Rais Samia: Kazi zipo nyingi Tanzania, ni vijana kuchakarika na kuona fursa

Ndio inavyotakiwa ,Safi Sana kwa kuwaeleza .Kuna mamikopo yasiyo na Riba inatolewa na Halmashauri lakini Kazi yao kuchat kulalamika sasa sijui wanategwmea nini
 
Minadhani sio kila wakati lazima kiongozi atoe neno kwanye mahafali. Ifike basi hata viongozi wajifunze kukaa kimya baada ya salam tu.
Wanatafuta umaarufu ambao kimsingi tayari wanao.

Hawajui kabisa kuwa kwa maneno yao wanakuwa wanatonesha madonda ya walio wengi wasiyo na ajira.

Anasema vijana wajiajiri wakati hiyo mitaji watu wanaisikia kwenye tbc na channeli ten
 
Hawana tofauti na wewe unayeshinda lumumba ukiwaramba miguu mabosi wako.

Unapotupiwa sh 10000 basi umemaliza kazi na kujiona wewe ndiyo Sanko wa dsm.
 
Ndani ya miaka 3 jinsi ya kuleta maendeleo na kumaliza tatizo la ajira nchini.
1.Ondoa futa kodi zote za kuingiza magari ya mizigo na abiria nchini kodi yake utaipata mara mbili yake kupitia indirect tax.Kwenye mafuta,leseni za udereva,fine za traffic, parking fee,ushuru wa stand,spare za magari,leseni na vibali mbalimbali.Gari moja uajiri si chini ya vijana 3.
2.Toa ruzuku kwenye viwanda vya kuzalisha matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei trekta moja uajiri zaidi ya watu wanne.
3.Jenga schemes za umwagaliaji KILA kijiji upitapo mto pande zote mbili watu walime mwaka mzima ni aibu sana kwa maji ya mito kumwaga maji yake baharini badala ya mashambani.Soko la mazao nje ya nchi lipo tele
4.Jenga vyuo vya ujuzi kila kata kopesha vijana ujuzi baada ya kumaliza darasa la saba wakapate ujuzi wautakao.
Kukopesha vijana waende chuo kikuu kisha warudi mtaani kuendesha bodaboda na kuwa machinga ni upotevu Mkubwa Sana wa kodi zetu na kuongeza idadi ya masikini nchini.
5.Fungua mipaka watu wauze watakapo nje ya nchi kuna masoko tele.Legeza masharti ya vibali Ili export ikue.
Ni sekta mbili tu zingine takataka hazifikii kilimo na madini kwa kuajiri vijana wote nchini na kuongeza pato la taifa bila kutegemea kukopa na kukamua kodi wananchi.
6.Peleka KILA kijiji mashine za kutengeneza interlocking block na vigae Ili watz wote wajenge nyumba bora kwa gharama nafuu kabisa
Mjerumani kwa miaka 15 alituletea maendeleo makubwa Sana ccm imeshindwa nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…