Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili Nchini Kenya kuanzia 04|05|2021

Pengine wana anchor interest za mabeberu katika EAC. Tumeshaona ile controversial contract walioingia na UK bila ya nchi za jumuia ya EA kuridhia.
 
Pengine wana anchor interest za mabeberu katika EAC. Tumeshaona ile controversial contract walioingia na UK bila ya nchi za jumuia ya EA kuridhia.
Mkuu, shikilia hapo hapo; kumbe tupo pamoja.

Maana yangu ilikuwa inalenga huko, na tutakwenda tu taratibu kuyafunua haya.

Ni COVID-19 tu ndiyo imekuja kutifua, na kufifisha kasi. Lengo ni kuifanya nchi hiyo kama kituo kikuu cha hao wakubwa wakisimamia maslahi yao kwenye ukanda huu.

Ndiyo maana ya "AnchorNation"

In real terms, it is a satellite state.
 
Ku deal na Kenya kwakutumia akili tu hutawaweza, niwa kora wa ajabu. Hapa ubabe lazima uchanganywe kwenye hiyo equation.
Hawatuwezi kwa akili wale. Hakuna haja ya ubabe. Watu wanakutegemea uwalishe unatumia ubabe wa nn? Akili tu maana wanakuhitaji. Lazima wale. Na ss tunahitaji mazao yawe na soko.
 
Hawatuwezi kwa akili wale. Hakuna haja ya ubabe. Watu wanakutegemea uwalishe unatumia ubabe wa nn? Akili tu maana wanakuhitaji. Lazima wale. Na ss tunahitaji mazao yawe na soko.
Mkuu usilale usingizi ukategemea utaendelea kuwalisha kila siku. Wameanza kupokea mahindi kutoka DRC. Si umesikia wameshapeleka jeshi la kulinda amani DRC. Jiulize jeshi la Kenya na DRC wapi na wapi. Wamewashindwa Alshababu sasa wanawafuata Interahamwe ili walinde mashamba ya mahindi ya wakubwa zao.
 
Chonde chonde mama Samia, uwanja wote wako lakini suala la kuchangia ardhi yetu na movements za holela holela za raia usilegeze! ... wenzetu wamecheza rafu na ardhi yao na sasa wanaitumbulia majicho ardhi yetu, ambayo tayari haitutoshi!
💣💣💣💀
 
Akienda huko atakuwa amevuka miiko yote ya taifa hili.

Atahesabika kuwa msaliti wa nchi hii.

Sidhani kwamba anaouthubutu wa kufanya jambo kama hilo.
 
Hizo ni Siasa zisizo tija . Zimepitwa Na wakati.Hivi Sasa ili ukuze uchumi wako unahitaji busara Na hekima
 
Nimeshangaa sana. Sijui watu hawa wanaishi dunia gani kwakweli
Mualiko gani ule wa harakaharaka. Hawakusubiri hata SSH azoee mazingira ya ikulu? Nadhani hata baadhi ya milango ya ikulu alikuwa hajaigusa bado wamesha mtuma sijui Amina nani vile maana mama yule alikuwa anaongea kwa kuhema utadhani alitembea kwa miguu kutokea Nairobi.
 
Ndo maana nasema nguvu haina maana ni akili tu inahitajika.
Kwann watumie nguvu mpaka za kijeshi wakati wana jirani mwenye ardhi nzuri na mazao bora? Ni suala la ushawishi tu, win win.
 
Time will tell. Maana hata akina Kagame, Museveni walishawashtukia wakenya. Ule umoja wao wa COW na visa yao ya pamoja ilikuwa haina manufaa zaidi kwa nchi nyingine isipokuwa Kenya. Waethiopia nao wamewakimbia walijipendekeza ili Ethiopia itumie bandari ya Lamu. South Sudan nao nikama hawana hamu nao. Sasa wanamuhai mama wamjenge ingali mapema.
 
Ndo maana nasema nguvu haina maana ni akili tu inahitajika.
Kwann watumie nguvu mpaka za kijeshi wakati wana jirani mwenye ardhi nzuri na mazao bora? Ni suala la ushawishi tu, win win.
DRC ni shamba la bibi mkuu, Rwanda imechuma mpaka imechoka. JPM waliwafungia vioo sasa wanajaribu bahati yao kwa mama. I hope ile soft tone ya mama sio uhalisia wake when comes to decision making and actions.
 
JPM was right kwa ajili ya kuwaonyesha kuwa hey ss si wa kuchezewa ila in long run hatuwezi funga vioo tu, Tutakosa hewa.
 
Eeenheee!

Na kweli, akiendelea na spidi hii ya kuelekea huko anakokwenda, "atakula bata" kweli kweli!

Jamaa wanamsoma na kumhesabia hatua tu!
Yaani ngoja tusubiri tuone itakavyo kuwa.
 
Hizo ni Siasa zisizo tija . Zimepitwa Na wakati.Hivi Sasa ili ukuze uchumi wako unahitaji busara Na hekima
"Busara na Hekima"; huku unayemwonyesha hayo akikunyonga kwa tai yako? Hizo ni akili za wapi?
 
Mleta mada mtu wa hovyo. Kila nchi inapaswa kusimamia maslahi yake! Kwa Kenya tuna maslahi pia. Badala ya kuoinga ziara, mpe mama maslahi yetu na utake yawasilishwe huko.

Jua hili, nothing lasts forever. Tusingeendelea na mabishano na tit-for-tat zilizokuwepo kipindi cha mwendazake. Hebu tuondoe chuki katika mambo ya msingi. Maslahi yetu yawekwe mbele! Hamtaki mabeberu, hata majirani hamtaki pia???
 
"Busara na Hekima"; huku unayemwonyesha hayo akikunyonga kwa tai yako? Hizo ni akili za wapi?
Mbona nyinyi mnaisaga Na kuinyonga Zanzibar ? Au mkuki ni kwa Zanzibar kwa Tanganyika ni mchungu
 
Kuna mtu wa hovyo kuliko wewe, au kwa vile hujitambui tu!

Hiyo "last forever" inakusaidia nini hata huelewi unalotetea?
We hujui kuwa hao 'mabeberu' unaowaimba wana mbinu nyingine za kuwatumia watu kama hao?

Wewe ni akili lala kwelikweli!
Watu kama wewe ndio hutupiwa kimfupa chini ulambe, halafu unakuja hapa na vimaneno maneno visivyoeleweka.
 
Shida ni pale mama anapoona mtangulizi wake hakuwa sahihi kwa kila kitu na sasa hivi anafumua mpaka visivyostahili Kenya akiwachekea atajutia badaye jamaa wanafiki sana mama Mungu akupe maarifa uwe shujaa
Twaihitaji Kenya ili Wakulima wetu wafaidike kidogo.
Bila wao wakulima wanaumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…