Rais Samia kuisimamisha Dunia kutokea Cuba hapo Kesho

Kwa hiyo dunia nzima ikiongozwa na Trump itakuwa ina bubujikwa na machozi ya furaha?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mwashamba anautafuta Ukuu wa Wilaya na ameweka malengo kweli.
 
Mkubavu mkubwa
 
Kwanini usiandae andiko zuri ambalo litaeleza yafuatayo:
1. Serikali ifute hadhi ya Baba wa taifa na Sa100 awe ndo Mama wa Taifa.
2. Tanganyika iwe koloni rasmi la Zanzibar na jina libadilishwe liwe Jamhuri ya Zanzibar.
3. Uelezee uchaguzi hauna maana kwa kuwa Sa100 ni mungu mtu.
Ukifanya hivi mkuu hakika mkeka unaokuja lazma jina lako liwepo
 
Unadhani dunia ni basi la mwendokasi au daladala ya mbagala!?
πŸ˜‚πŸ€£

Raisi anatokea matakoni mwa dunia huku, kila jambo msaada mpaka tundu za choo za shule, akasimamishe dunia. πŸ˜‚πŸ€£
Akili nyingine iliyokufa hii hapa!
 
06 November 2024
Rais wa Tanzania atakutana na DΓ­az-Canel katika ziara ya kiserikali nchini Cuba

Nov 6 (EFE).- Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anasafiri kwenda Cuba Jumatano hii kuanza ziara ya kiserikali ambapo atakutana na mwenzake wa Cuba, Miguel DΓ­az-Canel, pamoja na ahadi nyingine, imeripotiwa. Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hii ya Afrika Mashariki.

Ziara ya Hassan inalenga kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili, ikilenga mahsusi katika kukuza matumizi ya kimataifa ya Kiswahili, mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazotumiwa sana barani humo, yenye wazungumzaji zaidi ya milioni 200 duniani.

Rais Hassan na rais wa Cuba
DΓ­az-Canel wanatarajiwa kushughulikia masuala kama vile ushirikiano mpya wa kiuchumi na kidiplomasia ili kutatua changamoto za kimataifa kwa manufaa ya pande zote mbili.

Pia watachunguza mikakati inayolenga kufungua njia mpya za ushirikiano wa vyama vya ushirika katika maeneo kama vile afya, elimu, sanaa, michezo, utalii na uchumi wa bluu, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania.

Moja ya matukio muhimu katika kipindi cha rais Hassan itakuwa mahudhurio yake kama mgeni mkuu katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kiswahili mjini Havana Ijumaa hii, siku ya mwisho ya safari yake.

Mkutano huo ulioandaliwa na balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ni sehemu ya mpango wa kuhamasisha matumizi ya Kiswahili katika nchi za Caribbean na Amerika Kusini.

Takriban watu 400 wanatarajiwa kuhudhuria, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Tanzania.

Marais Hassan na DΓ­az-Canel pia watawasilisha kamusi mpya ya Kihispania-Kiswahili na kijitabu cha methali za kawaida katika lugha zote mbili, kilichotolewa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM na Chuo Kikuu cha Havana. EFE
 
Ashukuriwe Samia kwa ushindi wa Trump.
Nani kama mama?!....CCM wamefundisha Trump jinsi kushinda uchaguzi......
 
Duh,
Yaani dunia waache kufuatilia ushindi wa Trump wakusikilize wewe chawa na waliokununua kuwatumikia?!
Hata akienda USA unakuta hata rais wa USA mwenyewe hajui kama kuna rais wa nchi fulani ya Afrika yuko nchini kwake. Watu wako busy na kushughulika na masuala muhimu ya watu wao. Ni watawala wa Afrika pekee ndio unawakuta wanaona ufahari kusafiri safiri nchi za watu.
 
Dogo nchi imefirisika tanroads wasimamizi wa miradi mikubwa wako hoi
Wakandarasi wazabuni wa vifaa na washauri wa miradi (consultants) hawajalipwa Miaka 2bsasa

Ccm baada ya kuona nchi Haina mapato ya kutosha kugharamia miradi mnamtumia kitila kuuambia mtatumianmfumo wa PPP ambaobutawanyonya zaidi wanyonge wenu

Kwani pamoja na kulipa Kodi sasa tutawalipa wawekezaji kupitia barabarani

Alafu mjinga mjinga chawa
Unatuletea upuuzi wa kusifia mambo ya kijinga
 
Acheni porojo na uzushi wa kitoto
 
Hahahaah mamilioni ya watu duniani kote yanasubiria kongamano la kiswahele! πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜›

Na dunia isimame kumsikiliza mama yetu! Haijasimama kusikilizia rais wa dunia anachaguliwa then isimamishwe na kikongamano cha polepole kisiwani Cuba, hahaha
 
Hahahaah mamilioni ya watu duniani kote yanasubiria kongamano la kiswahili! πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜›

Na dunia isimame kumsikiliza mama yetu! Haijasimama kusikilizia rais wa dunia anachaguliwa then isimamishwe na kikongamano kisiwani Cuba, hahaha
Wivu utakuuwa ndugu yangu
 
Hiyo ziara ya Cuba haina tija kwa taifa huwezi ukawasikia marais smart na wazalendo kwa nchi zao kama Kagame au Ruto ameenda kupoteza muda huko!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…