Tetesi: Rais Samia kubadilisha Baraza la Mawaziri hivi punde

........bora afanye hivyo, itakuwa onyo kali hasa Kwa wale wanaodhani Bi. Mkubwa ni dhaifu na kwamba kuwepo kwake madarakani kunawafanya wawe juu ya Sheria, she plays very smart, btw she can......
 
Mkuu let us wait and see what kind of reshuffle she will make. I bet many ministers will be sacked.
 
Mpaka sasa zimerudi ngapi hazina?
Au ni porojo zilezile za kubadilisha upepo?

Tumechoka mambo ya kubadilisha badilisha tunataka watu warudishe hela zetu na wakishindwa wafungwe
( ambalo tunajua ni ndoto) ila acha tujifariji masikini
 
"Hivi punde" maana yake ni muda mfupi ujao ndani ya siku hii ya leo au ndani ya dakika chache zijazo, au ndani ya lisaa hili tulilonalo muda huu
 
story za vijiweni ni za kuziacha hapohapo, ukimaliza gahawa, rudisha kikombe na story ziache hapo!
 
Kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha upigaji mkubwa wa fedha za umma, Mh Rais Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajia kutengua uteuzi wa mawaziri ambao wizara wanazozisimamia zilionyesha upigaji mkubwa. Aidha, wakurugenzi ambao halmashauri zao zilipewa hati chafu nao watafyekelewa mbali na panga la Mh Rais. Na wale waliopata hati zisizoridhisha watahamishwa vituo vyao vya kazi ili kupewa nafasi ya mwisho kujirekebisha.

Kana kwamba hii haitoshi, inasemekana vigogo wote ambao walihusika moja kwa moja au kwa kushindwa kusimamia taasisi zao na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma, nao watasombwa na mafuriko haya na wengi wao watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria. Moto wa mama umewaka. Waliodhani anatania siku alipochukia na kuwatukana stupid, msidhani alikuwa anatania. Mbivu na mbichi lazima zijulikane. Hakuna hata mtu mmoja atakayechezea fedha za umma akabaki salama. Taarifa hizi zimepenyezwa na watu walio karibu na utawala.

MAONI YANGU
Namuunga mkono mama Dr Rais Samia kwa kuwachukulia hatua watendaji waloshindwa kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuwashughulikia mafisadi wote lakini nashauri jambo hili lifanyike kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha kwamba ni wale tu waliohusika na uzembe au ubadhirifu ndio wanachukuliwa hatua kali. Isitokee watu wasiohusika kuingizwa kwenye mkumbo. Utawala washeria sharti uchukue nafasi yake.

Nawasilisha.
Akimtoa nchemba tu na makamba urais npaka 2040
 
Huyo tumeshazoea kauli zake za kuonyesha kuwa anataka kufanya mabadiliko makubwa lakini anaishia maneno tu au anagusagusa tu hapa na pale bila kufanya mabadiliko ya maana.

Tatizo la msingi ni waziri mkuu siyo hawa mawaziri wadogo.

Waziri mkuu ameshindwa kumsaidia yeye Samia, na wala hakumsaidia ipasvyo Magufuli kuthibiti ufisadi kwenye halmashauri huko.
 
🤣🤣🤣yani muda huu mshaketi kwenye vijiwe vya kahawa na kashata?mbona bado mapema Sana,hii ni gahawa ya mchana,chungu kumesa🤔
 
Huyu Mama adhabu yake kali kabisa ni kuwaita wezi "Mastupid" imeisha hiyo watu wanajipigia kwa uhuru wa Manyani.
 
Naona waziri Ulega anaziara za vyombo vya Habari kujikomba kwa Wana chi kuomba huruma ya Wana nchi, ngoja tuone yajayo yanafurahisha
 
Tusubiri tuone mkuu. Wakati ukuta. Safari hii mama Samia lazima apindue kila jiwe. Tumechoka kuibiwa fedha zetu na mafisadi kila kukicha.
labda watabadilishwa wapishi wa ikulu. wa Dar waende Dodoma na wa kule waletwe Dar.
 
Hawezi kubadirisha Baraza la Mawaziri wakati Bajeti zinaendelea kuwasilishwa Bungeni.

Hilo la Wakurugenzi anaweza lakini sio Baraza la Mawaziri.

Kama kutakuwa na mabadiriko kwenye Baraza la Mawaziri basi itakuwa baada ya kumalizika Bunge la Bajeti mwezi Juni.
 
Kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha upigaji mkubwa wa fedha za umma, Mh Rais Dokta Samia Suluhu Hassan anatarajia kutengua uteuzi wa mawaziri ambao wizara wanazozisimamia zilionyesha upigaji mkubwa. Aidha, wakurugenzi ambao halmashauri zao zilipewa hati chafu nao watafyekelewa mbali na panga la Mh Rais. Na wale waliopata hati zisizoridhisha watahamishwa vituo vyao vya kazi ili kupewa nafasi ya mwisho kujirekebisha.

Kana kwamba hii haitoshi, inasemekana vigogo wote ambao walihusika moja kwa moja au kwa kushindwa kusimamia taasisi zao na kusababisha upotevu mkubwa wa fedha za umma, nao watasombwa na mafuriko haya na wengi wao watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria. Moto wa mama umewaka. Waliodhani anatania siku alipochukia na kuwatukana stupid, msidhani alikuwa anatania. Mbivu na mbichi lazima zijulikane. Hakuna hata mtu mmoja atakayechezea fedha za umma akabaki salama. Taarifa hizi zimepenyezwa na watu walio karibu na utawala.

MAONI YANGU
Namuunga mkono mama Dr Rais Samia kwa kuwachukulia hatua watendaji waloshindwa kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuwashughulikia mafisadi wote lakini nashauri jambo hili lifanyike kwa umakini mkubwa kwa kuhakikisha kwamba ni wale tu waliohusika na uzembe au ubadhirifu ndio wanachukuliwa hatua kali. Isitokee watu wasiohusika kuingizwa kwenye mkumbo. Utawala washeria sharti uchukue nafasi yake.

Nawasilisha.
Mungu amuwezeshe kufanya hayo.
Isiwe ni tetesi tu
 
Back
Top Bottom