Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Kiongozi bila kuwa na dira yako si kiongozi. Kosa kubwa la Samia ni kukosa dira. Yeye amekuwa ansikiliza anti-Magufuli tu bila kuwa na dira yake mwenyewe. Anafuata uongozi wa Kikwete ambao pia haukuwa na dira yoyote zaidi ya kutaka kufurahisha wafuasi tu. Ukitaka kuongoza kwa kufurahisha watu basi huwezi kuongoza. Principle moja ya leadership ni "kukaza sauti kidogo."Siasa za mivutano ‘Confrontational Politics’ aliziweza Mwendazake, sidhani kama Rais Samia ataziweza.
Alipoingia madarakani Samia alikuja na hoja ya ‘Maridhiano’, hoja ambayo ilipokelewa vizuri na pande zote ingawa kwa shingo upande, baadhi hawakufurahishwa.
Kwa kiasi kikubwa siasa za vyama vya Upinzani hasa CHADEMA zilianza kupoa si kwa sababu ya vitisho vya vyombo vya dola bali walitegemea siasa za Rais Samia zinaweza kuwa tofauti na siasa za Mwendazake.
Hali imekuwa more of the same, imeanza kubadilika, mabadiliko haya naweza kusema yamechagizwa zaidi na ujio wa Mkataba wa Bandari.
Wananchi wameanza kusema wazi kuwa hawakubaliani na uamuzi wa Rais, yeye na wapambe wake wanasema anatukanwa.
Rais (CCM) kwa kutumia vyombo vya dola wanataka kuonesha wao ndio walioshika mpini, wanaompinga wameanza kushughulikiwa kama ilivyokuwa kipindi cha Magufuli.
Je, Samia ataziweza siasa za Mwendazake? Anao uhuru na uwezo wa kufunika kombe mwanahalamu apite ili amalizie kipindi chake.
Msikilize General Mwakiborwa kuanzia dakika ya 35:00