Maigizo mara nyingi hayageuki na kuwa mambo halisi.Alipoingia madarakani Samia alikuja na hoja ya ‘Maridhiano’, hoja ambayo ilipokelewa vizuri na pande zote ingawa kwa shingo upande, baadhi hawakufurahishwa.
Samia ni muigizaji mzuri, mtu mwenye hadaa za kuwalaza akili watu kwa muda.
Aliigiza kuwa mtiifu na mfuasi mzuri wa Magufuli katika hali ngumu sana.
Mtu aliyemsoma wakati ule, akirudi leo na kumsoma Samia huyu tulie naye sasa hawezi kuamini kuwa ni mtu huyo huyo mmoja.
Lakini, pamoja na hadaa nyingi za maridhiano na CHADEMA, bado dalili za udanganyifu wake zilijitokeza mara kwa mara katika maridhiano hayo.
Jambo muhimu sana kwake alilosisitizia CHADEMA walizingatie, ni kuacha kumzodoa, kutumia lugha ya maudhi na mambo kama hayo.
Hili alilisisitiza, akijua kwamba katika mazingira ya aina hiyo, sura yake halisi itafunuka, kama inavyojionyesha sasa