Tetesi: Rais Samia kubadilisha Baraza la Mawaziri hivi punde


Kaa kwa Kutulia , Mfa Maji hakosi kutapatapa, Magu hapa anakujaje !
 
Huwa tunawaambia hapa, the two best presidents of our country ni:
• Mwl Julius Kambarage Nyerere (Baba wa Taifa)
• Mwl John Pombe Magufuli (Baba wa Uchumi)
Mh! Huyo namba 2 mwizi, mtoe kwenye orodha mkuu.
 
Hana huo uwezo, akibadili chochote this time ataishia kugusa ma-DAS tu.

Huko kwingine hawezi kugusa mpaka kwa ruhusa maalum tu.
Soma hapo juu vizuri,amesema this time hatanii tena...
 
Sahauni kuona Mwigulu Nchemba akitolewa hapo Finance Docket kwani ndiyo anasababisha Mama kupata Pesa nyingi za Misaada ya Wazungu kutokana na Maandiko yake hivyo Mama anampenda mno na hapo hatomtoa ng'o.

Nimemaliza.
Mhe.Mwigulu anafanya kazi nzuri sana.Wizara hiyo ina changamoto nyingi sana.Lakini anajitahidi sana kuzikabili.
 
KWENYE WIZARA YA FEDHA AKIKALISHWA DR. KIMEI, DR. SAMIA ATAPUMUA KWELI KWELI, BECAUSE HE KNOW HOW TO FIND CASH, AND PLAN IT BETTERLY FOR FUTURE.!
 
Ndani ya siku chache zijazo mkuu; hata wiki haiishi.
Ikitokea kama ulivyobashiri (ndani ya wiki hii) naomba uni-tag ili niweze kukupa credits zako. Isiipotokea vile vile, naomba uni-tag pia. Tafadhali naomba usiache
 
Mhe.Mwigulu anafanya kazi nzuri sana.Wizara hiyo ina changamoto nyingi sana.Lakini anajitahidi sana kuzikabili.
Leta ushahidi mkuu, usiongee maneno matupu.
 
Huwa sielewi jambo moja, hao wakitolewa huwa inasaidia nini? Alafu pia wakitolewa leo, baada ya miaka miwili mbele wanarudishwa.

Kusema ukweli kabisa bado naona kuna watu hatujui tunataka nini. Adhabu ya mtu aliyefuja pesa ya serikali sio kutolewa kwenye nafasi yake. Adhabu zipo na zimeainishwa kisheria kabisa

Tokea raisi aingie ameshawatema mawaziri wengi tu na wengine kawabadilishia wizara, lakini pamoja na hayo umeona Kuna tija gani hadi Sasa? Kipi kitakua cha ajabu akiwatoa sasa?

.............
 
Kama ni kweli basi itakuwa ni hatua moja nzuri mbele.
Hatua nzuri mbele? Ukimtengua ntu aliyeiba oesa huwa inasaidia nini?

Mkapa alitengua, kikwete alitengua, Magufuli alitengua, Samia ameshatengua. Hebu sasa tujiulize inasaidia nini? Tena waziri anayetenguliwa leo sababu ya ubadhirifu ndio atateuliwa kesho akija raisi mwingine
 
Kweli kabisa mkuu. Wale jamaa asipowang'oa watamharibia sana kwenye uchaguzi wa 2025. Lakini ngoja tusubiri tuone jinsi itakavyokuwa kwa kuwa yeye ndiye mwenye maamuzi ya mwisho. Tusiandikie mate ilhali wino upo.
Hii comment imeonyesha kiwango cha chini. Mwigulu au makamba wakitolewa kwenye uwaziri inasaidia nini? Kiwatoa kwenye uwaziri inahusianaa vipi na yeye kwenye uchaguzi wa 2025?

Unataka kusema kuna watu hawatampigia kura kwa kuwa mwigulu na makamba wapo? Pia unataka kusema tatizo la serikali ya sasa ni mwigulu na makamba?

Mimi nadhani hatujui tatizo letu kubwa ni lipi
 
Kutengua bila uwajibishaji ni bure tu na atakayeingia atapiga anajua atatenguliwa ila atakuwa kakusanya pesa ambayo kwa mshahara wake asingeikusanya kwa miaka 100
Ndio hili hata mimi kila mara nahoji. Ukimtengua waziri kwa sababu ya ubadhirifu inasaidia nini zaidi ya kumpa likizo ya kutumia pesa alizopiga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…