Hizo siasa za mivutano mbona alizianza mapema tu, pale alipombambikia Mbowe kesi, aliyekuwa akiidai Katiba Mpya kaa nguvu, baada ya Samia kusikika akisema ukinipara nitakuparua.
Baada ya pale kelele za watu kudai Mbowe aachiwe huru zaidi ya miezi sita mfululizo ndizo zikamlainisha, akamtoa, na kumualika ikulu moja kwa moja akijua wazi alipogusa alikosea.
Baada ya hapo ndipo akaja na ile issue ya maridhiano, haya maridhiano aliyafanya akidhani wapinzani akiwemo Mbowe atawateka akili, hasa baada ya "kumtuliza" ikulu, kwamba hata akikosea mbele ya safari, hawatamgusa..
Bahati mbaya huu mkataba wa hovyo wa bandari umekuja kumvurugia kila kitu, sasa kazi kwake, naona uzalendo umeshaanza kumshinda, anawakabidhi hiyo kazi wakina Kingai ili wamsaidie kuwanyamazisha wanaozidai bandari zetu.
Sasa ngoja tuone, baada ya hii stage ya kwanza ya kuwaita na kuwahoji wala tusijue wanawaambia nini, watakuwepo waoga wataonyamaza, na wale wakaidi wataoendelea kuhoji, tuone next time watafanywa kitu gani na kina Kingai.