananchi wanaijua katiba iliyopo, na wakati gani atatoa tamko kuwa wanaufahamu na katiba inayopendekezwa?
..Naamini wakati muafaka wa kutoa elimu ya Katiba ni kipindi cha KAMPENI ZA KURA YA MAONI kuhusu Katiba pendekezwa.
..Kwa msingi huo wakati wa kuandika Katiba Mpya ni sasa.