Rais Samia kuanza safari ya kikazi nchini DR Congo

Yule mwingine alikuwa hasafiri watu wakasema anasababisha nchi kuwa na mahusiano mabaya ya nje,sasa huyu mwingine anatoka naye wanasema anatafuna kodi za wananchi,sijajua bado watanzania tunataka raisi wa aina gani...

Labda malaika....

#KaziIendelee
 
Umesoma nilichoandika?Wapi nimepinga Rais kusafiri?Hoja yangu ni kwamba Rais anapotoa kipaumbele cha kusafiri kwenda Congo,Burundi sijui Zimbabwe,je hizo ndiyo nchi zenye tija kwa Taifa letu kuliko nchi nyingine duniani?
Nchi nyingine zipi zenye tija kwa uchumi wetu mkuu? Za magharibi zinazotupa mikopo ya masharti makubwa au?
 
Msafara wake una watu wangapi? Kuna nini huko?
 
Wajumbe wa msafara kina nani? Wale wazee wa Saigon waliokuwa wanatafuta wawekezaji enzi zile inabidi watupe mrejesho
 
Hakuna sehemu niliyopotosha.....unapotosha ili nionekane mpotoshaji?!!!

Mtiririko wa comments zangu uliangazia tija ya safari za mh.Rais na nchi zinazotuzunguka...nikatolea mfano wa Burundi,Zambia ,Kongo(land locked countries) na matumizi ya bandari yetu kwao.....nikauliza kwa hiyo bandari yetu haina tija.....ukaja na kusema sina STATISTICS za wao KUTUINUA KIUCHUMI.....nikaendelea kukutaka UNIWEKEE STATISTICS zako kinzani....matokeo yake hujaniwekea na unang'ang'ana tu kuwa NIMEPOTOSHA...khaa😲😲😲
 
Wengine wanataka labda aende UJERUMANI....

Mathalani Ujerumani ni marafiki zetu Sana.....lakini tukumbuke ya kwamba ni miaka tu ya karibuni ambako BAADHI YA WABUNGE WA CDU (marafiki wa Chadema) wakiwa ndani ya BUNGE lao(BUNDESTAG) walitupinga TUSIENDELEE NA UJENZI wa kituo cha uzalishaji wa megawati 2200 za umeme pale Mwalimu Nyerere....kisa tutaharibu TURATHI la dunia la SELOUS.....

#KaziIendelee
 
Kuwauzia bidhaa/mazao maskini wenzetu hatutapiga hatua yoyote. Tutafute masoko huko dunia ya kwanza.
 
Safari zao ni vinchi vya ovyo tu kama jiwe
Huwezi kusikia wameenda ulaya na marekani
Au wanaziogopa cnn na fox news
 
Umepotosha uma kwa sababu huwezi kuibuka tu na kusema kuwa Congo au Burundi ina tija kuliko nchi nyingine duniani kwa hiyo inafaa kupewa kipaumbele katika ziara za Rais wakati huna ushahidi unaosupport kauli yako hiyo.

Unapoongea masuala yanayohitaji shahidi za data bila kuwa na shahidi hizo ni upotoshaji.
 
Safi sana, hii ndio staili yake ya kukuza na kudumisha uhusiano kati ya nchi yetu na nchi nyingine ikiwa ni pamoja hizi za majirani wetu. Binafsi sioni ubaya wala tatizo to this approach by our President. Si mnajua in life, kila mtu na in this sense, kila kiongozi, ana staili yake na approach yake ya kutawala na kuongoza nchi na watu wake na kufanya vile anayodhani ndiyo NJIA NA APPROACH SAHIHI ya kufikia malengo yake ya muda mfupi na muda mrefu kwa manufaa ya nchi na watu wake.
 
Mkuu, umesomea uchumi?
Kama jibu ni Ndiyo basi unatumia vibaya taaluma yako kutetea Uzurulaji wa Miss Vasco da Gama.
Wewe unawaza ujenzi wa Reli na uwepo wa Bandari uta/unasaidia kukuza Uchumi wetu ila wachumi na Viongozi wetu wameona Tozo ndo zitasaidia kukuza Uchumi.
 
Nchi nyingine zipi zenye tija kwa uchumi wetu mkuu? Za magharibi zinazotupa mikopo ya masharti makubwa au?
Siyo kweli kwamba nchi za Magharibi huwa zinatupa mikopo ya gharama kubwa kwa kuwa tumeshuhudia mara nyingi nchi hizi zikitoa mikopo ya gharama nafuu hata mara nyingine kutusamehe mikopo hiyo.
 
Siyo kweli kwamba nchi za Magharibi huwa zinatupa mikopo ya gharama kubwa kwa kuwa tumeshuhudia mara nyingi nchi hizi zikitoa mikopo ya gharama nafuu hata mara nyingine kutusamehe mikopo hiyo.
Kweli tunahitaji kubishana on this kuwa nchi za magharibi huwa zinatupa au hazitupi mikopo migumu na yenye masharti magumu!? Kweli hakuna ajuaye haya na namna walivyotuwekea ngumu juu ya ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere huko Rufiji, eti kwa kigezo cha kuharibu mazingira ya Selous Gama Reserve!? Hakuna ajuaye hili na mengine mengi!? Tusijifanye hamnazo kwa mambo yaliyo wazi!
 
Naam!

Rais wa Jamhuri ya MUUNGANO WA TOZO.
Hayo ni maneno ya watu wasioitakia mema na maendeleo nchi hii; ni mfano mzuri wa mchawi anayetaka kukulelea mwanao kwa nia ya kumtumia kichawi! Ndivyo walivyo wasioitakia mema nchi, watatoa majina mengi ili kuwakatisha tamaa wazalendo wa nchi hii katika kujenga uchumi na kujiletea maendeleo yao. Hivi hiyo misaada kutoka Japani au Amerika au Uchina na kwingineko, unadhani wao wanazipata wapi kama siyo kwenye KODI NA TOZO ZA WATU WAO!? Hebu tujiongeze kwa faida ya nchi yetu.
 
Sio nchi hii mtu anaiba mabilioni ya pesa anakaa miaka yake mitano jela, anapigwa faini ya milioni 8 anaenda kutumia uswahilini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…