Rais Samia kayataka mwenyewe, alikuwa ameanza vizuri tu

Magufuli alilaaniwa na baadhi yetu kwa siasa zake hizo hizo ambazo leo mleta mada unaziona zina afadhali kuliko za sasa.

Mkuu awamu ya tano watu walificha pesa mpaka JPM akaongelea suala hilo hadharani, leo hii biashara nyingi mpya zinafunguliwa na hakuna anayeficha pesa.

Hakuna wamiliki wa bureau de change wanaoteseka kwa kunyang'anywa biashara zao mpaka wanapata presha zinazowaua kama ilivyokuwa awamu ya tano.

Kila rais anayekuwa ikulu hubebeshwa mzigo wa lawama, na mpaka akiondoka ndio tunakumbuka mema yake.
 
Ni nguvu ya wafadhili huko nje inayomuongoza Rais Samia. Tunategemea misaada kwa sehemu pana ya bajeti yetu na akawa hana cha kufanya ili mambo ya ndani yaweze kwenda vizuri.

Kukaa meza moja na wapinzani ni katika kutekeleza matakwa ya wenye pesa, hivyo huwezi kumsikia Rais SSH akiongea licha ya kutukanwa na kina Lissu tena matusi ya kukera sana.

Anachokifanya SSH kilimshinda JPM aliyekubali kufa na tai shingoni. Hakukubali kutii kila amri ya mzungu aliamini katika uhuru na jeuri ya mwafrika.
 
Kufuta upinzani na kuleta upya??Fara
 
Huu mkataba umeleta mpasuko mkubwa. Umefufua kwa nguvu JPM spirit. Na bahati mbaya, wanaoipigia debe wengi hawajiwezi kwa hoja, akili, ushawishi wala mvuto wa kisiasa.
Wamebaki kutukana watu mitandaoni. Kiburi si maungwana. Kusema kweli watanzania wamesema na wamesikika. Kuwadharau ni kujidharau wenyewe
 
Kila shetani na mbuyu wake Magufuli alikuwa na mazuri na mabaya yake lkn hakuwa na mawazo ya kuuza rasilimali za nchi kama huyu wa leo.
 
Yawezekana ni mchezo ndani ya CCM wanahakikisha avuruge kuelekea 2025 then watu wa Usalama waseme mama pumzika upepo umekugomea kabisa. Afu jamaa waibuke dk ya 90 ya mchezo kuchukua ndoo.
 
Ha ha ha ha ha tamaaa kwa kwenda mbele ccm ndivyo walivyo.
 
tulia maza ni bingwa

Sent from my CPH2371 using JamiiForums mobile app
 
Kila shetani na mbuyu wake Magufuli alikuwa na mazuri na mabaya yake lkn hakuwa na mawazo ya kuuza rasilimali za nchi kama huyu wa leo.
Tatizo naloliona kwako lipo kwa watanzania wengi.

Kuamini katika maneno ya upotoshaji yasiyo na ukweli wowote. Hakuna anayeuza nchi hata robo ya Mita moja.

Ni uwekezaji ambao hata Magufuli angeufanya kama angekuwa hai. Kwani SGR ilijengwa kwa ajili ya shughuli hii hii tunayomtukania Samia leo hii!!

Watanzania aliyeturoga keshakufa kitambo.
 
Magufuli hakupaswa kuwa kiongozi haswa ngazi ya urais, ndio maana aklitawaliwa na jazba. Eti kwamba afute upinzani alete upinzani wenye staha, kwani upinzani unawekwa na CCM? Kama unaingia madarakani kwa njia zisizo za staha, ni staha gani unaitaka baada ya kupora uchaguzi?
 
Mkataba usio na kikomo ni sawa na kuiuza tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…