Rais Samia kukopa(tena) 1billion USD from IMF

Tusiogope kukopa, deni haliui, kinachoniuma mimi ni matumizi ya anasa ya Serikali - ma V8 za nini ? kwa nini tusitumie Suzuki na R4 tena kwa watumishi wachache tu wengine wajitegemee usafari.
 
Kwetu kumekucha mimi wala sina shida na wewe nimeshakuelewa ipo sio siyo ya mbali utalaumu yale yale aliyokuwa akifanya Magufuli usiempenda sema kwa sasa uelewi utekelezaji wale.

👋
 
Kwetu kumekucha mimi wala sina shida na wewe nimeshakuelewa ipo sio siyo ya mbali utalaumu yale yale aliyokuwa akifanya Magufuli usiempenda sema kwa sasa uelewi utekelezaji wale.

👋
Nilaumu kwa lipi? Magufuli aliharibu uchumi kwa kuvuruga private sector,FDI na kudanganya kwamba hakopi wakati anakopa tena kwa riba kubwa na ufisadi juu kwa hiyo hafai kabisa na kulaumiwa ni haki yake 👇







 
Tatizo sio kukopa bali hiyo mikopo inatumikaje? Nchi inakopa pesa mwisho zinaingia kwenye mifuko ya wanasiasa.
 

Amekopa ili aweze kuongeza mishahara aliyoahidi, hakuna pesa hazina wameshamaliza akiba yote walioikuta.

Kwa kifupi anakopa ili kuendesha Serikali, hakuna pesa!
 
Wacha akope. Kinakuuma nini sindio tumemchaguwa atuwakilishe na wazee wakasema anafaa yani wacha akope tu. Tupunguze domo
 
mkuu stimulus loan for whom? raia wanachechemea na kujiangukia ovyo kwa njaa na kukosa ajira wakitaabishwa na tozo na bei kali ya petrol hebu tusaidie maelezo hiyo loan inawakwamuaje!! hivi sisiem huwa hawakai vikao kuhoji mikopo ya serikali?
Haya mambo hayatakiwi yapelekwe kiasiasa, sasa wachumi wenyewe ndo hao akina madelu ndo unaona mambo ni shaghalabaghala....
 
upigaji halmashauri hautoisha.mbona hapa bukoba ukarabati wa jengo la mkuu wa wilaya unasuasua ati sababu wameshtukiwa na mkuu wa wilaya kuzipiga.waliweka bajeti kubwa ya ukarabati tofauti na uhalisia wake na waliposhtukiwa na mkuu wa wilaya bukoba mjini wanapita mtaani kusema ati ngoja akae kwenye kile kiofisi pale uwanja wa ndege mpaka akome.wapigaji nchi hii ni wengi kutoka juu mpaka chini wamejaa wapigaji tu hasa kipindi hiki cha mama.
 
Amekopa ili aweze kuongeza mishahara aliyoahidi, hakuna pesa hazina wameshamaliza akiba yote walioikuta.

Kwa kifupi anakopa ili kuendesha Serikali, hakuna pesa!
Ndivyo kakuambia au? Acha ujinga wako..

Hao wamekuja kwa ajili ya majadiliano na bahati nzuri Serikali ya SSH huwa inasema.

Kwa.hiyo.subiria ikiwa tayari watasema.
 
Wacha akope. Kinakuuma nini sindio tumemchaguwa atuwakilishe na wazee wakasema anafaa yani wacha akope tu. Tupunguze domo

Nani kamchagua? Mimi siyo labda wewe, mimi raisi wangu wa mwisho niliyemchagua alikuwa Magu (RIP)!
 
Wacha akope. Kinakuuma nini sindio tumemchaguwa atuwakilishe na wazee wakasema anafaa yani wacha akope tu. Tupunguze domo
mama hajachaguliwa ni matakwa ya kkatiba jamani mbona mnapotosha?
 
Tusiogope kukopa, deni haliui, kinachoniuma mimi ni matumizi ya anasa ya Serikali - ma V8 za nini ? kwa nini tusitumie Suzuki na R4 tena kwa watumishi wachache tu wengine wajitegemee usafari.
Naunga mkono hoja 100% ! Hata L/cruiser hard top zinafaa sana lakini watu wameshajizowesha KAZI NA BATA !! Wengine wanataka Chopa !!
 
Hiyo itakuwa ni stimulus loan kwa ajili ya kusawazisha hali ya kiuchumi.......muhimu ni hiyo mikopo kutumika kuleta tija zaidi.
Haitakuwa na tija yoyote, watu watagawana kiujanjajanja tu kisingio kikiwa hicho hicho covid 19 recovery.
 
Dah jamaa unanibishia bila kujua tu. Hela zimechapishwa sana kulipa wanunuzi wa ndani wa bond za serikali. Sina haja ya kubishana na wewe maana najua ninachoongea. Taarifa zinazotolewa public ni tofauti sana na uhalisia.

Pia mimi huyo Samia sioni kama anao uwezo wa kuongoza nchi hivyo usinihusishe naye.
 
Nchi masikini hii mikopo itumike ipasavyo.
 
Mkuu mimi nimeshasema Samia hana uwezo wa kuongoza nchi na Magufuli pia alikuwa hivyo hivyo. Tatizo kuanzia awamu ya 5, kaua biashara na uzalishaji wa ndani na matokeo yake vyanzo vya mapato vikapungua na matokeo yake ni kukopa kila siku ili kuendesha serikali na kujenga.

Samia ni mtapanyaji hivyo kudhibiti bei hataweza. Walichotakiwa kufanya kwenye mafuta ni kuondoa utitiri wa kodi na kupunguza matumizi ya serikali ili kufidia. Hivi gesi ya kwenye magari inachimbwa hapa? Ufahamu wangu sio mkubwa sana kwenye hili maana recently nimesikia hizi gesi za kupikia mitaani sio zinazochimbwa hapa. Halafu bei ya gesi ni ndogo kwasababu watumiaji ni wachache, wakiwa wengi wataweka Tena utitiri wa kodi na tutarudi palepale.

Magufuli amekopa hovyohovyo pia, ujenzi kuanzia zahanati, masoko, viwanja vya ndege, reli na bwawa vyote ni mikopo huku kwenye majukwaa anadanganya kwamba ni hela za ndani. Ninaunga mkono kukopa kwa ajili ya bwawa na reli ila mikopo mingine iwe ile inayochochea uzalishaji wa ndani na kuboresha export.
 
Vipi kuhusu exchange rate kwa Magufuli hela yetu imekuwa stable sana! Magufuli was better maana alikopa na vitu vinaonekana in ground!
Ukiwa unakopa na kupokea hela nyingi za kigeni kama mikopo unategemea currency yako isiwe stable?
 
Hizo hela alizichapishia wapi hadi iwe siri kwa dunia? Na aliziingiza vipi kwenye vitabu vya serikali kwa situ kubalance vitabu au unadhani unaweza kuiongopea dunia kwenye deni lako la ndani.

Huwa mnaishi kwenye dunia yenu na kudhania kila kitu ni kujiropokea tu kama mpo uwanja wa mwembe yanga.

Unajua madhara ya kuchapisha hela au unajiongelea tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…