Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Sawa
 
Kwanza wewe hapo unalima hekari ngapi kwa mwaka?Mama ameongea na vijana ambao hata robo hekari hawezi lima.Sasa kijana huyu hata ukimpatia trekta na pembejeo bure,bado kwake anaamini kilimo ni kwa masikini na wasiofika vyuo vikuu.
Hata upewe trekta na kila kitu kama soko hamna unauzaje,,,unalima vizuri unakuta bidhaa imefurika sokoni
 
Naichukulia positive. Watanzanania tunahitaji change ya mindset kwa kuwa nyakati za Ku graduate na kusubiri placement ya Serikali hazipo.

Ni bora unapowapa watu kidonge kichungu wanywe lakini wapone ugonjwa.
Huwasaidii kwa kufanya hivyo utaonekana mpumbavu tu! The government has to show the way forward..Kama ni kupitia kilimo yatafutwe masoko yatakayopokea produce toka kwetu.

Estates zianzishwe na serikali watu wazalishe kama ni sukari ama mazao mengine yenye high demand in tonnes watu walime milango ya export iwe wazi ni ku conform na standards tu.

Masoko makubwa ma 4 au 5 yatabadilisha hali ya maisha ya graduates. Facilitation ya serikali ni muhimu kwa kufanikisha hilo sio kujiropokea tu upuuzi...Kulikwaga na Pamba na katani na watu walizalisha wakaishi vyema tu by that time.

Serikali isijondoe kwenye lawaMa katika hili hata kidogo its to be blamed inside out! Haijatekeleza wajibu wake vizuri. Wenzetu palipoendelea huko welfare ya wananchi ndio kazi kuu ya serikali. Huku watu wanagombania vyeo tu bila aibu.
 
Unavyoongea kirahisi kama vile kutemea mate kinyesi.
 
Tatizo nchi hii kuna kasumba ya kudharau kazi kama hizo. Tena vijana waliosoma wanaona fedheha kubwa kufanya hizo kazi. Lakini hiyo kasumba ingepigwa vita na kuondolewa vijana wengi wangefanya hizo kazi. Kama unavyowaona vijana wa kibongo wanabeba boksi Ulaya, wanaosha wazee, wanaosha masufuria hotelini, wanasafisha vyumba vya mahotelini wanalipwa na wanatuma hela kusaidia familia zao.
 

Umekula usiku huu kweli?

Njoo hapa bongo uoshe hayo masufuria kwny mahoteli/migahawa ambapo mshahara wake Ni utapewa ukoko wa wali uliochanganywa na maharage na buku 2 per day.

Hapa watu wanahudumia wazee wasiojiweza,wanawaogesha,kuwavisha pampus,kuwafulia nguo mshahara wao Ni Kati ya 60,000 mpk 100,000+ kulala na kula kwa mwajiri.

Hayo maboksi bongo utayebebea wapi?

Kusafisha hotel na kufua mashuka hizo kazi zipo na mshahara hata laki kwa mwezi haufiki na utafua Sana mavi ya wadau wale waasisi wa kutumia KY kwny hayo mashuka ya Lodge mpk utaikimbia kazi.

Kuna Maisha sasa hapo?
 
Soma nilichoandika uelewe kabla ya kukurupuka kujibu. Kazi za chini siyo lazima u housegirl na u houseboy au kusugua masufuria au kusafisha hotelini. Hata hizo kazi za kilimo na uvuvi zilizozungumzwa na Rais ni za chini. Sasa kama unalipwa laki 1 si ni bora kuliko kutokuwa na ajira? Ndiyo maisha hayo chochote ni bora kuliko kutokuwa na ajira. Vijana kutokuwa na ajira zozote hata zile ambazo unaona za chini ni hatari. Kumbuka "an idle mind is the devil's playground".
 
Too sad... anyway ndio maisha mkuu...usikate tamaa utapata tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…