Pre GE2025 Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa hadi apone, aagiza uchunguzi wa tukio hilo

Pre GE2025 Rais Samia kugharamia matibabu ya Sativa hadi apone, aagiza uchunguzi wa tukio hilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
..aunde Tume ya Kijaji itakayochunguza tukio zima, na mengine ya aina hiyo.
Hivi nyie hamuoni usanii kwenye haya maelezo.
1. Eti rais wa nchi hajui habari ya kinachoendelea kwenye nchi yake pasipo kuarifiwa na kiongozi wa chama kingine
2. Eti rais wa nchi siyo kama tu hajui, bali hajui afanye nini, mpaka akumbushwe kuwa yeye kama amir jeshi ana wajibika kuchukuwa hatua.
Da, kweli Tanzania ni nchi ya vituko na usanii.
 
Angeliwa na Fisi wangenyamanza kimya kama sio wao.
Hii ni serious kesi na ilitakiwa ijulikane kimataifa ila ni tatizo ni kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari. Karne ya leo unakuta watu wanapanga kulisha fisi mzoga wa binadamu tena kwa kumuua?
 
Naunga mkono hoja. Ifikie wakati tuwe wastaarabu. Wahusika wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Tukio la yule mtoto aliyeuwawa kule Bukoba lilichukua siku chache tu kwa watuhumiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Sioni ni kwa nini katika hili tukio, nguvu kubwa inataka kuwekezwa kwenye matibabu pekee, huku kukiwa hakuna habari yoyote ile ya kuwahusu watuhumiwa wa tukio. Au ndiyo muendelezo ule ule wa tukio la kutekwa na kuteswa kwa Dr. Ulimboka! Kushambuliwa kwa Tundu Lissu, nk?
Haya maneno ''ifike mahali blah blah.......'' ndiyo yanaimaliza Tanzania. Hiyo ''mahali'' haitakaa ifikiwe kwa maneno. Kla kitu utasikia ''ifike mahali...'''. Kwanza hili tamko la Zitto ni usanii mtupu. Ni njia ya kuzima huu ukatili kwa maneno na ahadi. Rais angekuwa anajua wajibu wake asingesubiri mpaka akumbushwe na Zitto anawajibika kufanya nini. Na nina uhakika kuwa huyo jamaa alikuwa amevaa nguo za timu ya Simba ambaye ndiye mhusika mkuu, angejua Samia hapendi huu unyama basi asingethubutu kuamrisha binadamu mwenzake auawe na kulishwa fisi.
 
Mwenye wimbo wa afande sele unaoitwa darubini kali atuwekee baadhi ya vipande vyake......
 
Back
Top Bottom