Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili Nchini Kenya kuanzia 04|05|2021

Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili Nchini Kenya kuanzia 04|05|2021

mama yuko vizuri sana ,she is genius ,calm and collected slow bt sure anajua anachokifanya, kuongoza nchi sio sawa na kuongoza familia, diplomasia ni muhimu sana ,na mama ameshasema "ukitaka kuenda mbali nenda pekee na ukitaka kuenda mbali zaidi nenda na wenzako"
Amna lolote ni msemo tu, dunia ya akuna cha bure bila kufanya kazi,anataka kutuletea ya awamu ya 4 ya Jk eti nisipo zurula watoto watakufa njaa maana naenda kuemea,hao Wakenya walimsumbua sana Jk kwenye utawala wake, mpaka wakawashawishi Kagame/Museven/Kinyata wakanzisha umoja wao, Mpaka bomba la mafuta lingelipitia Kenya kama asingelikuwepo Magufuri,sasa anarudi kulekule tulikotoka zamani za kuzurula tu,hatatue shida za Watanzania kwanza walionchagua,sio kuzurula hovyo,Kenya amna chochote sanasana kuwauzia nafaka tu, Wakenya walikuwa wezi wa Madini yetu baada Jpm kuingia madarakani akawapiga pini, uchumi wao umeyumba,wao ndio walikuwa wauzaji wakuu wa Tanzanate,dhahabu kuliko Tanzania, Baada ya Magufuri kufa wanatafuta pakutokea, ndio maana wameanza mialiko ya ajabu.Mama akituzingua nasi tunamzingua,asiturudishe Misri, atutaki kurudi kwenye taifa ombaomba.mungu ibariki Tanzania
Ficha ujinga wako...Mama Samia amefanya ziara kibao mikoani akiwa VP,,,hakuna asichokifahamu kuhusu hii nchi. Tumuache Mama arudishe mahusiano ya kibiashara na majirani zatu.

Mama anataka kuongeza mapato...huwezi kuongeza mapato kama hufanyi biashara kubwa na nchi zinazokuzunguka.
Biashara gani unafanya na Kenya?ukitoa biashara ya nafaka akuna biashara hapo,sana sana wanatafuta uruma kwa Samia alegeze msimamo juu ya lasilimali zetu,waanze kutufanya shamba la bibi kama enzi za Jk.
 
Ningependa sana kuamini kwamba mama na wasaidizi wake wanao ufahamu mzuri wa hali hiyo; vinginevyo tusubiri tu mvuruganyo utakaofuata kama matokeo ya 'naivity' yao.
Shida ya hawa majirani
Akatengeneze win win situation na majirani.
Kenya hawanaga hiyo "win-win" ukilegea umeumia. Niseme tu pengine Magu alikuwa extreme kwenye maamuzi yake mengi lkn linapokuja swala la ku deal na Kenya JPM model ndio sahihi na nina wish SSH amentain hilo otherwise....
 
Sijawahi hata siku moja kudhani kuwa "Tanzania inaogopa ushindani", sijui dhana hii inatoka wapi?

Ushindani si unyang'anyaji wa kutumia hila, au kuwa kituo cha unyang'anyi toka sehemu nyingine duniani.

..Lets be honest.

..otherwise we will not address the problems that we have, and will not improve ourselves.
 
Labuda anaenda kucheki na afya si mnejionea juzi alivyokuwa anakohoa kohoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ana tatizo afadhali achekiwe na Wachina - nikikumbuka jamaa hawa walivyo vunja jumuhia ya Afrika Mashariki na ku grab every mali available, Taifa letu likaachwa solemba binafsi ntakuwa mtu wa mwisho kuamini tena Wakenya.

Narudia kuwakumbusheni tena kwamba tusije kujidanganya hapa ukweli utabaki kwamba deep down Wakenya hajabadirika lolote for the better - lengo lao ni kutaka kuitumia Tanzania kwa manufaa yao binafsi na Taifa lao - hivi sasa Wakenya wapo kwenye harakati za kujaribu kuhujumu bomba la mafuta kutoka Uganda kuja Tanga, wana lobby international enviromentalists ili wajaribu kuiwekea a monkey spanner project nzima wakijidai project sio rafiki kwa mazingira/ecosystem - madai ambayo ni ulaghai mtupu, hata hydroelectric power gen complex kwenye mto wa Rufiji nayo walisha ijengea hoja eti itaharibu maelfu ya ekta za misitu na kuwafanya wanyama na raia wakose makazi - kumbukeni vile sakata la ujenzi wa barabara ya kukatiza Serengeti na Ngorongoro, Wakenya walikuwa wanaipinga kwa nguvu zao zote, wakati fulani waliwahi kuituhumu Tanzania kwamba inazuhia Nyumbu kuvuka mto Mara na kwenda kwenye mbuga ya Kenya ya Masai Mara,mambo ya ajabu sana kuhusu majirani wetu hawa!!

Bahati mbaya ni kwamba si rahisi kumchagua nani awe jirani yako, hivyo sisi kama Taifa tuna wajibu wa kuwa makini kupindukia,tujitahidi kuiishi na Wakenya kwa akili, hakuna haja ya kujikomba komba kwao - tukifanya makosa ya kushindwa kuweka mipaka kwenye masula yaomahusiano yetu hilo lita kuja ku-cost our Nation an arm and leg - forewarned...

He said "SON, take time to know her is not an overnight friend"
 
Ntatofautiana na wanaobeza hii ziara kwa wakenya, mimi naunga mkono asilimia 100 Kenya ni muhimu sana kwa uchumi wetu na sisi ni muhimu sana kwa uchumi wao.

Mkuu Ziara ni Nzuri sana Kibiashara ila Lazima Kuwa Mwangalifu na Afya zetu Corona na Janja ya wakenya

Cc: The Boss Mkuu angalia hii clip utajua wakenya Wakoje hakuna tena hakuna Mtanzania anaewajidi wakenya Ujanja hii clip ilikuwa Enzi ya Utawala wa Magu wakenya Wali bloo Angalia Clip Vizuri ni ya Mwaka jana walisema wao wenyewe kuwa Rais wai ni Mjanja mjanja sasa kakutana na kitu from Tanzania,Anakupa huku kumbe anafaidi kule...
Wakenye akikupa moja ujue anachukua 2!
Angalia hii clip utanielewa tuu!
Ndio hawa hawa wakenya wanasema Watanzania eti ni wezi sio waaminifu[emoji851][emoji851][emoji28]
Cc joka kuu Kalamu1
 
Kutengeneza diplomasia na Kenya ni jambo la Msingi sana
Kumbuka Kenya ni kiungo muhimu sana hapa EA
Ni wajinga tu wachache wanaopinga hili
Hakuna anaepinga kuhusiana na kujenga uhusiano mzuri na Kenya. Concern ya wengi ni kuwa umakini mkubwa unahitajika sana kudeal na hawa watu. Historia ibaki kuwa mwalimu na mwongozo wetu.
 
Shida ya hawa majirani

Kenya hawanaga hiyo "win-win" ukilegea umeumia. Niseme tu pengine Magu alikuwa extreme kwenye maamuzi yake mengi lkn linapokuja swala la ku deal na Kenya JPM model ndio sahihi na nina wish SSH amentain hilo otherwise....
Tukitumia akili win win ipo. Wanatuhitaji sana, dunia ya sasa ni technology na akili.
 
Nimeshangaa sana. Sijui watu hawa wanaishi dunia gani kwakweli
Hiyo dunia yako ikoje, mbona huelezi unabaki tu "kushangaa"!

Hivyo ndivyo utakavyokabiriana na dunia yenye mapambano?
 
Kutengeneza diplomasia na Kenya ni jambo la Msingi sana
Kumbuka Kenya ni kiungo muhimu sana hapa EA
Ni wajinga tu wachache wanaopinga hili

Mkuu watu hawapingi ila wanasema kuwa waangalifu tuu...
Kenya hawaaminiki...
Ni wazungu tuu ndio wanawaamini wakenya!
Angalia Clip nimeituma kwa The boss,
Kwanza wana machungu mnoo kukosa Ujenzi wa Bomba la mafuta,
 
..Lets be honest.

..otherwise we will not address the problems that we have, and will not improve ourselves.
I cannot be more honest than I have always been on Kenya; they are not competitors, they are grabbers by any means necessary.
And what's worse, they are willing to be agents of forces from outside the region to sabotage their neighbors' efforts.

We have always improved ourselves up to this point, so what's new we should expect?
 
Mwaliko uliletwa haraka haraka, kana kwamba kuna dharura!

Sasa mama ameamua kuitikia mwaliko huo wiki ijayao. Haieleweki yaliyokuwemo ndani ya barua ile iliyowasilishwa kwake Dar es Salaam yalihitaji atembelee haraka hivyo; bila shaka ni ya manufaa makubwa kwao; na pengine na kwetu pia hadi mama akaona asichelewe zaidi.

Ni mwezi juzi tu, March, hawa jamaa walipokataza mahindi ya wakulima wetu yasiende kwao kwa visingizio vya kuwa yana 'mycotoxins', uamzi waliofanya kibabe na wakustukizia, kumbe ulikuwa ni uamzi uliotokana na kulinda maslahi ya wakulima wao zaidi kuliko athari za afflatoxins..., hivi huko kwao mahindi ya wakulima wao hayana tatizo hilo!

Na huko miaka ya nyuma je, walipokuwa wakila mahindi yetu, walikufa wangapi? Sisi tunaokula hayo mahindi, miili yetu ni sugu? Uamzi huo haukuwa wa kiungwana kwa jirani unayeshirikiana naye katika biashara.

Siyo hivyo tu, hawa jamaa ni wazuri sana wa kulaumi na kulalamikia wengine huku wao wakijiona kuwa ndio kipimo kinachotakiwa kutumiwa na majirani zao.

Sukari, maziwa mayai, kuku wa Uganda wamezuia kuingia kwao wakilinda wazalishaji wao, huku wao wakihimiza Uganda inunue bidhaa kutoka kwao.

Sasa angalia wanavyomkaribisha mama atakapotembelea -

Wanaandika: Tanzania President to visit Kenya this week.

"She has the responsibility of correcting the continuous tariff between the two neighbouring countries."

Kwa hiyo ni wajibu wa mama kurekebisha, wao hawana linalowahusu!

Wakati mama Samia akitembelea huko, ni vema awe na uelewa mpana kuhusu majirani zetu hawa. Hawa tumetoka nao mbali sana, na bila shaka historia yote anaifahamu vyema.

Ni vizuri pia ajikumbushe wenzake (marais) walivyoshughulika na hawa majirani. Asije akajikuta yeye anasakamia tu toka kwa huyo mwenzake ambaye anajulikana kuwa kizabinazabina mkubwa. Hana msimamo yupo kila mahala, akijiuza na kuwachimba wenzake.
Kahangaika sana na EPA, akitaka tutumbukie tu humo kwa manufaa yake bila kujali sisi tutafaidika vipi. Anatafuta kuingia kwenye mikataba ya kibiashara na mataifa mengine, bila kujali uhusika wake katika jumuia yetu...

Bila shaka haya yatakuwa ni sehemu ya maongezi kati yao, na pengine mama naye kajiandaa ipasavyo.

Tutamsikiliza kwa makini.

====

By Aggrey Mutambo
Senior Diplomatic Writer

Nation Media Group

What you need to know:
If the visit goes ahead as planned, the Tanzanian leader will be coming to Nairobi nearly five years since her predecessor made a similar visit.

Tanzanian President Samia Suluhu is likely to visit Nairobi this week in a trip laden with diplomatic significance.

If the visit goes ahead as planned, the Tanzanian leader, who took over from John Pombe Magufuli following his death in March, will be coming to Nairobi nearly five years since her predecessor made a similar visit.

The trip was confirmed by two diplomats familiar with the arrangement.

She has the responsibility of correcting the continuous trade tiffs between the two neigbouring countries.

In a speech to Parliament last week, President Suluhu told legislators that her administration will pursue economic diplomacy with partners in the region and across the world, signaling intent to repair relations with the outside world.

“If you call it a change, then it will be a renewed effort on economic diplomacy,” she said, referring to better ties with the East African Community, Southern Africa Development Community and the recent Africa Continental Free Trade Area (AfCTA).

Collaboration
President Suluhu’s policy, she pledged, will run on a smoother domestic programme to attract investors, while sustaining relations with key partners the country trades with.

She thinks her diplomats must work better at making the country attractive rather than being an island.

“Our diplomatic staff have to be competent in striking deals in investment and trade promotion as well as seek strategic partners in tourism”, she said.

The itinerary of the planned Kenyan trip had not been made public by Saturday with officials indicating there were still final touches to be made. But the Sunday Nation understands she intends to meet with business lobbies in Nairobi, after holding talks with President Uhuru Kenyatta to discuss bilateral issues.

Renewed trust
This would be her first State visit since taking power, although she has already made an official trip to Uganda where the two countries signed a multi-billion-dollar oil pipeline deal with French oil giant Total and China’s CNOOC.

Frequent non-tariff wars with Kenya have slowed down trade to an average of Sh40 million a year, down from Sh64 billion during Jakaya Kikwete’s era.

Nairobi has indicated renewed trust in the organs of the East African Community whose secretariat is now headed by Kenyan, Dr Peter Mathuki. “We intend to sort out the issues through the established organs of the EAC,” said Johnson Weru, PS for Trade when asked on Kenya’s plan to eliminate the trade wars.

amutambo@ke.nationmedia.com

UPDATES:

Tanzania President Samia Suluhu Hassan is set to jet into Kenya Tuesday, May 4th, for a two-day State Visit.

According to @StateHouseKenya,H.E Pres. Uhuru Kenyatta will receive H.E Pres. Suluhu at State House.
Kila mara huwa nasema shule yako ni very shallow
 
Mkuu watu hawapingi ila wanasema kuwa waangalifu tuu...
Kenya hawaaminiki...
Ni wazungu tuu ndio wanawaamini wakenya!
Angalia Clip nimeituma kwa The boss,
Kwanza wana machungu mnoo kukosa Ujenzi wa Bomba la mafuta,
Acha machungu ya bomba la mafuta, ni interest yao kuona mradi wa Bagamoyo port haufanikiwi, vilevile hawapendi kuona SGR ya kwetu inakamilika kwasababu ya soko la Rwanda, Burundi & DRC. Vipi unadhani wako happy na uwepo wa ATC mpya? Vipi bwawa la umeme likikamilika na kufanya gharama za uzalishaji mali kuwa chini na pengine tukapata FDI na kuifanya nchi kuwa kivutio cha wawekezaji wa nje? Kuna mengi ya kuya protect against hawa vouchers.
 
Bi mkubwa anapasha pasha muda si muda dege litaruka USA huko.
 
Acha machungu ya bomba la mafuta, ni interest yao kuona mradi wa Bagamoyo port haufanikiwi, vilevile hawapendi kuona SGR ya kwetu inakamilika kwasababu ya soko la Rwanda, Burundi & DRC. Vipi unadhani wako happy na uwepo wa ATC mpya? Vipi bwawa la umeme likikamilika na kufanya gharama za uzalishaji mali kuwa chini na pengine tukapata FDI na kuifanya nchi kuwa kivutio cha wawekezaji wa nje? Kuna mengi ya kuya protect against hawa vouchers.
'In fact', wana hofu kubwa mno juu ya kuinuka kwa Tanzania.

Yote hayo uliyoyataja, na mengi zaidi yanayosubiri; kama mradi wa gesi ukikamilika Tanzania itakuwa ni tofauti sana na hii iliyopo sasa.

Ni viongozi wetu wakose tu akili, lakini hatuna lolote la kujitweza kwa Kenya.

Tatizo lao kubwa sasa ni kutaka kujiingiza kiaina ili wafaidike na miradi hiyo.

Kwa mfano, sasa wanajitambulisha kama "anchor nation", sijui wana'anchor' kitu gani kwa Tanzania!
 
Back
Top Bottom