tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha upigaji mkubwa wa fedha za umma, Mh Rais Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajia kutengua uteuzi wa mawaziri ambao wizara wanazozisimamia zilionyesha upigaji mkubwa. Aidha, wakurugenzi ambao halmashauri zao zilipewa hati chafu nao watafyekelewa mbali na panga la Mh Rais. Na wale waliopata hati zisizoridhisha watahamishwa vituo vyao vya kazi ili kupewa nafasi ya mwisho kujirekebisha.
Kana kwamba hii haitoshi, inasemekana vigogo wote ambao walihusika moja kwa moja au kwa kushindwa kusimamia taasisi zao na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma, nao watasombwa na mafuriko haya na wengi wao watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria. Moto wa mama umewaka. Waliodhani anatania siku alipochukia na kuwatukana stupid, msidhani alikuwa anatania. Mbivu na mbichi lazima zijulikane. Hakuna hata mtu mmoja atakayechezea fedha za umma akabaki salama. Taarifa hizi zimepenyezwa na watu walio karibu na utawala.
MAONI YANGU
Namuunga mkono mama Dr Rais Samia kwa kuwachukulia hatua watendaji waloshindwa kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuwashughulikia mafisadi wote lakini nashauri jambo hili lifanyike kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha kwamba ni wale tu waliohusika na uzembe au ubadhirifu ndio wanachukuliwa hatua kali. Isitokee watu wasiohusika kuingizwa kwenye mkumbo. Utawala washeria sharti uchukue nafasi yake.
Nawasilisha.