Pre GE2025 Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa hadi apone, aagiza uchunguzi wa tukio hilo

Pre GE2025 Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa hadi apone, aagiza uchunguzi wa tukio hilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
hyena-pexels.jpg

Fisi nao wapewe Mifupa ya Shilingi ngapi kwa kutomla SATIVA?!
 
Aibu kubwa. Inaonesha nijinsi gani mtu hana hata tone la aibu, Sijui ni kukosa akili au uwezo wa kufikiria ndio mdogo.
Kitendo tu cha Muathirika kusema alifikishwa osterbay sikutegemea mtu kama yeye kujikosha na kutoa msaada tena matibabu.

Nilitegemea kusikia ameeanza na mkuu wa kituo cha osterbay
Kwahiyo Aanze na Mkuu wa kituo kwa maelezo ya Mtu mwenye ile Hali?

Shida ya Dogo wenu katukana Kila mtu mitandaoni akijiona yeye ni mwamba

Jifunzeni kuheshimu watu

Unakuta unabishana na Jambazi wewe ukadhani keyboarder mwezio


Mjifunze kujadili mambo kwa hoja

Jamaa Kila mtu alikua anamtukana matusi ya nguoni
 
Ningemuelewa Kama angeenda na kumwomba wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua.
Tayari majeruhi keshasema aliyekuwa na kupelekwa katakana ya osterbay.
Huu aliyofanya Zitto kabwe ni zaidi ya uchawa, amechukulia matatizo ya mwenzake Kama fursa.
Uhainkwanza
 
Rais Samia kama kweli ana dhamira anatakiwa aagize waiohusika wote wakamatwe, kwa sababu wanafahamika, siyo kuchunguza, kwa sababu wanajulikana. Isije ikawa anajikosha kwa kujua kuwa uchafu wa Serikali yake umejulikana. Tujiulize, kama Sativa angekuwa amekufa na kuliwa na wanyama, na hivyo kukosekana kwa first hand information inayowataja polisi kuhusika, huo uchunguzi kweli ungefanyika?

Yaani Serikali iliyohusika kilutaka kumwua, baada ya kunusurika, inajifanya ina huruma ya kutaka kumtibu!!

Kama Samia kweli ana dhamira njema, aagize wahusika wote wakamatwe mara moja.
Ww unayo dhamira hiyo acha jeuri
 
Huwezi Amini,,,lakini hili ni Igizo imesukwa hii baada ya muda Fulani Jamaa makazi yake yatakuwa nje ya Tz au bara la Africa
 
Sijawai mwona Rais mwenye Upendo kama huyu jamani hadi Raha mama mwenye huruma mama mwenye Upendo,ila vijana wa twita tuache kuchukua jambo hili kama vita
 
Kwahiyo Aanze na Mkuu wa kituo kwa maelezo ya Mtu mwenye ile Hali?

Shida ya Dogo wenu katukana Kila mtu mitandaoni akijiona yeye ni mwamba

Jifunzeni kuheshimu watu

Unakuta unabishana na Jambazi wewe ukadhani keyboarder mwezio


Mjifunze kujadili mambo kwa hoja

Jamaa Kila mtu alikua anamtukana matusi ya nguoni
Baada ya hao watu kutukanwa suluhisho la kumdhibiti ndio iwe kifo? hayo si matumizi yamwisho kabisa ya akili.

Hata kama dogo katukana matusi kiasi gani, kulikuwa na njia nyingine za kumpa kibano lakini sio kutaka kumuua tena kimya kimya na kama alikuwa amefanya makosa wangemkamata kwa uwazi na kutaja makosa yake Public
 
Zito kwenye harakati nzito za kuhakikisha CHADEMA inakufa😀😀😀
 
Baada ya hao watu kutukanwa suluhisho la kumdhibiti ndio iwe kifo? hayo si matumizi yamwisho kabisa ya akili.

Hata kama dogo katukana matusi kiasi gani, kulikuwa na njia nyingine za kumpa kibano lakini sio kutaka kumuua tena kimya kimya na kama alikuwa amefanya makosa wangemkamata kwa uwazi na kutaja makosa yake Public
Endelea na wewe kutukana watu matusi

Kuna mtu ukimtusi Mama yake arudii mara mbili

Nakuambia Tena huyo bwege Bado umjui

Anaweza kukutukana siku nzima matusi ya nguoni

Mimi adhabu waliyompa ni ndogo sana
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu ya Kijana Edgar Mwakabela (27) maarufu Sativa, kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa tukio lililomtokea Kijana huyo ambaye hivi karibuni alikiri kuwa alitekwa Jijini Dar es salaam June 23,2024 na kupatikana akiwa amejeruhiwa usiku wa kuamkia June 27,2024 katika Hifadhi ya Katavi.

Taarifa iliyotolewa leo July 02,2024 na Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe imesema “Jana, July 01, 2024 nimepata nafasi ya kumtembelea Kijana aliyetekwa, kuteswa kwa kujeruhia vibaya kwa risasi kwa Sativa, nimezungumza na Sativa, Ndugu zake pamoja na Watu wanaomhudumia, tangu Katavi mpaka sasa, nimeuona umoja wa kitanzania kwenye jambo hili, nawashukuru wote waliomchangia na wanaondelea kuchanga, hivi ndivyo inavyopaswa kuwa, aliyoyapitia yanaumiza na kusikitisha sana, yaliyomtokea Sativa ni lazima tuyakomeshe”

“Baada ya kutoka Hospitali, nilifanya jitihada za kumtafuta Rais wa Tanzania, kuzungumza nae, kumuelezea tukio la Sativa kutekwa, kupigwa risasi, na kutupwa msituni Katavi, pamoja na matukio mengine ya Watu kupotea, ambayo yamekithiri katika siku za karibuni, nimemueleza, yeye kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu anao wajibu wa kulinda usalama wa Raia, na kwamba matukio ya namna hii yanachafua taswira na haiba yake, na yanaondoa murua wa R Nne zake (4R's)”

“Nimemnasihi Ndugu Rais juu ya umuhimu wa yeye binafsi kuagiza ufanyike uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama ju ya tukio hili pamoja na mengine ya namna hii, kama Taifa tunahitaji kushirikiana pamoja kukomesha mambo ya Watu kutekwa, kuuawa, kupigwa na kutupwa misituni, yeye Rais anapaswa kuwa wa kwanza kwenye hili, Ndugu Rais amenisikiliza, na ameahidi kufanyia kazi ushauri wangu kwake”

“Kama hatua ya awali amenieleza kuwa yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu ya Sativa, kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa, pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa jambo hili, ninamshukuru Ndugu Rais kwa mwanzo huu, kila safari ndefu, inaanza na hatua ya kwanza, naamini sasa tutaanza safari ya kwenda kule tunakotaka, ambako tabia za kutekana zitakomeshwa”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi milioni 35 kwa ajili ya matibabu ya Edger Mwakabela maarufu Sativa ambaye anapatiwa matibabu katika hospitali ya Aga khan baada ya kupitia masaibu ya kutekwa na kuteswa.Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa kupitia chapisho lake la karibuni alilolitoa katika ukurasa wake wa mtandao wa X (Twitter) ambapo amemshukuru Rais Samia kwa kutimiza ahadi kwa kulipia gharama za awali za matibabu ya Sativa."Tumepokea nakala ya malipo kiasi cha 35 milion kwenda Agakhan Hosptali.

Leo (Julai 02, 2024) jioni Sativa atafanyiwa upasuaji. Hizi ni gharama za awali tuombe kila kitu kiende sawa na gharama zisiwe kubwa huko mbele. Kuna faida kubwa kwa Mhe Rais kuweka mkono wake katika hili. Hii ni salamu kwa walioko nyuma ya swala hili" Ameandika Olengurumwa.Aidha ameeleza kuwa na tumaini na ushauri walioutoa kama THRDC wa kuundwa kwa tume huru itakayochunguza tukio lililomtokea Sativa huku akiwashukuru wadau waliosimama mstari wa mbele katika kuhakikisha Sativa anapata huduma bora kama vile Kiongozi Mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao ni Martin Masese na Boniface Jacob ambao walihakikisha taarifa za kupotea kwa Sativa zinajulikama ndani ya majukwaa ya kimitandao na nje ya majukwaa.
Pia soma

Kupokea msaada wake itakuwa sawa na kumkufuru Mungu aliyemponya kijana huyo kuliwa na fisi kama watekaji wa serikali ya Samia walivyotaka
 
Wanaendelea kutafutwa.,Wala haihitaji Rais kuamuri maana wenye wajibu huo kisheria wapo.

Kwani waliomuua mtoto Albino ni Rais aliamuru? Si ni Polisi wenyewe wanafahamu wajibu wao kisheria au?
Kwahiyo ukumuona huyo mama yako akitoa maagizo mbele ya vyombo vya habari kwamba amesikitishwa na vyombo vya usalama vihakikishe waliomteka mtoto albino wakamatwe, mbona la sativa kapiga kimnya katangaza msaada tu ina maana hajui mtuhumiwa no 1 ni muriro!?
 
Kwahiyo ukumuona huyo mama yako akitoa maagizo mbele ya vyombo vya habari kwamba amesikitishwa na vyombo vya usalama vihakikishe waliomteka mtoto albino wakamatwe, mbona la sativa kapiga kimnya katangaza msaada tu ina maana hajui mtuhumiwa no 1 ni muriro!?
Hata Sasa amesikitishwa ndio maana amewachangia pesa za matibabu na Waziri wa Mambo ya ndani amesema Uchunguzi unaendelea wa kuwasaka wahusika.

Sasa hapo wewe unataka nini?
 
Hata Sasa amesikitishwa ndio maana amewachangia pesa za matibabu na Waziri wa Mambo ya ndani amesema Uchunguzi unaendelea wa kuwasaka wahusika.

Sasa hapo wewe unataka nini?
Huyo waziri aliyesema serikali isiusishwe na tukio wewe ni maiti inayotembea kuna uchungizi hapo?
 
Back
Top Bottom