Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Rais Samia amesema Vijana wengi wanasubiri Ajira wanapomaliza kusoma, lakini hawahangaiki kutafuta fursa za kazi. Ameeleza, "Kazi zipo nyingi Tanzania, ni Vijana kuchakarika, kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia"

Ametoa rai hiyo leo Januari 07, 2022 wakati akishiriki Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Amesisitiza, "Naombeni kaangalieni fursa za kazi. Fursa zipo nyingi na ni aibu kijana kukaa bila kazi"

Ameongeza, "Na hapa nitazungumzia changamoto inayofuata ambayo ni nyie Vijana kutokujua au kutotumia fursa zilizopo. Hamzitumii kabisa! Niwaombe sana Vijana, kuna fursa nyingi. Piteni Vyuoni mtaelekezwa jinsi ya kuziona fursa hizo"

Kuhusu changamoto ya Mitaji kwa Vijana amesema kuna Fedha za Halmashauri na Mifuko kadhaa ambayo inatoa Mikopo kwa Vijana imeanzishwa, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi kubwa ya Vijana

Sikiliza sehemu ya hotuba yake kuhusu Vijana na Kazi:

View attachment 2072394
Sawa
 
Kwanza wewe hapo unalima hekari ngapi kwa mwaka?Mama ameongea na vijana ambao hata robo hekari hawezi lima.Sasa kijana huyu hata ukimpatia trekta na pembejeo bure,bado kwake anaamini kilimo ni kwa masikini na wasiofika vyuo vikuu.
Hata upewe trekta na kila kitu kama soko hamna unauzaje,,,unalima vizuri unakuta bidhaa imefurika sokoni
 
Naichukulia positive. Watanzanania tunahitaji change ya mindset kwa kuwa nyakati za Ku graduate na kusubiri placement ya Serikali hazipo.

Ni bora unapowapa watu kidonge kichungu wanywe lakini wapone ugonjwa.
Huwasaidii kwa kufanya hivyo utaonekana mpumbavu tu! The government has to show the way forward..Kama ni kupitia kilimo yatafutwe masoko yatakayopokea produce toka kwetu.

Estates zianzishwe na serikali watu wazalishe kama ni sukari ama mazao mengine yenye high demand in tonnes watu walime milango ya export iwe wazi ni ku conform na standards tu.

Masoko makubwa ma 4 au 5 yatabadilisha hali ya maisha ya graduates. Facilitation ya serikali ni muhimu kwa kufanikisha hilo sio kujiropokea tu upuuzi...Kulikwaga na Pamba na katani na watu walizalisha wakaishi vyema tu by that time.

Serikali isijondoe kwenye lawaMa katika hili hata kidogo its to be blamed inside out! Haijatekeleza wajibu wake vizuri. Wenzetu palipoendelea huko welfare ya wananchi ndio kazi kuu ya serikali. Huku watu wanagombania vyeo tu bila aibu.
 
Sio aibu tu, Bali ni fedheha.
Yaani kwa fursa zilizopo Tanzania kijana unakosaje kazi.

Umeshindwa kulima,
Umeshindwa kufuga,
Umeshindwa hata kutengeneza funza uwauizie wafugaji kuku.
Umeshindwa kutengengeneza hydroponic folder uwauzie wafugaji.
Umeshindwa hata kutafuta pori ukapande majani ya ng'ombe(hayahitaji mbolea Wala kumwagilia) upige hela

Ukiziorodhesha zinaweza zikafika laki Saba
Unavyoongea kirahisi kama vile kutemea mate kinyesi.
 
Tatizo nchi hii kuna kasumba ya kudharau kazi kama hizo. Tena vijana waliosoma wanaona fedheha kubwa kufanya hizo kazi. Lakini hiyo kasumba ingepigwa vita na kuondolewa vijana wengi wangefanya hizo kazi. Kama unavyowaona vijana wa kibongo wanabeba boksi Ulaya, wanaosha wazee, wanaosha masufuria hotelini, wanasafisha vyumba vya mahotelini wanalipwa na wanatuma hela kusaidia familia zao.
 
Ajiuzulu urais aje tutafute nae kazi aone kama zipo kweli.

FC0908A5-36AB-45DB-801D-580442EFD683.jpeg

975B49CC-668A-4C4A-9A0E-4C8A3F2B357B.jpeg
 
Tatizo nchi hii kuna kasumba ya kudharau kazi kama hizo. Tena vijana waliosoma wanaona fedheha kubwa kufanya hizo kazi. Lakini hiyo kasumba ingepigwa vita na kuondolewa vijana wengi wangefanya hizo kazi. Kama unavyowaona vijana wa kibongo wanabeba boksi Ulaya, wanaosha wazee, wanaosha masufuria hotelini, wanasafisha vyumba vya mahotelini wanalipwa na wanatuma hela kusaidia familia zao.

Umekula usiku huu kweli?

Njoo hapa bongo uoshe hayo masufuria kwny mahoteli/migahawa ambapo mshahara wake Ni utapewa ukoko wa wali uliochanganywa na maharage na buku 2 per day.

Hapa watu wanahudumia wazee wasiojiweza,wanawaogesha,kuwavisha pampus,kuwafulia nguo mshahara wao Ni Kati ya 60,000 mpk 100,000+ kulala na kula kwa mwajiri.

Hayo maboksi bongo utayebebea wapi?

Kusafisha hotel na kufua mashuka hizo kazi zipo na mshahara hata laki kwa mwezi haufiki na utafua Sana mavi ya wadau wale waasisi wa kutumia KY kwny hayo mashuka ya Lodge mpk utaikimbia kazi.

Kuna Maisha sasa hapo?
 
Soma nilichoandika uelewe kabla ya kukurupuka kujibu. Kazi za chini siyo lazima u housegirl na u houseboy au kusugua masufuria au kusafisha hotelini. Hata hizo kazi za kilimo na uvuvi zilizozungumzwa na Rais ni za chini. Sasa kama unalipwa laki 1 si ni bora kuliko kutokuwa na ajira? Ndiyo maisha hayo chochote ni bora kuliko kutokuwa na ajira. Vijana kutokuwa na ajira zozote hata zile ambazo unaona za chini ni hatari. Kumbuka "an idle mind is the devil's playground".
 
Sisi watoto wa masikini kilio chetu kuna siku kitasikika tu maana tunasoma kwa shida ajira hakuna na unakuta mtu kapata ajira kwa koneksheni maana ni mtoto wa kibopa fulani arafu hajawahi ijua shida ni nn hata akitutukana kulala njaa ni uzembe ni sawa tu maana hawajui kuna kukosa acha tukejeliwe si sisi si ndo tunawachagua watuboreshee maisha wanaishia kutusimanga ila poa tu one day yes.
Too sad... anyway ndio maisha mkuu...usikate tamaa utapata tu.
 
Back
Top Bottom